Haiti:Watawa saba wametekwa nyara
Vatican News
Ndugu Sita wa Shirika la Moyo Mtakatifu walitekwa nyara asubuhi ya tarehe 23 Februari 2024, walipokuwa wakielekea kwenye Utume wao wa Shule ya Yohane XXIII nchini Haiti. “Tunawaombea ukombozi wao na kukomeshwa kwa janga hili la ukosefu wa usalama, wanaandika watawa wa kike na kiume wa eneo hilo katika taarifa, ambao wanasisitiza kwamba shule ndiyo pekee ambayo bado inafanya kazi katika eneo hatarishi katikati mwa shule ya mji mkuu wa Port-au-Prince. Padre ambaye alikuwa ametoka kuadhimisha Misa katika Kikanisa cha Mama Yetu wa Fatima, katika wilaya ya Bicentenaire ya mji mkuu, pia alitekwa nyara.
Askofu Dumas alifanyiwa upasuaji
Wakati huo huo, Askofu Pierre-André Dumas, askofu wa Jimbo la Anse-à-Veau na Miragoâne, alifanyiwa upasuaji mara mbili mara baada ya kujeruhiwa Dominika iliyopita na mlipuko katika nyumba aliyokuwa amefikia wakati wa ziara ya Port-Au-Prince. Kwa sasa hali yake inaendelea vizuri na ameanza kula, kwa mujibu wa vyanzo vya ndani vinaripoti juu ya kuhamishiwa katika hospitali ya Miami.
Ukosefu wa usalama na ukosefu wa utulivu unaendelea
Hali katika nchi hiyo ya Caribean bado ni mbaya sana kuhusiana na ukosefu wa usalama unaosababishwa na ukosefu mkubwa wa utulivu wa kisiasa na polisi ambao hawawezi kukabiliana na magenge yenye silaha ambayo yanapamba moto hasa katika mji mkuu. Mapadre na wa Kitawaa mara nyingi ndio walengwa wa utekaji nyara unaofanywa na vikundi vya wahalifu, wakishawishiwa na imani kwamba Kanisa la Haiti ni tajiri na linaweza kulipa fidia. Kipindi kigumu cha mwisho kilianzia takriban mwezi mmoja uliopita wakati watawa sita walipotekwa nyara kutoka katika Bus. Katika hafla hiyo, Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana alisali kwa ajili yao kuhusu: “maelewano ya kijamii nchini Haiti na kutoka mwaliko kwa kila mtu “kukomesha ghasia zinazosababisha mateso mengi kwa watu hao wapendwa.”