Tafuta

2024.02.04 Kardinali Czerny yuko  Sudan Kusini kuanzia 2 hadi 9 Februari 2024. 2024.02.04 Kardinali Czerny yuko Sudan Kusini kuanzia 2 hadi 9 Februari 2024. 

Kardinali Czerny:“Tuko karibu na watu wa Sudan Kusini”

Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kukuza Maendeleo Fungamani ya Binadamu,aliyetumwa na Baba Mtakatifu Francisko katika maadhimisho ya mwaka wa I wa ziara yake nchini Sudan Kusini mwaka 2023 aliyoanza 2 hadi 9 Februari 2024,anatarajia kwenda Renk 8 Februari na atabariki Mtumbwi inaotumiwa na Caritas kusafirisha wakimbizi kwenye Mto Nile hadi Malakal.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la kuhamasisha Maendeleo Fungamani ya Binadamu, Kardinali Czerny alitumwa na Baba Mtakatifu Francisko katika maadhimisho ya mwaka wa kwanza wa ziara ya Papa nchini Sudan Kusini aliyohitimisha huko kuanzia tarehe 3 -5 Februari 2023. Safari hiyo ya Kardinali  ilianza 2 hadi 9 Februari ambapo anaendelea kukutana na waamini na viongozi wa Kanisa na serikali ambapo pia amekutana na Rais wa Nchi hiyo.

Papa akikutana na Kanisa la Sudan Kusini 2023
Papa akikutana na Kanisa la Sudan Kusini 2023

“Kuhakikisha uchaguzi huru na wa kuaminika.” Ndiyo ahadi iliyosisitizwa tena na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, akikutana na Kardinali Michael Czerny ambapo pia  alisisitiza tena ukaribu wa Baba Mtakatifu  na Vatican  kwa watu wa Sudan Kusini na kuhimiza upya wito wake kwa viongozi wa Sudan Kusini “kukumbatia amani na utulivu wakati nchi yao inapoelekea kwenye kipindi cha mpito cha kidemokrasia. Papa Francisko anatarajia kuona uchaguzi wa kuaminika, huru na wa haki nchini Sudan Kusini.

Papa Francisko wakati yuko Sudan Kusini 3-5 Februari 2023
Papa Francisko wakati yuko Sudan Kusini 3-5 Februari 2023

Kwa upande wa Rais Kiir alijibu kwa kukaribisha nia ya Vatican kuunga mkono uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi Desemba mwaka huu 2024. Kura hiyo ni sehemu ya makubaliano ya amani ya mwaka 2018, ambayo yalimaliza miaka mitano ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoua mamia kwa maelfu ya watu. Lakini masharti ya makubaliano hayo, ikiwa ni pamoja na kuunda jeshi la umoja wa kitaifa, bado hayajatekelezwa. Mnamo Agosti 2022, serikali ya mpito ya Sudan Kusini iliongeza mamlaka yake kwa miaka miwili hadi Februari 2025, na uchaguzi uliopangwa kufanyika Desemba 2024.

Maisha ya wasudan wanahitaji msaada wa upatanisho
Maisha ya wasudan wanahitaji msaada wa upatanisho

Hii ni kuwezesha wadau kukabiliana na changamoto katika kutekeleza masharti yanayosubiri Mkataba wa Uhuishaji wa 2018 juu ya Azimio la Migogoro katika Jamhuri ya Sudan Kusini (R-ARCSS). Makubaliano hayo yalilenga kuhitimisha serikali ya mpito huku uchaguzi ukipangwa kufanyika mnamo Desemba 2022. Hata hivyo, kutokana na kuchelewa kwa utekelezaji, uchaguzi huo uliahirishwa hadi 2023 na kisha 2024. Wakati wa ziara yake kuanzia tarehe 2 hadi 9 Februari 2024 Kardinali Czerny anatarajia kusafiri hadi  huko Renk tarehe 8 Februari 2024 ambapo atabariki Mtumbwi inaotumiwa na Caritas ya eneo hilo kusafirisha wakimbizi kwenye Mto Nile hadi Malakal.

Mtumbwi wa Caritas unaosafirisha wakimbizi hadi Malakal
Mtumbwi wa Caritas unaosafirisha wakimbizi hadi Malakal

Ikumbukweli katika fursa ya Ziara ya Kitume ambayo ilimalizika nchini Congo (DRC) tarehe 31 Januari-3 Feb) 2023 na baadaye  Kusini mwa Sudan, Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Umoja wa Kikristo lilibainisha kwamba “Kuwasili kwa Papa Francisko nchini Sudan Kusini kuanzia tarehe 3 -5 Februari 2023  kunaashiria mwanzo wa hija ya kiekumene ya amani ambayo haijawahi kutokea.” Katika ziara yake ya kitume iliyomuona jijini  Juba, ambao ni mji mkuu wa nchi hiyo, Baba Mtakatifu alisindikizana na Askofu mkuu Justin Welby wa Canterbury, na Mchungaji Iain Greenshields Msimamizi wa mkutano mkuu wa Kanisa la Scotland. Mbali na kuwa na umuhimu ulio wazi kwa wananchi wa Sudan na kwa hali ya kisiasa na kijamii ya nchi hiyo, Hija hiyo ilikuwa na  thamani kubwa ya kiekumene. Na ilikuwa ni kwa mara ya kwanza kwa Askofu wa Roma kufanya ziara ya pamoja na viongozi wa Makanisa ya Kianglikani na Kipresbyterian iliyopyaishwa. Takriban theluthi mbili ya wakazi wa Sudan Kusini ni Wakristo na kiwango cha ushirikiano na umoja kati ya tamaduni mbalimbali za Kikristo hadi sasa zimekuwa nzuri sana.

Kardinali Czerny Nchini Sudan Kusini
06 February 2024, 14:55