Tafuta

Kardinali Marengo,Msimamizi wa Kitume wa Mongolia na waamini  wake. Kardinali Marengo,Msimamizi wa Kitume wa Mongolia na waamini wake. 

Mongolia,Kard.Marengo:Kwaresima ni kipindi cha sala na upatanisho

Tumezingatia mada ya sala katika Mwaka huu wa Sala kwa utashi wa Papa katika maandalizi ya Jubilei.Jumuiya ya Wamongolia inahisi kuwa na uhusiano mkubwa na Vatican.Tulitafsiri ujumbe wa Papa wa Kwaresima katika lugha ya Kimongolia na kuusambaza siku ya Jumatano ya Majivu.Alisema hayo Kardinali Marengo,Msimamizi wa Kitume huko Mongolia.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kadinali Giorgio Marengo, Msimamizi wa Kitume wa Ulaanbaatar, akizungumza na Shirika la Habari za Kimisionari (FIDES) kuhusiana na kipindi cha Kwaresma alisema kuwa “Jumuiya yetu ndogo ya Kikatoliki huko Mongolia inapitia kipindi hiki cha  Kwaresima cha nguvu. Jumuiya tisa za parokia zimezindua programu zao za kichungaji na kiroho. Tumezingatia mada ya sala, katika Mwaka huu wa Sala, iliyooneshwa na Papa kwa ajili ya maandalizi ya  Jubilei. Wakati huo huo -wa Kwaresima daima una kipengele cha kuvutia kwa sababu huanza na Mwaka Mpya wa Mwezi (Lunar.) Mwaka huu kalenda ya Kimongolia iliendana na tarehe iliyopitishwa nchini Korea na China. Tulikuwa na mkesha wa Mwaka Mpya mwishoni mwa Juma na kisha; katika Juma lililofuata mchakato wa safari ya Kwaresima ilianza na Jumatano ya Majivu.”

NCHINI MONGOLIA
NCHINI MONGOLIA

Kwa upande mmoja, Mkesha wa Mwaka Mpya ni wakati wa wingi na sherehe, si wa sadaka; kwa upande mwingine unaleta maadili ambayo yanapatana sana na Injili, kama vile kufanywa upya, kwa mfano. Kila kitu lazima kiwe kipya, kwa nia ya upyaisho halisi, wa kina, sio tu wa nje nje,” alisisitiza Kardinali Marengo. Kwa kufafanua zaidi Msimamizi wa Kitume alisema “Lazima tupatane-ili kila kitu ambacho kimeshuhudiwa katika mwaka uliopita, kutokubaliana au mvutano fulani, kuachwa kando na tuanze tena na mahusiano ya amani. Kipengele cha pili: ni wakati ambapo kila mtu tunasherehekea mwaka mmoja zaidi, kwa sababu baridi iko nyuma yetu na wazee wanaheshimiwa kama wabebaji wa hekima ya pamoja. Kwa maana hii pia kuna maelewano kwa sisi Wakristo, tukizingatia sura ya baba kama mama wa kiroho ambao tunaweza kuwageukia zaidi mara kwa mara wakati wa Kwaresima.”

JUA LIKICHOMOZA NCHINI MONGOLIA
JUA LIKICHOMOZA NCHINI MONGOLIA

Jumuiya ya Wamongolia inahisi kuwa na uhusiano mkubwa na Vatican: “Tulitafsiri ujumbe wa Papa Francisko wa Kwaresima katika lugha ya Kimongolia na kuusambaza siku ya Jumatano ya Majivu. Pia ningependa kuwakumbusha kwamba hivi karibuni, lugha ya Kimongolia iliingia rasmi kama lugha ya 52 ambayo kwayo Vatican News inasambazwa. Sasa tuna jukwaa hili ambalo kwa sasa tunaweza kutafsiri katekesi ya Jumatano ya Papa na Sala ya Malaika wa Bwana kila Dominika yak ila Juma. Ni urithi wa mafundisho ya Papa ambao watu wanaweza kushauriana: tujaribu kuthamini kile ambacho Papa Francisko anakumbusha sisi katika kipindi huki cha Kwaresima. Kardinali Marengo aliendelea: “Ningependa kusisitiza tena mjadala huu wa mahusiano mapya, yaliyopatanishwa kwa sababu tafakari ya amani ambayo kwa bahati mbaya inaonekana kuwa inajadiliwa katika sehemu nyingi za dunia inategemea hii. Wito wa Mwaka Mpya wa Lunar husaidia tuchukue hatua hii: ili amani ifike, ni lazima kila mmoja wetu aanzie katika mahusiano yake, kwa kuwa wafanyakazi na wapandaji wa amani. Kwa hiyo ni mwaliko wa kujitolea kwa amani kuanzia uongofu wetu binafsi.”

KUBARIKI KWA SANAMU YA MAMA WA MBINGUNI ILIYOPATIKANA HUKO MONGOLIA
KUBARIKI KWA SANAMU YA MAMA WA MBINGUNI ILIYOPATIKANA HUKO MONGOLIA

Tarehe 5 Machi 2024  Kanisa mahalia litakuwa na  siku ya Mafungo ya kiroho ya  Kwaresima kwa mapadre, wamisionari waliowekwa wakfu wanaume na wanawake waliopo Mongolia, pamoja na uwepo wa Padre Mauro Giuseppe Lepori, Abate Mkuu wa Shirika la Cistercian. Hatimaye, katika ngazi ya upendo, Tume ya Haki, Amani na Uadilifu wa Uumbaji inajaribu kuchukua hatua kuwasaidia wakulima ambao, katika maeneo ya vijijini, wamezuiliwa na maporomoko ya theluji hasa. Na kwa njia hiyo “Baada ya siku chache mkulima anaweza kupoteza karibu mifugo yake yote kwa sababu wanyama wamezama kwenye theluji. Tunajaribu kuelewa kile tunachoweza kuwafanyia katika hali halisi: hii inaweza kuwa moja ya ahadi ambazo tungependa kufanya, kama  sifa zetu za Kwaresima za udugu,” alihitimisha Kardinali Marengo.

KARDINALI MARENGO AKIBARIKI SANAMU YA MARIA MAMA WA MBINGU
KARDINALI MARENGO AKIBARIKI SANAMU YA MARIA MAMA WA MBINGU
24 February 2024, 10:23