Italia,Machi 24 Siku ya Wamisionari Mashahidi:Wenye moyo unaowaka!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Ni ushuhuda unaoakisi na unaoangazia njia ya kiroho, ambao huimarisha, huo ndio ushuhuda wa mashahidi wanaoadhimishwa kila mwaka, ifikapo tarehe 24 Machi kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya kuwakumbuka Wamisionari mashahidi wote, iliyoanzishwa kunako mwaka 1993 na Missio Giovani, yaani kitengo cha vijana cha mwelekeo wa Italia ya Mashirika ya Kipapa ya Kimisionari(PMS). Katika fursa hiyo mwaka toleo la 32 la mwaka 2024, la siku hii, Missio Giovani wamesambaza nyenzo na maandishi ya kuhimiza maadhimisho ya mikesha, sherehe za kiliturujia na mipango inayohusiana na Siku hiyo, ambayo mwaka huu inakwenda sambamba na Dominika ya Matawi, ikiwa ni mwanzo wa Mateso, kifo na Ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo.
Kwa mujibu wa Giovanni Rocca, Katibu wa Missio Giovani, alikumbusha katika maandishi ya utangulizi miezi michache iliyopita kuwa: Siku ya Wafiadini wamisionari ina asili yake katika ukumbusho wa Mtakatifu Oscar Romero, aliyeuawa tarehe 24 Machi 1980. Kumbukumbu yake inaendelea, mwaka baada ya mwaka kumwilisha kielelezo cha ukaribu kwa uchache na wa kujitolea usiokoma kwa kazi ya Injili. Kujitolea kwake pamoja na watu wa Nchi ya Salvador, kupambana dhidi ya serikali ya wasomi isiyojali hali ya wanyonge na wafanyakazi, inaendelea kuzungumza na vijana na zaidi, akikumbuka hitaji la maisha ya Kikristo kuzingatia sala kama vile utunzaji wa dada na kaka. Miongoni mwa nyenzo mbalimbali za uhuishaji za kimisionari zilizosambazwa na Missio Italia, pamoja na misaada ya maombi, pia kuna video nane za kumbukumbu za mashahidi waliouawa (kuanzia na Wamisionari wa Comboni Ezechiele Ramin hadi kwa mlei aliyewekwa wakfu Luciano Lanzoni, aidha kwa mlei Annalena Tonelli hadi mmisionari Loredana Vigini,) pamoja na michoro ya mikono ya mshikamano.
Mada inayoongoza Siku hii ni “Moyo unaowaka” na inarejea wimbo wa wanafunzi wa Emau. Kwa mujibu wa Angelo Fracchia, msomi wa Biblia na mwalimu wa kidini, aliandika juu yake katika tafakari ya kawaida ya mada iliyoambatanishwa na hati na nyenzo, akipata msukumo kutoka kwa mfano wa Mtakatifu Stepheno Shahidi wa kwanza wa mashahidi wa Kikristo. Kwa mujibu wake alisema kuwa: “Stefano hakuogopa kuongea, kueleza, hata kwa ukali wa wazi ikiwa ni lazima. Lakini, wakati huo huo, yeye hakufanyi jeuri dhidi ya wale waliompiga mawe, hakutukana, na hana hatia. Alikaza macho yake kwa Yesu, akitambua ndani yake kiongozi ambaye tayari alikuwa amepitia yale anayopitia. Naye, akiimarishwa na ukaribu wa Baba, daima alibaki katika upendo huo, bila kulipiza kisasi, bila kulalamika juu ya udhalimu, kwa macho ya huruma na ya wazi."