Tafuta

2024.03.28 Maadhimisho ya Siku za Juma Takatifu nchini Mongolia 2024.03.28 Maadhimisho ya Siku za Juma Takatifu nchini Mongolia 

Kusherehekea Pasaka huko Mongolia ni furaha ya watu wanyenyekevu!

Kardinali Giorgio Marengo,msimamizi wa kitume wa Ulaanbaatar nchini Mongolia alisimulia taratibu na desturi za jumuiya ndogo ya Kikatoliki iliyokusanyika katika siku hizi Tatu za Juma Kuu:machozi machache ya hisia na tabia nyingi,hata bila maonesho makubwa ya nje."

Na Giorgio Marengo

Juma takatifu Takatifu lina uzoefu nchini Mongolia kama wakati muhimu, maalum na wa kipekee. Kwa angalau miaka miwili wakatekumeni ambao ni wazima wamejitayarisha kwa wakati huu, ambacho ni kifungu cha msingi cha maisha yao. Kuwasindikiza katika safari hii hutusaidia sisi wamisionari kuhuisha maajabu na msimamo mkali wa fumbo hili. Kwa maana hiyo, kuwa hapa pamoja na kaka na dada hawa wanaotaka kukaribisha kifo na ufufuko wa Kristo kwa uhuru maishani mwao hututia moyo tuifanye sherehe kuwa yetu, kuiishi kwa bidii na ufahamu upya.

Hizi ni nyumba za Mongolia
Hizi ni nyumba za Mongolia

Siku ya Matawi hushuhudia jumuiya zetu zikiperusha matawi membamba ya misonobari (mitende na mizeituni iko mbali sana), ambayo ndiyo kwanza inaanza kuchupua kutokana na majira ya baridi kali. Maandamano ya kawaida - kila mara hufanyika  ndani ya nafasi zinazotambuliwa na mamlaka tu - mara nyingi waamini ukumbana na upepo wa baridi na vumbi. Kipindi cha baridi ni msimu mgumu zaidi hapa, na mabadiliko ya ghafla ya joto, mifugo dhaifu na watu wenye matatizo ya kimwili. Fumbo la kuzaliwa upya kwetu hutokea katika wakati muhimu zaidi wa mzunguko wa asili, karibu kana kwamba Bwana Wetu alikuwa amechagua msimu huu kufikia kiwango cha chini kabisa cha ubinadamu wetu maskini.

Sherehe ya Misa ya Krisma tuliyoifanya siku ya  Jumanne kwetu inawakilisha tukio muhimu kwa mapadre wanaotoka hata maeneo ya mbali zaidi. Walipyaisha ahadi zao za kikuhani katika Kanisa kuu lenye waamini wachache na watawa wengine. Kisha tulikaa kwa kutafakari kwa ufupi fumbo la ukuhani uliowekwa wakfu na kula chakula cha mchana kwa furaha. Kurudi kwa parokia lazima kufanyike kwa muda mfupi, ili kuepuka hatari za barabara za barafu. Kila Parokia ilipata uzoefu wa Utatu Mtakatifu kwa kutunza vizuri liturujia na kumkaribisha askofu, ambaye anajaribu kujionesha angalau katika jumuiya za mji mkuu. Usiku mtakatifu utafika na  Moto hutawashwa ndani ya jengo la  jadi, kama ishara ya familia.

Maadhimisho ya Pasaka nchini Mongolia
Maadhimisho ya Pasaka nchini Mongolia

Kwa kuzunguka na msongamano wa magari na taa zinazowaka za jiji, wengi wao wakiwa hawajui kinachoendelea. Kanisa kuu la umbo la ger (yaani hema la Kimongolia) limefunikwa na giza, ambalo hupungua giza hilo wakati maandamano yenye mishumaa na mishumaa ya waamini wanapoingia. Nyimbo  zinaimbwa kwa lugha ya Kimongolia; pamoja na picha zake za kishairi, zikikumbusha nyimbo za kiutamaduni …. Kutoka hapo muda si mrefu wakatekumeni watakaribia kisima cha ubatizo na kuvaa mavazi meupe ya maisha mapya; mtu anafika na vazi deel ambalo ni (vazi la kiutamaduni) lililotengenezwa hasa kwa hafla hiyo. Machozi machache ya hisia, utulivu mwingi na furaha nyingi, hata bila maonesho makubwa ya nje yanayjitokeza. Uzoefu kwa njia hii, siku takatifu za Pasaka ni baraka ya kweli hata kwa wale ambao tayari wametembea kwa muda mrefu katika imani. Kila kitu huchangia kurejesha upya wa imani.

Jumatatu ya Pasaka tunakutana na wamisionari huko Khandgait, msituni nje kidogo ya Ulaanbaatar, ambapo Uwakilishi wa kitume una nyumba ya kiroho. Tunasherehekea katika Kanisa dogo la mbao, lililopashwa moto siku moja kabla kwa hafla hiyo. Miaka fulani theluji ilianguka sana, nyakati nyingine jua la masika huangaza. Kila mmoja wetu anahisi kubadilika sana kutokana na uzoefu wa siku zilizopita na tunamsifu Aliyefufuka kwa ajili ya washiriki wapya wa jumuiya ambao wamezaliwa upya kwa maisha mapya katika maji ya ubatizo.

Maadhimisho ya Pasaka nchini Mongolia
Maadhimisho ya Pasaka nchini Mongolia

Katika masikio na moyoni swali la Yesu baada ya kuosha miguu yake: “Je, unaelewa kile nilichokufanyia?” (taz Yh 13:12). Hatutaelewa kikamilifu, lakini siku za Pasaka hutusaidia kwa usahihi katika njia hii ya kurudi tena na tena kwa mwelekeo wa chanzo cha imani yetu. Na kuwasha tena moto ule uliowaka katika vifua vya wanafunzi wa Emau, sasa wakiwa tayari kusonga hatua zao kwa furaha kuelekea ulimwengu wakingoja tangazo lililobadilisha historia.

Kardinali Marengo
29 March 2024, 17:27