Kard.Zuppi:Jumuiya ya Kimataifa isikilize miito ya Papa ya amani
Vatican News
Miito ya Papa kwa ajili ya amani nchini Ukraine na Mashariki ya Kati inawatazama wote hata kwa Juumuiya ya kimataifa. Rais wa Baraza la Maskofu Italia (CEI), na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Bologna, Kardinali Matteo Zuppi, katika tukio la kumbukizi ya Alcide Amedeo Francesco De Gasperi (aliyekuwa mwanasiasa wa Kiitaliano na mwanzilishi wa chama cha Demokrasia ya Kikristo na aliwahi kuwa waziri mkuu wa Italia katika serikali nane za muungano zilizofuatana kuanzia 1945 hadi 1953), alizungumza kando ya tukio hilo kuhusu takwimu za mwanzilishi wa Demokrazia ya Kikristo, ulioandaliwa na Mfuko aliouanzishwa jijini Roma.
Katika suala hilo alibainisha kwamba sehemu mbili zilizohusika katika vita, lakini hata sehemu ya tatu ile ya Ulaya ambayo ni tunda la amani hii, urithi wa kizazi ambao aliusishwa na De Gasperi.”Amani ndiyo maelekezo ya Kardinali Zupi kwamba ni muhimu indelezwe kujengwa kama mpango ambao aliouanzisha lakini pia ambao lazima ukue na kwende mbele.”
Kadinali alieleza kuwa, kuna hitaji la dharura la kuwa na Ulaya yenye nguvu zaidi: “Ulaya lazima iimarishe umoja wake ili wote wawe na uzito zaidi kama kambi ya amani katika ulimwengu uliosambaratishwa na vita, kwa ajili ya udugu huo wa ulimwenguni pote ambao bado ni wa lazima leo hii”. Unyeti wa De Gasperi na maono na njia yake, kwa maneno ya Kardinali Zuppi, lazima yahamasishe kila mtu, hasa wale wanaojihusisha na siasa kwa kufuata msukumo wa Kikristo, kwani De Gasperi hakua tu kumbukumbu inayotufanya kutazama zamani, lakini pia kutufanya tutazama ya sasa na tuchague yajayo.” Alisema Mkuu wa Baraza la Maaskofu Nchini Italia.