Tafuta

Dominika ya nne ya Kipindi cha Pasaka inajulikana kama Dominika ya Mchungaji Mwema, kama Yesu anavyo jiongelea mwenyewe kuwa ni “Mchungaji mwema.” Dominika ya nne ya Kipindi cha Pasaka inajulikana kama Dominika ya Mchungaji Mwema, kama Yesu anavyo jiongelea mwenyewe kuwa ni “Mchungaji mwema.” 

Tafakari Dominika ya Kristo Yesu Mchungaji Mwema Siku ya 61 ya Kuombea Miito

Ujumbe wa Papa Francisko katika Maadhimisho ya Siku ya 61 ya Kuombea Miito Mitakatifu unanogeshwa na kauli mbiu: “Tunaitwa kupanda mbegu za matumaini na kujenga amani.” Baba Mtakatifu anafafanua kuhusu watu walioko safarini mintarafu ujenzi wa Kanisa la Kisinodi na kutambua uwepo wa Roho Mtakatifu. Kama sehemu ya maadhimisho ya Mwaka wa Sala kwa ajili ya maandalizi ya Jubilei ya Mwaka 2025 anasema sala ndiyo nguvu na ufunguo wa matumaini.

Na Padre Joseph Herman Luwela, - Vatican.

UTANGULIZI: Kadiri ya Mwinjili Yohane Kristo anatumia “Mimi ndimi” mara saba kujielezea mwenyewe “Mimi ndimi Mkate wa uzima (6:35), Mimi ndimi nuru ya ulimwengu (8:12), Mimi ndimi mlango (10:9), Mimi ndimi Mchungaji mwema (10:11), Mimi ndimi ufufuo na uzima (11:25), Mimi ndimi njia, ukweli na uzima (14:6) na Mimi ndimi Mzabibu wa kweli (15:1)". Hapa anarejea Jina takatifu sana alilojitambulisha Mungu kwa kinywa chake kwa Musa, MIMI NDIMI NILIYE, kwa kiyahudi ‘Ehyeh asher Ehyeh’ (Kut 3:14) na hivi kwa “Mimi ndimi” hizi Yesu anarejelea zaidi umungu wake kuliko ubinadamu wake. Leo tunamtafakari Kristo “Mchungaji Mwema” tukiombea pia miito mitakatifu. Dominika ya nne ya Kipindi cha Pasaka inajulikana kama Dominika ya Mchungaji Mwema, kama Yesu anavyo jiongelea mwenyewe kuwa ni “Mchungaji mwema.” Yesu anatupa sura ya Mchungaji mwema anaye wafahamu kondoo wake: anawaita, anawalisha na kuwaongoza. Ni kwa sababu ya hili Kanisa limeipendekeza kuwa siku ya kuombea miito duniani. Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko katika Maadhimisho ya Siku ya 61 ya Kuombea Miito Mitakatifu ndani ya Kanisa unanogeshwa na kauli mbiu: “Tunaitwa kupanda mbegu za matumaini na kujenga amani.” Baba Mtakatifu anafafanua kuhusu watu walioko safarini mintarafu ujenzi wa Kanisa la Kisinodi unaosimikwa katika utamaduni wa kusikilizana na kutambua uwepo wa Roho Mtakatifu. Kama sehemu ya maadhimisho ya Mwaka wa Sala kwa ajili ya maandalizi ya Jubilei ya Mwaka 2025 anasema sala ndiyo nguvu na ufunguo wa malango ya matumaini.

Dominika ya Kristo Yesu Mchungaji Mwema
Dominika ya Kristo Yesu Mchungaji Mwema

Waamini ni mahujaji wa matumaini na wajenzi wa amani na kwamba, lengo kuu la safari ya maisha ni kuishi kwa haki, amani na upendo na kwamba, lengo na wito ni kuwa ni mashuhuda wa Injili ya matumaini kama sehemu ya ujenzi wa Ufalme wa Mungu, kwa kutoa kipaumbele cha kwanza kwa Kristo Yesu na Kanisa lake; umoja, amani na udugu. Kila mwamini ajitahidi kugundua wito wake sahihi katika Kanisa na Ulimwengu, kwa kuwa hujaji matumaini na wajenzi wa amani. Katika siku hii kila Mkristo mkatoliki na wote wenye mapenzi mema tunaalikwa kutafakari juu ya zawadi ya thamani ya wito wa Bwana kwa kila mmoja wetu, kama washiriki wa watu wake waaminifu wa hija, kushiriki katika mpango wake wa upendo na kuiga uzuri wa Injili katika hali tofauti za maisha. Kusikia wito huo wa Mungu, ambao ni mbali na kuwa wajibu uliowekwa - hata kwa jina la maadili ya kidini ni njia ya uhakika kwetu kutimiza hamu yetu ya kina ya furaha. Maisha yetu hupata utimilifu tunapogundua sisi ni nani, karama zetu ni nini, wapi tunaweza kuzifanya zizae matunda, na ni njia gani tunaweza kufuata ili kuwa ishara na vyombo vya upendo, kukubalika kwa ukarimu, uzuri na amani, popote tunapojikuta.

Siku ya 61 ya Kuombea Miito Mitakatifu
Siku ya 61 ya Kuombea Miito Mitakatifu

UFAFANUZI: Katika somo la kwanza, lililochukuliwa kutoka katika Kitabu cha Matendo ya Mitume wahusika wakuu ni Paolo na Barnaba. Je, tunaweza kusema mitume wawili ni Wachungaji.? Yesu anaonesha wazi tofauti ya wachungaji. Tofauti anayotoa ni juu ya mchungaji yule anaye wafahamu kondoo wake na kuwajali, na wale wanaofuata tu mkumbo bila sadaka ya upendo. Yesu alitolea sadaka kamilifu kama Mchungaji wa Kimungu. Alikuwa yupo tayari kutembea nasi katika njia zote, sisi kondoo wake. Alikuwa yupo tayari kutoa sadaka ya kila kitu. Hakutaka mateso, kuonewa, kukataliwa na mambo mengine yamuondoe kutoka katika lengo lake la kuwajali na kuwatunza watu wake katika njia kamili. Inapaswa ituguse na sisi, kutufariji na kutupatia sisi ujasiri na kutambua ni kwa jinsi ghani upendo wake ulivyokuwa mkubwa kwetu. Katika Agano la Kale watu wengi maarufu walikuwa wachungaji: Yakobo, Musa, Daudi na wengine. Mungu amejulikana kama “Mchungaji wa Israel” anayewaongoza watu wake Israel kama kondoo, anawaponya majeraha, anawabeba kondoo wadogo na wasiojiweza, anawatafuta wanapopotea miambani na porini, kondoo hawapungukiwi kitu, katika majani mabichi huwalaza na kando ya maji ya utulivu huwaongoza, hawaogopi mabaya maana Yeye yupo pamoja nao kuwafariji (zab 23:1-2, 80:2, Eze 34, Yer 23:1-6). Yesu anatumia taswira hii kwake mwenyewe, “Mimi ndimi Mchungaji Mwema” (Yn 10:11,14), kwamba Yeye ndiye Mkombozi mtarajiwa na kwa hiyo… ukombozi umekwisha fika.

Hiii ni Dominika ya Kristo Yesu Mchungaji mwema
Hiii ni Dominika ya Kristo Yesu Mchungaji mwema

Tunachukuliwa kama kondoo katika zizi la Mungu, Kanisa. Sifa ya kondoo ni upole na usikivu. Hata hivyo wapo kondoo waoga wanaopaniki kirahisi kabisa, kondoo wengine wajinga, wanadanganyika kirahisi, wapo wanaofuata mikumbo, wengine hawawezi kujilinda wala kujitetea, wengine hawavutii, wengine wanaelewa polepole mno, wanadhurika kirahisi, wapo wenye madai mengi, wabishi, wasiosikia, wasiotabirika na wasio na utulivu... mazingira ya hivi yanahitaji Mchungaji makini, Mchungaji mwema. Tunachukuliwa kama kondoo katika zizi la Mungu, Kanisa. Sifa ya kondoo ni upole na usikivu. Hata hivyo wapo kondoo waoga wanaopaniki kirahisi kabisa, kondoo wengine wajinga, wanadanganyika kirahisi, wapo wanaofuata mikumbo, wengine hawawezi kujilinda wala kujitetea, wengine hawavutii, wengine wanaelewa polepole mno, wanadhurika kirahisi, wapo wenye madai mengi, wabishi, wasiosikia, wasiotabirika na wasio na utulivu... mazingira ya hivi yanahitaji Mchungaji makini, Mchungaji mwema ulivyokuwa mkubwa kwetu. Wakati upendo aliotoa mmoja kwa ajili yetu ni kamili, tena wakati wa wakati mgumu, huu ni msaada mkubwa. Na upendo unaotolewa kwa mwingine kama huu unatengeneza muunganiko wa kiroho ambao ni imara kuliko matatizo tunayo weza kukutana nayo. Haijalishi ni kitu ghani kigumu kinachoweza kuja katika njia zetu, tunapaswa kutambua upendo na msaada usio na kikomo kutoka kwa Mchungaji wetu mwema. Na kama tunaweza kuona upendo huo kamili kutoka kwa wengine, tunakuwa kweli tumebarikiwa mara mbili.

Mwombeni Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi wema na watakatifu
Mwombeni Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi wema na watakatifu

Katika hali nyingine Yesu anaongea kuhusu mfano wa mtu mwingine ambaye sio mchungaji mwema, ambaye anaona mbwa mwitu wakija na yeye hukimbia. Tunapaswa kuona ndani ya mtu huyu, vishawishi vyote ambavyo vyaweza kuja katika maisha yetu. Ni vigumu kubaki wakati wa nyakati ngumu. Ni vigumu kuwa karibu na wale wenye shinda wanapo tuhitaji sisi. Ni vigumu kuwa waminifu mpaka mwisho bila kuwa na aibu tunapo kukutana na vishawishi vya hofu. Yesu anatupa nguvu na msaada wa upendo kamili yeye akiwa kama Mchungaji wetu mwema, lakini pia anatuhitaji nasi turudishe upendo huu huu kwake, kwa kuwapatia wengine upendo huu huu mkamilifu. Pale ulipo shindwa na kupungukiwa tunamuomba yeye akuchunge kama mchungaji ili nawe uweze kuwachunga wengine. Mkimbilie mchungaji mwema na amini upendo wake kwako. Baba Matakatifu Fransisko, katika ujumbe wake wa siku hii anaendelea kusema: “Ninawafikiria kina mama na baba ambao hawajifikirii kwanza au kufuata fads za muda mfupi za wakati huu, lakini wanatengeneza maisha yao kupitia mahusiano yaliyotiwa alama na upendo na neema, uwazi kwa zawadi ya maisha na kujitolea kwa watoto wao na ukuaji wao katika ukomavu. Yesu kama mchungaji mwema hasimami kama mtu mwenye upole usio na maana, anayeridhika na kutazama tu kondoo wake wanapofikwa na hatari. Picha ya Mchungaji mwema ni ya mtu hodari, mkali na shujaa kama Daudi (1Sam 17:34-35). Yupo tayari kuyatoa maisha yake kwa ajili ya kondoo (Yn 10:11).

Malezi na Majiundo makini ni muhimu katika maisha na wito wa mapadre
Malezi na Majiundo makini ni muhimu katika maisha na wito wa mapadre

Zifuatazo ni sifa za Mchungaji mwema: ni mwema, ni mlinzi, mwongozaji, mlishi, mgawaji wa uzima, yu tayari kutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo wake. Leo, Kanisa zima linatukumbusha hitaji letu la kuomba, kama Yesu mwenyewe alivyo waambia wanafunzi wake, hivyo kwamba "mwombeni Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi katika mavuno yake" (Lk 10: 2). Tangu hapo awali Kanisa “ kwa asili yake ni umisionari" (Ad Gentes, 2), wito wa Ukristo unazaliwa ndani ya watu kutokana na kazi ya umisionari. Kusikia na kufuata sauti ya Kristo Mchungaji mwema, maana yake ni kuruhusi tuvutwe naye na tuongozwe naye, kujiweka wakfu kwake maana yake kumruhusu Roho Mtakatifu kututumia sisi katika mabadiliko haya ya umisionari, na kuamsha ndani yetu tamaa, furaha na ujasiri wa kutoa maisha yetu wenyewe katika utumishi wa Ufalme wa Mungu. Hapa aneendelea kusema ‚‘Kwa wakati huu, basi, safari yetu ya kawaida inatuleta kwenye Mwaka wa Jubilee wa 2025. Hebu tusafiri kama mahujaji wa matumaini kuelekea Mwaka Mtakatifu wa Jubilei ya Miaka 2025 ya Ukristo, kwa kugundua wito wetu wenyewe na mahali pake katikati ya karama tofauti zilizotolewa na Roho, tunaweza kuwa kwa wajumbe wetu wa ulimwengu na mashahidi wa ndoto ya Yesu ya familia moja ya kibinadamu, iliyoungana katika upendo wa Mungu na katika kifungo cha upendo, ushirikiano na udugu. Wafuasi wa mchungaji wa aina hii ni akina nani? Je, ni wale waliobatizwa na kuorodheshwa katika vitabu vya sakramenti ofisini na wanaotambuliwa na JNNK? Je, ni wale wasio na ubishi kwa Paroko na wepesi wa shughuli za Kanisa? Tazama, wafuasi wa kweli wa Kristo Mchungaji mwema ni wote wenye moyo wa ujasiri wa kujitoa kwa ajili ya kaka na dada zao katika Kristo.

Pandeni mbegu za matumaini na jengeni amani
Pandeni mbegu za matumaini na jengeni amani

Katika mzizi wa kila wito wa Kikristo tunaona harakati hii ya msingi, ya kuacha nyuma faraja yetu na mambo yote yanayo tupendezesha nafsi zetu na kujikita katika maisha ya Yesu Kristo. Ina maana ya kuondoka, kama Abrahimu, na kuacha sehemu yetu ya asili na kwenda mbele kwa uaminifu, tukijua kwamba, Mungu atatuonesha njia ya nchi mpya. Hii "kwenda mbele" isi tazamwe kama ishara ya mpango tu wa maisha ya mtu binafsi, hisia ya mtu, utu wa mtu mwenyewe. Kinyume chake, wale ambao wanamfuata Kristo wanapata uzima kwa wingi kwa kujiweka wenyewe bila kujibakiza katika utumishi wa Mungu na ufalme wake. Wito wa Kikristo kwanza kabisa ni wito wa upendo, upendo ambao hutuvuta sisi na kutuelekeza nje ya sisi wenyewe. Kuitika wito wa Mungu, maana yake kumruhusu yeye atusaidie kujiacha wenyewe kwakuondokana na usalama wetu wa uongo, na kutoka nje na kuenenda kwenye njia inayo ongoza kwa Yesu Kristo, aliye asili na hatima ya maisha yetu na furaha yetu. Ni nini kinampata mmoja anapokuwa kondoo wa Yesu? sio sisi tunaomtafuta Mungu bali ni Mungu mwenyewe ndiye anatutafuta na kutuita, “kondoo wangu waisikia sauti nami nawajua, nao wanifuata”. Wafuasi wa Yesu Mchungaji mwema wanaishi duniani na watu wengine. Dunia ina sauti nyingi, na nyingine kiukweli ni kelele zaidi kuliko sauti za kueleweka. Sauti/kelele hizo zinatoka kwa “wachungaji” wenye ahadi za uponyaji, ushindi, furaha, mali, vyeo, umaarufu na maisha ya raha na fanaka kwa wafuasi wao. Tutaitambuaje sauti ya Yesu Mchungaji wa kweli katikati ya kelele hizi zote? Ni kwa kuyazoesha masikio yetu kuijua sauti yake. Ukimsikiliza mtu mara moja na halafu humsikii tena kwa mwaka mzima hutaweza kuijua sauti yake. Tutaijua na kuizoea sauti ya Yesu Mchungaji mwema anayeongoza yote yahusuyo maisha yetu kwa kumsikiliza mara nyingi kwa njia ya sala, sakramenti na Neno la Mungu.

Tunaitwa kupanda mbegu za matumaini na kujenga amani
Tunaitwa kupanda mbegu za matumaini na kujenga amani

Ni wachungaji gani wa kuwaamini? maaskofu, mapadre, watawa na makatekista? ni sawa, lakini kwa taarifa tu kila mbatizwa ni mchungaji miongoni mwa kondoo wa Yesu. Mzazi anayetimiza wajibu wake kwa upendo na uvumilivu ni mchungaji mwema, mwalimu anayefundisha kwa moyo na uvumilivu ni mchungaji mwema, mfanyabiashara asiyetaka faida ya dhuluma ni mchungaji mwema, classmate anaye share vitabu na material yake special kwa wenzake ni mchungaji mwema, mfanyakazi anayepatana na kucheka na wote kule ofisini ni mchungaji mwema, baba anayewafundisha watoto namna ya kuyaishi malimwengu ni mchungaji mwema na mama anayevumilia yote kwa ajili ya Yesu ni mchungaji mwema. Kuwa mchungaji ni kuuishi wito wetu, leo ni siku ya kuombea miito. Wazazi wana nafasi ya kueneza miito kwa mfano mzuri wa maisha ya ndoa, mapadre kadhalika, watawa na makatekista. Vijana na watoto wawe wasikivu wenye kufundishika. Yesu Mchungaji mwema amesema “Mimi na Baba tu umoja”. Ili kuunganika na Mungu Baba ni lazima tumsikilize na kuwa “wamoja” na Yesu katika Roho Mt. Yaani, ni lazima tujitahidi kuwa na mawazo kama ya Yesu, kuiga tabia zake, kupita njia zake, kuzungumza kama Yeye, kuwa na mipango kama yake, kusema na kutenda kama Yesu. Kila mmoja aweke nia ya kubadilika na kuanza upya maisha yake ya imani kadiri ya kauli mbiu “mabadiliko yaanzie kwangu!”

Watawa wawe ni mashuhuda wa tunu msingi za Kiinjili
Watawa wawe ni mashuhuda wa tunu msingi za Kiinjili

Katika siku hizi kwanza tunaombwa tuombee Kanisa liweze kupata wachungaji wema na waadilifu wa kufanya kazi ya Kristo ya kueneza Injili, na kwamba Kanisa liweze kupata vijana wengi wanoitwa kwenye wito wa upadre na utawa ikiwa ni pamoja na watoto wetu wenyewe. Kuwa mahujaji wa matumaini na wajenzi wa amani, basi, inamaanisha kuweka msingi wa maisha yetu kwenye mwamba wa ufufuo wa Kristo, tukijua kwamba kila juhudi iliyofanywa katika wito ambao tumekumbatia na kutafuta kuishi kwa kudhihirisha, kamwe haitakuwa bure.   Kushindwa na vikwazo vinaweza kutokea njiani, lakini mbegu za wema tunazopanda zinakua kimya kimya na hakuna kitu kinachoweza kututenganisha na lengo la mwisho: kukutana kwetu na Kristo na furaha ya kuishi milele katika upendo wa kidugu. Anakazia Papa Francisko Basi, tuamke na tuweke kama mahujaji wa matumaini, ili, kama Maria alivyokuwa kwa Elizabeti, sisi pia tunaweza kuwa wajumbe wa furaha, vyanzo vya maisha mapya na mafundi wa udugu na amani.

D. Mchungaji Mwema
20 April 2024, 09:35