Mikutano ya Mtakatifu Francis wa Sales huko Lourdes
Benedetta Capelli–Lourdes na Angella Rwezaula-Vatican.
Chini ya vazi la Bikira Maria huko Lourdes Ufaransa katika kumbukumbu ya Mtakatifu Francis wa Sales, Msimamizi wa waandishi wa habari na wahariri wapatao 250 kutoka duniani kote wanakutana huko kuanzia tarehe 24 hadi 27 Januari 2024 katika Toleo la Mikutano ya kimataifa ya Mtakatifu Mtakatifu Francis wa Sales. Ni mikutano iliyoandaliwa na Shirikisho la Vyombo vya Habari vya Kikatoliki vya Ufaransa kwa ushirikiano na Baraza la Kipapa la Mawasiliano, SIGNIS (ni harakati ya kikanisa la walei kimataifa, kwa ajili ya wataalamu katika vyombo vya habari vya mawasiliano, ikiwa ni pamoja na vyombo vya habari, radio, televisheni, sinema, video, elimu ya vyombo vya habari, intaneti, na teknolojia mpya) na Umoja wa Kikatoliki wa Vyombo vya Habari vya Italia.
Toleo linawatia moyo wahusika wa mawasiliano
Hili ni toleo linalotaka kuwatia moyo wale wanaohusika katika mawasiliano kuhusu “Wakati wa misukosuko” ambayo ni mada ya siku hizi hadi siku ya Ijumaa tarehe 27 Januari 2024. Akili Mnemba(Artificial Intelligence)na Sinodi ya kisinodi ni misisitizo miwili inayohakishi hata hivyo ukweli wa mikutano hiyo. Kwa mujibu wa Xavier Le Normand, mratibu wa programu ya Mikutano aliuliza swali kuwa: “Vina uhusiano gani?”, jibu alisema si dhahiri kwa sababu inaonekana hakuna kitu kinachowafunga japokuwa ni mada zinazotikisa mazoea na dhamiri. Kimsingi mada hizi ni uchochezi unaowapa changamoto waandishi wa habari kwa sababu wanafanya kazi kwenye vyombo vya habari na kwa sababu ni Wakatoliki. Kinachoongezwa kwa hili ni wasiwasi wa mzozo wa Ukraine na vita kati ya Israel na Kundi la Hamas la kipalestina, hali ambazo waandishi wa habari, wanaporipoti juu ya kile kinachotokea, hawasamehewi kuhatarisha maisha yao.”
Kufunguliwa 24 - 27 Januari
“Mikutano hiyo imefunguliwa tarehe 24 Januari 2024 kwa Ibada ya Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mama Bikira Maria wa Louredes katika, njia ya kuanza hija ya waandishi wa habari chini ya ulinzi wa Mama Maria, kwa kumkabidhi utajiri na hatari ya taaluma, lakini pia kuomba mwanga kwa usahihi katika wakati huu wa machafuko." Hiyo imetafuatiwa na kikao kinachohusu jukumu la vyombo vya habari katika kukabiliana na vita. Siku ya Alhamisi tarehe 25 Januari 2027 tafakari hiyo itazingatia matumizi ya Akili Mnemba(AI) na masuala ya maadili yanayotokana nayo. Itajadiliwa na waandishi wa habari waliobobea katika teknolojia ya kidijitali, wataalam ambao wamesaidia makampuni katika maendeleo ya Akili Mnemba (AI) na pia Mathieu Guillermin ambaye, katika Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican, aliwasilisha ujumbe wa Papa Francisko kwa Siku ya Amani Duniani mnamo Januari 1 ukilenga hasa Akili Mnemba. Pia itafuta hotuba ya Alessandro Gisotti, naibu mkurugenzi wa wahariri wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano ambaye atatafakari juu ya jukumu la vyombo vya habari katika mchakato wa sinodi. “Je, ChatGPT ina nafasi katika vyumba vya habari?” ni swali ambalo mwandishi wa habari wa Ufaransa Cécilia Gabizon atajaribu kujibu.
Tuzo ya Padre Hamel kwa washindi katika tasnia ya uandishi
Alasiri ya Alhamisi, tarehe 25 Januari 2024, Askofu Mkuu Celestino Migliore, Balozi wa Vatican nchini Ufaransa tangu 2020, anayejivunia utume wa muda mrefu katika diplomasia ya Vatican, atazungumza. Hata hivyo aliwao kuwa Katibu Msaidizi wa Mahusiano ya Vatican na Nchi na Mashirika ya kimataifa kuanzia 1995 hadi 2002, kabla ya kuteuliwa kuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Umoja wa Mataifa. Baadaye alishikilia nafasi ya Ubalozi wa Vatican nchini Poland, Urussi na Uzbekistan. Yeye ndiye atakayewasilisha tuzo ya 2024 ya Hamel iliyotolewa kwa Sarah-Christine Bourihane, kwa makala yake Captive et libre, iliyochapishwa Le Verbe mnamo Machi-Aprili 2023, ambamo anasimulia Historia ya mtawa kutoka Shirika la (Notre- Dame) Mama Yetu ambaye alisafiri hadi Afrika na kupita shida kubwa wakati wa utekaji nyara wake, akiungwa mkono na imani tu.
Mwandishi wa habari wa Kiitaliano Romina Gobbo pia alitunukiwa kwa makala yake ya Malaika wa Wanawake, iliyochapishwa mnamo Septemba 2023 katika jarida la Italia liitwalo Messaggero di Sant'Antonio, Padova, akizingatia sura ya Daktari Denis Mukwege, wa Congo,(DRC) anayejishughulisha na magonjwa ya wanawake, mwanzilishi wa Hospitali ya Panzi huko Bukavu, (DRC) ambapo wanawake waathriwa wa kubakwa kama silaha ya vita wanatibiwa. Mnamo 2018, Dk. Denis Mukwege alipokea Tuzo ya Amani ya Nobel pamoja na Nadia Murad. Tuzo ya Hamel ilizaliwa mnamo mwaka wa 2017, mwaka mmoja baada ya kifo cha Padre Jaques, aliyeuawa katika Kanisa lake huko Mtakatifu -Étienne wa Rouvray tarehe 26 Julai 2016 mikononi mwa wafuasi wawili wa Kiislamu. Utambuzi huo unakusudia kutuza kazi ambazo zimeangazia mpango unaopendelea amani na mazungumzo ya kidini. Siku ya mwisho ya Mikutano ya Kimataifa ya Mtakatifu Francis wa Sales, Ijumaa tarehe 26 Januari 2024, itajikita katika hitaji la kanuni za usimamizi wa Akili Mnemba (AI), lakini Sinodi bado itajadiliwa kama chombo cha kuponya migawanyiko iliyopo ndani ya Kanisa.
Mtakatifu Francis wa Sales
Mtakatifu Fransisko wa Sales alizaliwa tarehe 21 Agosti 1567 huko Lyon, Ufaransa, 28 Desemba 1622 na alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki kwa jimbo la Geneva (Uswisi). Ni Mtakatifu anayejumusiha undano wa matunda bora ya karne XVI, na ni kati ya watu muhimu zaidi katika Marekebisho ya Kikatoliki na katika Taalimungu ya maisha ya kiroho. Mchungaji halisi, aliyerudisha katika Kanisa Katoliki Waprotestanti wengi, na kuwafundisha kwa maandishi yake Wakristo wamheshimu na kumpenda Mungu. Pamoja na Yoana Fransiscaw wa Chantala alianzisha shirika la Hija. Kwa ajili hiyo anaheshimiwa kama mtakatifu na mwalimu wa Kanisa. Pia kama msimamizi wa waandishi wa habari, watunzi na wanafasihi, magazeti ya Kikatoliki, bubu na viziwi. Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 24 Januari yak ila mwaka.
Sala ya Mtakatifu Francis wa Sales
Ee Mungu wangu, ninakutolea siku hii. Ninakutolea sasa mema yote nitakayotenda na ninakuahidi nitapokea kwa upendo wako magumu yote yanayonikabili. Unisaidie kuenenda siku hii namna inayokupendeza. Ee Bwana, mimi ni wako, tena ninatakiwa kuwa wako tu, si kwa mwingine yeyote. Roho yangu ni yako, nayo inatakiwa iishi kwa njia yako tu. Utashi wangu ni wako, nao unatakiwa kupenda kwa ajili yako tu. Ninapaswa kukupenda kama asili yangu kuu, kwa kuwa ninatoka kwako. Ninapaswa kukupenda kama lengo na pumziko langu, kwa kuwa nipo kwa ajili yako. Ninapaswa kukupenda kuliko nafsi yangu, kwa kuwa nafsi yangu inatoka kwako. Ninapaswa kukupenda kuliko mimi mwenyewe, kwa kuwa uzima wangu ni wako na ndani yako. Amina.