Erfurt:Siku ya 103 ya Kikatoliki Ujerumani imeanza na ujumbe wa Papa
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Takriban wageni 6,000 walikusanyika katika eneo la Kanisa kuu la mji mkuu wa Thuringia, ambapo asilimia saba tu ya wakazi wanadai kuwa na imani ya Kikatoliki na chama cha siasa kali za mrengo wa kulia,(AfD) kilizidi asilimia 20 ya kura. Papa Francisko na mkuu wa serikali ya Ujerumani wamerejea, angalau kwa njia isiyo ya moja kwa moja, kuhusu uchaguzi ujao wa Ulaya.
“Wakristo lazima wachukue msimamo dhidi ya kutengwa. Lakini pia tunataka kufanya kampeni ya umma na ya kisiasa ili kuboresha hali ya maisha na, hasa, kutoa sauti kwa wale wasiosikilizwa. Amani haiwezekani bila haki. Sio Ulaya tu, bali pia katika sehemu nyingine za dunia, haki za kimsingi za binadamu kwa sasa zinaonekana kuwa hatarini: kwa kuongezeka kwa chuki dhidi ya Wayahudi, ubaguzi wa rangi na itikadi nyinginezo zinazoelekea itikadi kali na vurugu.” Aliomba Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake. Papa aidha aliandika kuwa: “Migogoro mingi ya kiadili, kijamii, kiuchumi na kisiasa tunayopitia yote yana uhusiano.” Matatizo huathiri kila mtu na yanaweza tu kutatuliwa pamoja, katika mazungumzo mapana yenye sauti nyingi iwezekanavyo. Matukio mengi ya majadiliano katika Katholikentag yenye wawakilishi wengi wa ngazi ya juu na sekta muhimu za maisha ya kijamii hutoa fursa nzuri kwa hili," Francis alisema.
Steinmeier anaonya dhidi ya kutojali kidini
Katika hotuba yake ya ufunguzi, Rais wa Shirikisho la Ujerumani Bwana Steinmeier alisikitishwa na upotevu mkubwa wa imani katika makanisa. “Tunahitaji kuzungumza juu ya mabadiliko ya bahari," alisema. Hata hivyo, kwa maoni yake, Wakristo wanaendelea kutoa mchango muhimu kwa mshikamano nchini Ujerumani. Ni bahati kwa jamii yetu yote,” alisisitiza mkuu wa nchi, ambaye aliwashukuru Wakatoliki kwa kujitolea kwao katika Kanisa na katika jamii. Hata hivyo, katika sekta kubwa za jamii kunakuwa na hali ya kutojali dini na kile kinachopita zaidi ya maisha.
Steinmeier, ambaye alikuwa amevaa skafu ya zambarau ya Katholikentag, aliuliza, bila kukasirika kuwa: “Je, Makanisa yanatoa msukumo mdogo sana hapa? Je, ujumbe wao ni kimya sana, rangi sana, hadhi ya chini sana?” Na tena, kuhutubia watu ambao wanatafuta maana: "Je, watafutaji hawa wa dhati wanapata majibu ya kushawishi, wanapata uwezo wa kiroho, wanapata usaidizi wa huruma katika vikundi, jumuiya na mipango yetu?”
Nia ya kubadilisha mawazo
Askofu, Ulrich Neymeyr, wa Erfurt alielezea matumaini kwamba mkutano wa Kikristo katika jiji hilo unaweza kutoa msukumo kwa amani katika ulimwengu wetu, katika jamii yetu na katika Kanisa letu. Na akaongeza: “Tufanye mazoezi ya kupima na kutathmini hoja. Tujizoeze kubadilisha mawazo yetu." Rais wa Katholikentag, Irme Stetter-Karp, hapo awali alitoa wito kwa kila mtu kutetea demokrasia, ambayo ilitishiwa sana. Bila kutaja Chama cha AfD, Stetter-Karp alielezea uamuzi wenye utata wa kutokualika watu kutoka chama hiki kwenye vikao: “Watu wanaojipanga katika vyama vinavyozingatia kutengwa na utaifa wa völkisch hawana nafasi kwenye madawati yetu. Tunachora mstari wazi."
Washiriki 20,000 wanatarajiwa
Kauli mbiu ya Siki ya Kikatoliki Ujerumani(Katholikentag) katika mwak 2024 wa uchaguzi mkuu ni "The future belongs to people of peace" yaani “Wakati ujao ni wa watu wa amani.” Hafla hiyo itaendelea hadi Dominika tarehe 2 Juni 2024 na inagharimu karibu euro milioni saba. Zaidi ya washiriki 20,000 wanatarajiwa. Kansela wa Shirikisho Olaf Scholz (SPD) na mawaziri kadhaa wa shirikisho pia wanapanga kufika Erfurt. Siku ya Katholikentag itahitimishwa kwa hiyo Dominika kwa Ibada ya Misa Takatifu.