Vijana wa Korea kusini. Vijana wa Korea kusini. 

Seoul,Korea Kusini wasali kwa ajili ya Mapatano ya Nchi mbili

Mungu nifanye niwe chombo cha amani ni wito kwa wakatoliki wa Korea Kusini kwa ajili ya kuombea maridhiano ya nchi mbili.Jumanne tarehe 9 Januari 2024,ikiwa ni mwaka wa 29 baada ya misa ya kwanza,ya adhimisho la Ekaristi Takatifu la 1400: “Tunawasihi katika jina la Kristo:mpatanishwe na Mungu(2Kor,5,20).

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Tangu tarehe 7 Machi 1995, walianza maadhimisho ya Misa ya amani na upatanisho kwa watu wa Korea mbili kuendelea  bila kukatizwa kila Jumanne katika Kanisa Kuu la Myeongdong, jijini Seoul. Ilikuwa  mnamo tarehe 7 Machi 1995 hasa wakati ambapo Kadinali Stephen Kim Sou-hwan, wakati huo akiwa ni Askofu mkuu wa Seoul na msimamizi wa kitume wa Pyongyang, alipozindua mpango ambao ulikabidhi hatima ya peninsula kwa Mungu kwa njia ya sala ya juu zaidi. Misa ya Ekaristi haijawahi kuachwa kuendelea mbele, katika vipindi ambavyo uhusiano wa Kaskazini-Kusini ulionekana kuimarika na wakati wa mvutano na umbali kati ya serikali.

 Misa ya 1400 tangu 1995,Mpango wa maridhiano

Kwa njia hiyo hata Jumanne tarehe 9 Januari 2024, ikiwa ni mwaka wa 29 baada ya misa ya kwanza, ya adhimisho la Ekaristi Takatifu la 1400 lilifanyika, na kuwa kuwa na mwaliko uliochukuliwa kutoka katika barua za Mtakatifu Paulo: “Tunawasihi katika jina la Kristo: mpatanishwe na Mungu (2Kor, 5, 20). “Tunamwomba Mungu alete amani ya kweli na upatanisho katika peninsula ya Korea, ambako mivutano inaongezeka,” ilisisitiza kamati, ikikumbuka kauli mbiu inayorejeea uwepo wa waamini wa Kikatoliki huko Korea Kaskazini, zamani na sasa: “Kwakuwa tunawakumbuka wako hai. Kwakuwa tunasali kwa ajili yao, sala yetu itasikilizwa. Ni mpango wa kwanza na muhimu wa upatanisho wa kiroho uliohamaishwa na Jumuiya ya Wakatoliki wa Korea mwaka 2024, ambao Askofu Mkuu wa Seoul, Peter Chung Soon-taick, alikaribisha katika ujumbe wake kwa waamini, akitumaini kwamba neema na baraka za Mungu, ambaye amewapatia zawadi ya mwaka mpya, iwajaze maisha kila mtu. Aidha alisema kwa uchungu kwamba: “katika siku za hivi karibuni ulimwengu umetiwa alama na wimbi la migogoro na jeuri isiyo na kifani. Katika nyakati kama hizi wanasihi kwa dhati uingiliaji kati wa Mungu ili kuleta utulivu katika ulimwengu wetu, wakati huo huo tukijitolea katika kutafuta amani katika nyanja yao binafsi.”

Kwa wale wote wanaotafuta amani, tunaweza kuanza tena kutoka kwenye dhana iliyopendekezwa katika Sinodi ya Maaskofu hivi karibuni, iliyozungumzia “ushirika, ushiriki na utume.” Ili kufuatilia na kuendeleza amani, alisema Askofu Chung Soon-taick, ni lazima “kukuza ushirika na Bwana, na majirani zetu na sisi wenyewe; kumwilisha utume kwa kuishi mantiki ya Injili kinyume na mantiki ya ulimwengu; kuinua ushiriki hadi kiwango ambacho wakaaji wote wa ulimwengu hukusanyika kama wahusika wakuu katika maisha ya pamoja.” Mtazamo wa Kanisa Katoliki la Korea, ambalo linasimama pamoja na Makanisa ya madhehebu  mengine, ni kukuza amani kwa harakati kutoka chini kwenda juu.” Askofu pia alikumbusha kwamba, Kanisa la Korea Kusini liliadhimisha misa ya amani katika kumbukumbu ya miaka 70 ya usitishaji wa silaha wa Vita vya Korea, tarehe 27 Julai 2023. Katika maadhimisho hayo, “Baba Mtakatifu Francisko alituma ujumbe na kubariki Peninsula ya Korea, ambao ulitutia moyo kuwa manabii wa amani.

Papa alitumaini uwepo wa vifungo vya udugu

Pia katika ujumbe wa ‘Urbi et Orbi’ kwa wakati wa Noeli ya  2023 - Askofu aliendelea – “Papa alitumaini kwamba siku inakaribia ambapo vifungo vya kidugu vitaimarishwa kwenye peninsula ya Korea, kufungua njia za mazungumzo na upatanisho ambao unaweza kuunda mazingira ya amani ya kudumu. Sasa  ni wakati wa kuacha chuki na kufuata njia iliyooneshwa na Yesu. Tuombe pamoja ili tuweze kuwa mitume wa kweli wa amani,” alihitimisha Askofu Koo. Kwa nia hiyo mapokeo ya adhimisho hili maalum la Ekaristi ilianzishwa tarehe 7 Machi 1995 kwa misa ya kwanza ya upatanisho iliyoadhimishwa na Kardinali Stephen Sou-hwan Kim, wakati huo Askofu Mkuu wa Seoul na Msimamizi wa Kitume wa Pyongyang. Hapo mwanzo, maaskofu na mapadre wa Seoul walisherehekea misa kwa zamu. Kuanzia mwaka wa 2000, mapadre wapya waliowekwa wakfu katika jumuiya walisimamia Ekaristi. Tamaduni hiyo imeendelea kwa miaka 29, kila Jumanne saa 1 jioni, tu na usumbufu mfupi kwa sababu yajanga la uviko. Kuanzia Mei 2017, kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 100 ya kutokea kwa Mama Yetu huko Fatima, Kardinali Andrea Soo-jung Yeom, wakati huo Askofu Mkuu wa Seoul, kwa barua ya maalumu ya  kichungaji alitaka kuongeza mazoezi kusali  Rozari baada ya misa kwa upatanisho, kwa nia ya kukabidhi amani kwenye Peninsura ya Korea na amani duniani kwa Bikira Maria.

 

10 January 2024, 14:16