Zimbabwe:Maaskofu wanasema umaskini unaongezeka huku demokrasia ikifa pole pole
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Mkutano mwingine wa Maaskofu barani Afrika umeibua kilio cha hofu juu ya sera za kiuchumi zilizopitishwa na serikali ambazo zinazidisha hali ya umaskini na ambapo watu wengi wanaishi. Hawa ni Maaskofu wa Zimbabwe kama ilivyokuwa kwa wale wa Nigeria ambao walisema kuwa: “uamuzi wa serikali kuongeza ushuru huku raia wa kawaida wakihangaika kumudu mlo mmoja kwa siku umezorotesha hali za familia. Kwa watu wengi wazee na maskini hasa, imekuwa ghali sana kuishi. Bidhaa za kimsingi zinazidi kuwa ghali.” Walisema Maaskofu wa Zimbabwe katika taarifa yao. Uchaguzi wa mwezi Agosti 2023 uliokumbwa na mzozo umezuia mfumo wa kisiasa kiasi kwamba kulingana na maaskofu “watu wengi wanahofia kwamba tunaelekea kwenye serikali ya chama kimoja, huku demokrasia ikifa polepole.”
Kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Kimisionari la Kipapa (FIDES) linabainisha kuwa maaskofu wanasema kwamba "kutokana na siasa mbovu, mfumo mbaya wa uchumi na athari zake mbaya, watu wengi hukata tamaa." Aidha katika ujumbe huo Maaskofu kwa njia hiyo wanatoa mwaliko kwa watu wasiangukie katika jaribu la kukata tamaa bali zaidi ya yote kuomba. “Maombi sio njia ya kukwepa. Ni njia ya kutafuta suluhisho kwa changamoto zinazotukabili katika ulimwengu wetu na katika nchi yetu.”
Suluhisho zilizoanzishwa hata kabla ya akili juu ya hekima iliyovuviwa na Roho wa Mungu. Kwa hiyo ujumbe unatoa mwaliko wa kutumia fursa ya kipindi cha Kwaresima ili kuongeza maombi na uhusiano na Mungu “katika nchi na dunia iliyokata tamaa, kama Wakristo, tuweze kuwa vinara vya matumaini.” Licha ya kuimarika kwa uchumi wa nchi hiyo iliyorekodiwa mwaka 2021 na 2022, viwango vya umaskini, mazingira magumu na ukosefu wa usalama wa chakula vinaendelea kuwa juu.
Kuongezeka kwa msukosuko wa kimataifa na kukatika kwa ugavi kumechangia kupanda kwa bei ya nishati na chakula, pamoja na mfumuko mkubwa wa bei. Usumbufu wa msururu wa ugavi wakati wa janga la UVIKO-19, pamoja na vita vya Ukraine, vimeongeza mfumuko wa bei. Kutokana na athari za vita vya Ukraine, mwaka wa 2021, bei ya nishati iliongezeka kwa 80%, wakati bei za vyakula ziliongezeka kwa zaidi ya 30%. Kadhalika, mnamo 2022, bei za nishati ziliongezeka kwa 60%, wakati bei za vyakula ziliongezeka kwa 18% nyingine. Zimbabwe inasalia katika ugumu wa madeni na, ingawa ukopaji ni mdogo, deni la umma limeendelea kuongezeka, kutokana na malimbikizo ya nje na deni la urithi.