Nigeria,Mauaji ya Noeli:Hasira ya watu inaweza kutulizwa tu kwa kuwapatia haki
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Askofu Mkuu Alfred Adewale wa Jimbo Kuu katoliki la Lagos, akihutubia mbele ya Rais wa Nigeria Bola Tinubu kwa kuomba haki kwa waathiriwa wa mauaji ya Noeli katika Jimbo la Plateau alisema: “Waathiriwa wa uhalifu huu wanataka kuona hatua za kweli za kuleta haki kwa wapendwa wao. Hasira ya watu inaweza kutulizwa, tu ikiwa wale wanaoonekana kuwa na hatia watafikishwa mbele ya sheria.” Katika taarifa yake, Askofu Mkuu wa Lagos alisisitiza kwamba yote ambayo serikali imefanya hadi sasa ni kulaani mauaji na kutoa ahadi ambazo hazijatekelezwa, na kuchochea hasira na kuchanganyikiwa kwa Wanigeria. “Mazungumzo yanaanza kuonekana kama rekodi iliyovunjwa, na watu wanachukua ahadi kama hizo kwa chembe ya chumvi kwa sababu hakuna mtu ambaye amesikia mtu yeyote kupelekwa mahakamani au kuhukumiwa kwa uhalifu huo mbaya.
Wahusika wa mauaji hayo ni wakina nani
Hatuwezi kuruhusu hili liendelee,” alisema Askofu Mkuu Martins. “Tunataka kujua wahusika na wachochezi wao ni akina nani. Hadi haya yote yanatokea, maoni ya jumla ni kwamba wenye hatia wanalindwa na nguvu zenye nguvu ndani na nje ya mzunguko wa serikali.” Katika mashambulizi yaliyofanywa usiku wa mkesha wa Noeli na katika siku zilizofuata katika maeneo ya Bokkos na Barkin Ladi, magenge yenye silaha yalishambulia karibu vijiji 20, na kuua watu wasiopungua 198, kulingana na mamlaka katika Jimbo la Plateau. Vurugu hizo pia ziliwalazimu maelfu ya watu, wengi wao wakiwa Wakristo, kukimbia. Hata hivyo, miongoni mwa wahanga kutakuwa pia na wachungaji wa wanyama thelathini wa Kiislamu kama ilivyotangazwa Dominika tarehe 7 Januari 2024 katika mkutano na waandishi wa habari na muungano wa makundi ya wachungaji wa wanyama Kiislamu katika jimbo la Plateau.
Waandamanaji karibia 5,000 walishiriki maandamano tarehe 8 Januari
Mnamo tarehe 8 Januari 2024, Chama cha Kikristo cha Nigeria(CAN),chama kinacholeta pamoja madhehebu makubwa ya Kikristo ya Nigeria, kiliendeleza maandamano ya amani katika mitaa ya Jos, mji mkuu wa Jimbo la Plateau, ili kuomba usalama zaidi katika eneo hilo. Takriban waandamanaji 5,000 walishiriki katika maandamano hayo. Rais wa chama(CAN,)Daniel Okoh, alitaja mashambulizi na uharibifu wa nyumba na maeneo ya ibada kuwa mashambulizi dhidi ya amani na umoja wa watu wa Jimbo la Plateau. Okoh alihakikisha kuwa(CAN)itasalia pamoja na watu na taasisi za serikali katika wakati huu mgumu. Rais wa(CAN)alipongeza uingiliaji kati wa haraka wa gavana wa jimbo hilo, Caleb Mutfwang, na jeshi la Nigeria, akiwataka kuimarisha hatua za usalama ili kuzuia mashambulizi mapya katika eneo hilo. Polisi wa Nigeria walisema wamewakamata watu 11 wanaotuhumiwa kushiriki katika mashambulizi hayo.