Tanzania:Kanisa ni jumuiya na kila jumuiya ni familia
Na Francesca Merlo – Sukamahela, Tanzania.
Kanisa la Tanzania ni kijana na la lenye rangi. Sio tu kwamba wanaimba, bali wanaelewana na kila mmoja anajua maneno. Sukamahela (ni kijiji cha Makutupora, Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni,Singida)ni mfano kamili wa hili. Lina usanifu fulani kwake; ukiombwa kuchora Kanisa, lisingefanana na lile la Sukamahela, lililobuniwa na kujengwa kwa msaada wa watu kutoka kijijini na Padre Petro.
Huyo ni Padre wa jimbo lakini mzaliwa wa Slovakia ambaye amejitolea maisha yake kwa watu ndani na karibu na Sukamahela, na huku watu wanaliokusanyika kwa ajili ya misa ya Dominika wakitutazama kwa udadisi ni wazi kwamba Padre Petro si mgeni kwao. Sukamahela, Misa haianzi kwa wakati. Hata wanapokuwa na shughuli nyingi, watu wa Tanzania wanapumzika. Hata wageni wawili wenye kamera walipofika na kushiriki katika Misa yao ya Dominika. Kile ambacho mwanzoni kilionekana kuwa kusanyiko dogo kabisa, kumbe kuna kungoja kwa subira nje ya Kanisa, ghafla likawa na zaidi ya watu mia moja.
Viti vilivyokuwa nyuma ya Kanisa kwa haraka vilijaa wanawake na watoto wao wachanga na watoto walio na umri wa kutosha walichukua viti vyao vya mbele ya mkusanyiko. Wote ni marafiki, au wanakuwa marafiki haraka sana. Upande wa kushoto kwaya ilianza kuimba na mapema maelezo yakasikika kutoka kwenye kuta za mduara wa jengo. Kulikuwa na wanawake wengi kuliko wanaume, wote wamekaa upande wa kushoto. Mstari wa kwanza unapokwisha, uwepo wao unakuwa wazi na usio na shaka wanapochukua nafasi zao kama Nota za sauti wakiimba: “Roho wa Bwana amenijaza.”
Na ilikuwa dhahiri kwamba Roho wa Bwana yuko kila mahali katika barabara zenye vumbi. Hata “chini ya miti” ambapo Padre Petro aliadhimisha Misa yake ya Dominika ya tatu kwa sababu kijiji hicho hakijajenga bado kile kinachoelezwa hapa kama: “kituo kidogo” yaani Kanisa dogo lenye paa la mabati. Katika kijiji kingine, kituo kidogo, au misheni, kilijaa kama Kanisa kubwa la pande zote huko Sukamahela. Waliimba pia, kama katika makanisa mengine yote tuliyoingia Tanzania. Katika muktdha huo ni kweli kwamba Kanisa la Tanzania linahitaji mapadre zaidi na kwamba vijijini kote nchini vinastahili mmoja mmoja. Ni wazi kuona kwamba kila Kanisa ni jumuiya na kwamba kila jumuiya ni familia.
Nje ya Kanisa la Sukamahela, Maria na Ethel walinishike mkono. Walimwomba Franco, mpiga picha wetu na video, achukue picha yetu na kisha kunielekeza na kucheka, kwa upendo, alipowaonesha picha hizo kwenye skrini.
Tulitumia saa chache zilizofuata pamoja na watoto wengine kutoka kijijini. Mama zao wote walikwenda nyumbani. Hawakuwa na chochote cha kuwa na wasiwasi kuhusu hilo kwani wanajua kwamba kanisa lao ni jumuiya na kwamba kila jumuiya ni familia.
Hata wageni wawili na kamera zao wazingeweza kuharibu imani yao au kuharibu mapatano yao.