Tanzania:Kanisa la Bukoba limempata Askofu Jovitus Mwijage
Na Angella Rwezaula - Vatican.
Jimbo katoliki la Bukoba Tanzania, Jumamosi tarehe 27 Januari 2024 limefurahi kumpata Askofu Mpya Jovitus Francis Mwijage aliyewekwa na kusimikwa rasmi kuwa Askofu wa Jimbo hili katika, Ibada iliyoongozwa na Kardinali Protase Rugambwa, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu katoliki la Tabora, Tanzania huku akisaidiana na Askofu Msaidizi Methodius Kilaini, Msimamizi wa Kitume wa Jimbo hilo kabla ya tangazo la kustaafu ambalo lilitolewa mwishoni mwa maadhimisho ya Ibada ya Misa ya Askofu Mteule wa 5 mzaliwa wa Jimbo la Bukoba.
Ibada ya Misa Takatifu hiyo itanguliwa na Masifu ya jioni tarehe 26 Januari 2024 na ambayo yaliongozwa na Askofu Flavian M. Kassala Makamu rais wa TEC na Askofu wa Jimbo la Geita kwa kuudhuria na maaskofu, Mapadre, mashemasi na waamini Watu wa Mungu, katika Kanisa Kuu la Bukoka Tanzania. Katika Ibada ya Misa iliyofanyika katika Uwanja wa Mpira wa Kaitaba pia iliudhuriwa na Maaskofu wa Tanzania TEC, Maaskofu kutoka nje ya nchi kama vile wa Ngozi Burundi, Zambia, Mwakilishi wa Kanisa Kuu la Kigari, mapadre wa Jimbo 173, mapadre kutoka majimbo mbali mbali, ya Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, Zimbabwe.
Misa hiyo aidhailiudhuriwa na Mapadre wawakilishi kutoka Mabaraza ya Maaskofu kwenye kitengo cha Mashirika ya Kipapa ya Kimisionari(PMS), kama vile Hispania, Chekoslovakia, Balozi wa Vatican nchini Uganda, Viongozi wa Vyama vya kisiasa na Serikali wakiwakilishwa na Waziri Mashaka Doto Biteko, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Tanzania, Viongozi wa madhehebu mbali mbali, waamini wa Mungu na wenye mapenzi mema.
Kwa kuongoza na Injili iliyosomwa, Kardinali Protase Rugambwa ameanza tafakari yake akisema kuwa “ Maashamu Maaskofu, Maaskofu wakuu, waheshimiwa, viongozi wa serikali na wa taasisi mbali mbali, wapendwa, mapadre, watawa wa kike na kiume, wapendwa waseminari na waamini, walei nyote mlioko hapa na wenye mapenzi mema Kristo… Kwa namna ya pekee, ninapenda kuwasalimu, kuwapongeza na kuwashukuru, Mwashamu Askofu Desiderius Rwoma, Askofu Mstaafu wa Bukoba na Methodius Kilaini, Askofu Msimamizi wa kitume wa Jimbo hili ambaye masaa machache yajayo atamwachia uongozi Askofu mpya, anayewekwa wakfu, na kusimikwa rasmi katika adhimisho hili la leo. Aidha ninapenda kuwakumbuka, kuwaenzi na kuendelea kuwaombea Maaskofu waliotutanguliwa na sasa wanalala katika Kristo. Mungu awajalie pumziko jema, na taabu aliyowaekea watumishi wake waaminifu."
Kardinali Rugambwa aliendelea kusema kuwa: "Ndugu zangu tumekusanyika kwanza kumshukuru Mungu kulijalia jimbo la Bukoba mchungaji mpya. Nitapenda tuongozwe katika tafakuri hii na maneno ya kauli mbiu ya Baba Askofu Mteule, ambaye nimeona yanaendana vizuri kabisa na mawazo ya Mama Kanisa. Na mawazo yetu sote ambao tunaongozwa na tumekuwa tayari tuwe watu wa Sala, kwanza huyu Baba Askofu mteule na sisi wenyewe tukijiombea utume wetu na yote hayo tumeyafanya kwa unyenyekevu ambao Mama Bikira Maria, msimamizi wetu, Mama Maria mwenye huruma na zaidi ya hapo, yote hayo tuyafanye tukisukumwa na upendo wa kweli na upendo wa Mungu, upendo uliotukomboa sisi sote. Tutanapo yafanya hayo, hatuna budi na sina budu kusema, kwa wana Bukoba: “ Mwayukoa muno, kandi Omukama alinde...."
Kumpata Askofu mpya ni ishara ya upendo kwa Mungu, kwa watu wake. Na hakika Mungu anaendelea kutimizia ahadi yake aliyoitoa kwa kinywa ha Yeremiah: “Nami nitawapa ninyi wachungaji wanipendezao moyo wangu (Yer 3,15). Mungu amependa kutupatia huyu ndugu yetu tuliye naye hapa mbele yetu, tunaelekea kumwekea mikono kwa nguvu ya Roho Mtakatifu ili apate kuwa mchungaji wenu, kwa niaba ya Kristo, kuhani Mkuu na wa milele, hivyo ninawaalikeni wana Bukoba kumpokea kwa shukrani, tumheshimu, na kumstahi, kama wakiri na mjumbe wa Kristo miongoni mwetu. Kama mhudumu wa matakatifu ya Mungu aliyeteuliwa na Bwana mwenyewe kudumisha na kuendeleza kazi yake ya kufundisha, kwa kutakatifuza na kuwachunga kondoo wake. Kumpokea daima kwa maneno ya Yesu kwa mitume wake: “Awasikilizaye ninyi, ananisikiliza mimi, Naye wakataaye ninyi ananikaataa mimi, Naye anakataaye mimi amkataa Yeye aliyenituma (Lk 10,16).
Leo Mungu anawakabidhi nyinyi nyote kwa huyu mteule ili atembee nanyi na awaongoze katika safari yenu ya ufuasi wa Kristo. Akiwaonesha njia iliyofunuliwa na Mungu. Na kama tuliovyosika kutoka katika somo la kwanza, daima Mungu huwa ana mipango yake isiyojulikana kwetu: “Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni nilikutakasa, nikakuweka kuwa nabii wa mataifa (Yer 1,3).” Baada ya kusema yanayo yanawawahusu waamini, Kardinali Protase Rugambwa aliendelea huku akimgeukiia Mteule na kusema kwamba: Mteule atakumbuka na kuzingatia daima kuwa kundi alilokabidhiwa leo ni mali ya Kristo mchungaji. Hivyo anawalika waishi wito na atekeleze utume wake kwa kusikiliza daima Kristo. “Ninyi mmekuwa rafiki zangu mkitenda niwaamruyo. Si ninyi mlionichagua, bali ni mimi niliye wachagua ninyi, nami nikawaweka mwende mkazae matunda na matunda yenu yapate kukaa”(Yh 14,14-16).
Kumbe lazima awaongoze kondoo wa Bwana kwa kufuata nyao za Kristo aliye njia, ukweli na uzima. Ili kuweza kuzaa matunda na kama tulivyosikia katika Injili, ni lazima kuzishika amri na kuyafanya mapenzi ya mwenye kundi kama vile” “Baba alivyonipenda mimi, nami nilivyowapenda ninyi, kaeni katika pendo langu, mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu. Kama mimi nilivyozisha amrri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake.” Kumbuka pia kwa kushika amri tu haitoshi, kama hauna upendo kwa Kristo, ambayo ni sifa ya kwanza ya kuwa mtumishi wake. Upendo ndiyo ishara ya kipimo cha utendaji wetu. Yesu kabla ya kumkabidhi Petro uongozi wa Kanisa lake, alimuuliza mara tatu: “Petro wanipenda? basi chunga kondoo wangu.”
Kumbe ufanisi na mafanikio ya utumishi wako na wetu sote, utategemea zaidi ya upendo wako, kwa yule unayewakilisha. Na ukimpenda Bwana, utajaliwa pia namna ya kuwapenda wale uliokabidhiwa. Isitoshe, upendo kwa Bwana unadhihirishwa na njia ya upendo kwa kondoo. Yeye mwenyewe ameliweka wazi anaposema katika Injili ya Matayo: “Kadiri mlivyowatendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi. Kwa hiyo ni kwa upendo wa kibaba na kidugu, na upendo wote ambao Mungu anakukabidhi siku yake. Kama anavyosisitiza mara kwa mara Baba Francisko kuwa: “Maaskofu yabidi kuwa karibu na Mungu kwa njia ya sala.”
Kama ulivyopenda kuweka katika kaulimbiu yako, kuwa karibu na mapadre na kuwa karibu na watu wa Mungu. Bilashaka kwa upendo ndilo neno la tatu lililowekwa kwenye kaulimbiu. Usisahau kwamba umechaguliwa miongoini mwa watu kutumikia Mungu, kwa niaba yao. Wapende mapadre, sikiliza mahitaji yao, watie moyo, wasahihishe, hali ukiwachukulia kwa upole, kwa hisani na kwa uvumilivu, huku ukikumbuka wewe mwenyewe kuwa kielelezo cha utakatifu, upendo, upole na unyenyekevu wa Maisha. Kwa jinsi hivyo upendo na umoja wenu vistawishe kazi zenu za kitume. Upende pia watawa, wa kiume na kike. Ukiamini na kukuza mchango wao muhimu katika utume wa Kanisa hili mahalia la Bukoba. Wapende kwa dhati waamini walei ukiwaalika na kushiriki kikamilifu katika utume wa maisha ya Kanisa ili Jimbo la Bukoba lipate “sura halisi ya kisinodi, kutembea pamoja, sote pamoja.” Wapende na kuheshimu pia ndugu zetu wa makanisa mengine, waamini wa dini nyingine na hata wasioamini, kama sio katika jukwaa la imani, basi mtakutana katika lile la ustawi wa maendelo ya watu wa Bukoba na kwingineko.
Bilashaka ukiwapenda watu nao pia watakupenda, watakuheshimu na watakusikiliza, kwani Bwana ameahidi: “kondoo wangu wasikiao sauti yangu, nami ninawajua, nao wananifuata(Yh 10,27).” Na tusisahau hili tulilosikia kutoka kwenye sehemu ya Injili ya leo: “Amri yangu ndiyo hii mpendane kama nilivyowapenda Ninyi. Hakuna aliye na upendo kuliko huu wa mtu kutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake. Haya ninawaamuru ninyi mpate kupendana.” Na wakiri wa huduma ya Kristo aliye nabii, kuhani na mfalme, wewe utajitajirisha upendo wake wa kichungaji, kwa njia ya kufundisha, kutakatifuza watu wa Mungu na kuwaongoza. Katika kutekeleza jukumu lako la kufundisha na kuwatangazia watu njia ya Kristo kwa bidii na bila kuchoka na hayo ndiyo uliyoahidi jana ulipowekwa hiyo ahadi, kutangaza Neno la Bwana kwa uaminifu na ujasiri.
Yaone kuwa ni maagizo yanayoelekezwa kwako pia hayo aliyosema Mtume Paulo kwa Timoteo tuliyoyasikia leo hii. Basi usiuonee haya ushuhuda wa Bwana wetu, wala usinionee haya mimi mfungwa wake, bali uvumilie mabaya pamoja nami kwa ajili ya Injili, kwa kadiri ya nguvu ya Mungu; (2 Tm 1, 8). Katika sura ya Nne ya Barua hiyo hiyo Mtakatifu Paulo anazidi kumhasa Timoteo aliyekuwa amemweka kuwa Askofu wa Kanisa la Efeso, anasema: “ Hubiri neno, uwe tayari wakati ukufahao na wakati usiokufaa”, kaeni pia kemea na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho. Neno la Bwana linalikualika pia “Usiseme tazama Bwana mimi sijuhi kusema kwa kuwa bado ningali kijana, kama Bwana alliyomwambia Yeremiah, kama tulivyosikia leo, nawe pia anakwambia: “Usiogope kwa sababu ya hao, maana mimi nipo pamoja nawe nikuokoea (Yer 1,8).
Kwa msaada wa Roho Mtakatifu na kwa ajili ya jitihada zako, katika kutafakari na Neno la Mungu na kusisoma alama za nyakati, utaweza kutambua na kung’amua mapenzi ya Mungu na ujumbe wa kinabii unaotaka uwafikishie watu wako. Usikose pia kutoa mwanga na mwongozo wa machungu na karaha za wanadamu wa nyakati zetu, yaani magumu na matatizo ambayo watu wa nyakati zetu wanakabiliwa na kufadhishwa nayo. Hivyo uwashuri watu kulingana na mafundisho ya Kanisa, jinsi wanavyoweza kuyakabili na kutatua masuala ya kijamii yenye uzito wa kipekee, matatizo yahusuyo haki, amani, upatanisho na maridhiano, ustawi na maendeleo ya watu nk.
Hata hivyo zingatia kwamba daima ukweli lazima uendane na mapendo na maelewano. Katika jukumu lako la kutakatifuza, kumbuka kuwa umechaguliwa miongoni mwa watu na kuwekwa kwa ajili ya watu wote ili kutoa vipaji na sadaka kwa ajili yao na dhambi zao. Kumbe huduma katika kuombea na kuwatakatifuza watu hasa kwa njia ya Ekaristi Takatifu ambayo kwayo Kanisa uishi na kukua, hali likiwahubiria na kuwatakatifuza wale waliokabidhwa, nawe pia jitakatifuze ili upata kufikia uzima wa milele pamoja na kundi ulilokabidhiwa. Katika Muktadha huo mtume Paulo alimwonya Timoteo pia akisem: “ Uyatafakari hayo, ukae katika hayo ili kuendelea kwako kuwe dhahiri kwa wato wote.” Jitunze nafasi yako na mafundisho hayo, dumu katika mambo hayo, maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yake, na wale wakusikiao. Katika kutekeleza jukumu lama mchungaji na kiongozi, jitahidi kuwa kama yule atumikiaye akikumbuka daima, maelekezo ya Bwana: “Aliye mkubwa na awe kama aliye mdogo.” Na kwenye kuongoza kama yule atumikiaye (Lk 22, 26-27). Kuweka mbele yako macho yako kama mfano wa mchungaji mwema “aliyekuja siyo kutumikiwa bali kutumikia na kutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo.”
Wapendwa katika Kristo, ili kufanikisha utume wake mpendwa wetu, anahitaji sana ushirikiano wenu na sala zenu, na hilo ndilo alilotuomba sote. Kama vile Yeye anavyotuombea, anavyokuwa mwaminifu katika kutimiza mapenzi ya Mungu katika upendo na kutaka sisi vile vile tufanye kama yeye. Na yeyote atanguliwe na upendo wenu kwake na Kanisa la Bukoba na la ulimweni wote. Mpendwa Jovitus Mwijage, kwa furaha na imani kubwa katika Yeye aliye kuita umtumikie, tunakukabidhi kwa Mama Bikira Maria mwenye huruma, Mama yetu na msimamizi wetu, Mama wa Kanisa, Malkia wa Mitume ambaye licha ya changamoto alizokumbana nazo alibaki mwaminifu, kama wewe unavyotaka kuwa mwaminifu, kwa wito wake, kama wito wako. Yeye akutangulie daima na kukuongoza katika Maisha na utume wako wa kiaskofu. Roho Mtakatifu akujaze nguvu ili kuwa mahiri katika Uinjilishaji na uwe shuhuda, wakiri, mwaminifu wa Kristo, Amina.
Mara baada ya Misa na baraka, zilitolewa fursa za wawakilishi wa Kimataifa na ndani ya nchi kutoa neno ambapo miongoni mwao, Balozi wa Vatican, nchini Tanzania Askofu Mkuu Angelo Accattino alianza kumpongeza na zaidi kuzungumzia juu ya Askofu wa Kwanza mzawa wa Bukoba, Kardinali Laurean Rugambwa na wengine waliofuta na zaidi, alikumbusha juu ya tukio hilo kuwa maalum kwa sababu limerudisha nyuma historia ya Kardinali Rugambwa aliyetoa wakfu wa Kiaskofu huko Tabora na sasa Kardinali Protase Rugambwa kutoka jimbo hilo hilo la Tabora, ambaye alimwita(Rugambwa II...) kumweka wakfu Askofu Mteule, baada ya miaka 50 tangu uzoefu huo wa kusimikwa Rasmi kwa Askofu Nestory Timanywa mnamo 1974 huko Bukoba.
Balozi Accattino vile vile alishukuru ushirikiano mzuri uliopo kati ya Serikali na Kanisa, kwamba ni ishara ya uaminifu. Utume unahitaji nguvu. Kazi kubwa iliyopo ni kujenga madaraja kati ya Mungu na Watu. Matunda ya utume yanatokana na makuhani wanavyohudumia watu. Yesu alisisitiza umuhimu wa Umoja na ili wote kuwa pamoja kama yeye alivyokuwa pamoja Mungu wake. Balozi Accattino alisisitiza kuhamasisha mapadre umoja na upendo, lakini wakati huo huo akasema: “itakuwa haina maana iwapo hakuna ushirikiano kati ya maaskofu.” Katika hili alisema katika huduma Bwana alisema kuwa: “ukifanya yote hayo jifanye kuwa hustahili bali umefanya kama mtumishi hasiye na faida…”Kwa kuhitimisha alisema: “Mungu ni mwema kila wakati," na watu walijibu, "Kila wakati Mungu ni mwema."
Mara baada ya Balozi, wa Ctican Nchini Tanzania lilifuatia neno kutoka kwa Makamu rais wa Baraza la Maaskofu katoliki Tanzania (TEC) kwa niaba ya Baraza hilo, Askofu Fravian M. Kasala alianza“kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema hiyo, kwani kwa kupitia Baba Mtakatifu akamteua Jovitus Mwijaga ambaye amewekwa wakfu kama Askofu. Alimshukuru kwa utendaji wake katika Baraza lao la Maaskofu wa Tanzania mahali ambapo alikuwa akiongoza Kitengo cha Mashirika ya Kipapa ya Kimisionari(PMS) kwa miaka 10. Ni mategemeo yake kuwa uzoefu aliouchota wa muda mrefu na utendaji wake katika vyombo vya kimataifa, vitamsaidia kuliongoza Kanisa lake mahalia ambapo amerudi kama Askofu. Askofu Kasala aliwaomba waamini pia washirikiane naye katika utume huo anaouanza. Na viongozi wengine wa Serikali, kuanza na mgeni rasimi walipta kuzungumza, na baadaye zawadi mbali mbali zilitolewa kwa Askofu Mteule.