Baraza la Vijana wa Mediteranea watembelea Bunge la Ulaya na COMECE
Vatican News
Tarehe 4 Aprili 2024 ziara ya taasisi za Ulaya, jijini Brussels,Ubelgiji ya Baraza la Vijana la Mediterania imemalizika, ambayo ilikuwa ni ishara ya kazi iliyozaliwa kufuatia Mkutano wa Maaskofu na Meya wa Mediterania ambao ulifanyika Firenze nchini Italia kuanzaia tarehe 23 hadu 27 Februari 2022. Ujumbe huo, uliofuatana na Askofu Mkuu Giuseppe Baturi, wa Jimbo Kuu Katoliki la Cagliari na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Italia (CEI), ulipokelewa na Roberta Metsola, rais wa Bunge la Ulaya, na Askofu Mkuu Mariano Crociata, rais wa Tume ya Maaskofu wa Umoja wa Ulaya (Comece), pamoja na Askofu Mkuu Noël Treanor, Balozi wa Vatican katika Baraza la Umoja wa Ulaya. Kwa hakika, ziara hiyo ilijumuisha kwenda sehemu mbili: katika makao makuu ya Bunge la Ulaya na ile ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Nchi za Umoja wa Ulaya(Comece.)
Mkutano na Metsola Rais UE
Kwa mujibu wa Askofu Crociata, Mkutano na Rais wa Baraza la Ulaya “ulikuwa ni uthibitisho wa uhusiano ambao Kanisa, kupitia Shirikisho lake la Maaskofu wa (Comece,) linao na Bunge la Ulaya, na ambao unastahili kuendelezwa kwa sababu unaliruhusu Kanisa kutekeleza utume wake na kwa Bunge kukusanya sauti zinazotoka katika ulimwengu wa Kikatoliki, ambao ni sehemu muhimu ya watu wa Ulaya.” Akiendela Askofu Baturi alisema Rais Metsola, “alitaka kujifunza zaidi kuhusu motisha na muundo wa Baraza la Vijana la Mediterania. Pia alipendezwa na maono makubwa ya Giorgio La Pira, huku akiomba kuweza kuyaendeleza katika muktadha wa kihistoria unaohitaji mtazamo huo wa kinabii na kukumbuka kuwa Umoja wa Ulaya ni mradi wa amani zaidi ya yote.”
Msaada wa uhuru, demokrasia na haki
Katibu mkuu wa Baraza la Maaskofu Italia CEI alitoa shukrani kwa rais wa Bunge la Ulaya kwa “kujitolea kwake kwa ushirikiano na maelewano kati ya watu na msaada wake kwa uhuru, demokrasia na haki.” Pamoja na Baraza la Vijana la Mediterania, alieleza Askofu Baturi kuwa “tulitaka kuwawekea kamari vijana kwa sababu hii inamaanisha kuweka kamari kwenye elimu, juu ya uwezo wao wa kufikiria mustakabali tofauti.
Ulaya haiwezi kushindwa kutambua kile kinachotokea katika Mediterania, nguvu hai na uwezekano ulio nao wa kuendeleza hatua ya amani na urafiki ambayo itakuwa na athari duniani kote. Kwa sababu hii, kwa upande mmoja tunataka vijana wetu kutoka nchi 18 wajue taasisi za Ulaya, kwa upande mwingine tunaomba kwamba taasisi za Ulaya zizingatie nguvu hizi hai na zinazotarajiwa zenye uwezo wa kuamua, tunatumai, mustakabali tofauti. Kujenga madaraja ya mazungumzo, umoja na amani kati ya watu na tamaduni.) Baraza linalotafutwa sana na kuungwa mkono na CEI, linalenga kutunza hali ya kiroho, kuimarisha utendaji wa kichungaji katika kukabiliana na changamoto za leo na kujenga uhusiano wa kidugu, kama ilivyoripotiwa kwenye tovuti ya vijana wa Mediteranea(www.giovanimediterraneo.org)ambapo taarifa na habari zinapatikana.
Zaidi ya hayo, tarehe 16 Aprili 2024 makao makuu ya Halmashauri yatazinduliwa huko Fiesole (Fi), Italia. Msingi, utume na shughuli ziliwasilishwa na Bodi, kama sehemu ya tukio la siku hiyo la “Kujenga madaraja ya mazungumzo, umoja na amani kati ya watu na tamaduni.” Kazi hizo, zilizoletwa na MEP Beatrice Covassi, zilihudhuriwa na Askofu Baturi, Askofu Mkuu Crociata na Patrizia Giunti, rais wa Mtandao wa Mare Nostrum na Mfuko wa La Pira.