Sanamu ya Yesu mnazareti aliyewekwa iliyowekwa kwenye kioo katika maandamano ya tarehe 9 Januari 2024. Sanamu ya Yesu mnazareti aliyewekwa iliyowekwa kwenye kioo katika maandamano ya tarehe 9 Januari 2024.  (AFP or licensors)

Siku Kuu ya Mnazareti Mweusi imeanza tena huko Manila ikivuta maelfu ya watu

Watu milioni mbili walishiriki katika hafla ya kiutamaduni katika mji mkuu Manila,moja ya siku muhimu zaidi na iliyohudhuriwa na waamini wa Kanisa katoliki Nchini Ufilipino.Sanamu hiyo imefungwa kwenye sanduku la kioo ili kuzuia mashambulizi ya umati.Imekuwa sherehe ya kwanza bila vizuizi fulani baada ya janga la uviko-19.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Waamini hadi milioni mbili walishiriki tarehe 9 Januari 2024 huko jijini Manila katika maandamano ya kiutamaduni ya ‘Mnazareti Mweusi,’ moja ya hafla muhimu sana  kwa Kanisa Katolini nchini Ufilipino, nchi pekee yenye Wakatoliki wengi barani Asia na kuhusishwa na sanamu ya Kristo wa ambao ya miaka mia moja. Kila mwaka huhamisha sanamu hiyo takatifu kutoka mahali pa asili, la  kanisa la Mtakatifu Nicola wa Tolentino, kwenye  Parokia ya Quiapo,  katika mji mkuu, kwa novena kuanzia tarehe 31 Desemba  hadi  siku rasimi ya tarehe 9 Januari. Kwa njia hiyo mwaka huu imeona ushiriki mkubwa wa watu wanaoomba  neema ya kibinafsi au muujiza. Katika miaka mitatu iliyopita tamasha hilo lilikatizwa au limefanyika kwa kiwango kidogo kutokana na janga la Uviko-19; kwa sababu hiyo, toleo la sasa limewakilisha wakati wa kusherehekea zaidi na kuzindua tena kifungo cha waamini na Yesu anayebeba msalaba.

Sanamu ya Mnazareti ni ya kihistoria

Sanamu ya kihistoria ya Mnazareti Mweusi, ukubwa wa maisha na iliyofunikwa kwa kioo ili kuwazuia waamini wasikwee kama ilivyokuwa hapo awali, ambapo iliandamana katikati ya mji wa Manila baada ya misa iliyoadhimishwa alfajiri sana. Tukio lenye maana dhabiti ya kiroho na kiapo na ambalo hufichua uhusiano wa karibu kati ya imani, jamii na mila na utamaduni. Mwaka huu mamlaka imetuma zaidi ya wafanyakazi elfu 15 wa usalama na wafanyakazi wa matibabu kando kando ya njia, tayari kuingilia kati katika kesi ya dharura. Waamini milioni mbili walishiriki katika safari kwa kwenda (polepole) kuelekea Kanisa la Quiapo, kulingana na makadirio ya kwanza yasiyo rasmi kwamba  miongoni mwa watu ni jambo la kawaida kutoa heshima kwa sanamu, ambayo ina nguvu za miujiza ya uponyaji, wa magonjwa yasiyoweza kupona au kupata neema. Hata hivyo kwamba ingetosha kuigusa  tu  kwa hivyo chaguo la kuifungia kwenye kioo ni, kuepusha ajali za watu kutaka kukwea juu ya sanamu hiyo.  Padre Hans Magdurulang, msemaji wa toleo la 2024 la Mnazareti, aliripoti kwa Shirika la Habari za Kidini la Asia (AN) kwamba tangu asubuhi hiyo  tayari kulikuwa watu milioni moja na lakini tatu.

Ushuhuda wa waamini huko Manila

Dori Hael Marquez, mama wa watoto wawili, alisemakuwa amekuwa mshiriki wa Mnazareti Mweusi kwa miongo kadhaa. “Nimepokea miujiza kutoka Kwake daima.” Hayo yaliungwa mkono na Mavic Duque, mama wa watoto sita ambao ni watu wazima, ambaye anaamini hivi: “Asante sana, Bwana wetu mpendwa Yesu wa Nazareti, kwa baraka zako juu yetu na kwa wokovu wetu katika maisha ya kila siku. Utatuongoza daima. Viva Nuestra Yesu Mnazareti”. Ushuhuda mwingine wa Luzviminda Parada, mfanyakazi wa sekta ya kibinafsi, aliongeza: “Katikati ya bahari yenye uchangamfu ya waabuduo, Sikukuu ya Mnazareti Mweusi inafunuliwa kama sherehe yenye nguvu ya imani, umoja na roho ya kudumu ambayo inatufunga katika safari hii takatifu.”

Asilimia 82 ya wakati wa Ufilippini ni wakatoliki

Nchini Ufilipino, zaidi ya 82% ya wakazi takriban milioni 110 ni Wakatoliki. Miongoni mwa sherehe za kidini, maandamano ya “Mnazareti Mweusi” ni kati ya sherehe maarufu sana. Sanamu hiyo inawakilisha Yesu aliyeinama chini ya uzito wa Msalaba. Ililetwa Manila na Padre  Augustino, Mhispania mnamo mwaka 1607 ndani ya meli kutoka Mexico. Kulingana na mapokeo, mashua hiyo ilishika moto wakati wa safari, lakini sura ya Kristo iliepuka moto kimuujiza kwa kugeuka kuwa nyeusi. Hapo awali Padre Sabino Vengco, wa Ufilipino, alisema kuwa rangi nyeusi inahusishwa na matumizi ya kuni. Maandamano hayo yanaadhimisha harakati ya kwanza ya sanamu hiyo, ambayo ilifanyika mnamo tarehe 9 Januari 1767. Katika njia nzima (kilomita saba) ya Tafsiri, ambayo huchukua saa kadhaa, kundi la waamini hugusa au kumbusu sanamu kama ishara ya kujitolea, kuunda mikusanyiko mikubwa. Ndio maana katika miaka ya hivi karibuni hafla hiyo imeghairiwa au imepata vikwazo vizito katika suala la kuzuia na afya ya umma.

ufilipino
10 January 2024, 15:44