Tafuta

Mafuriko makali yameacha mji wa serikali ya Rio Grande do Sul katika hali ngumu huko Brazil. Mafuriko makali yameacha mji wa serikali ya Rio Grande do Sul katika hali ngumu huko Brazil.  (AFP or licensors)

Kanisa la Hungaria limetoa msaada huko Brazili kufuatia na mafuriko makali

Baraza la Kudumu la Maaskofu nchini Hungaria limeamua kutoa msaada wa haraka wa dola za kimarekani 14.035,88 kwa ajili ya Parokia ya Mtakatifu Martin katika serikali ya Rio Grande do Sul kusaidia wenye kuhitaji kwa chakula,mavazi na vifaa vya usafi.Ni katika kuingilia kati dharurua ya mafuriko makali nchini Brazil

Vatican News

Baraza la Maaskofu nchini Hungaria, linaingia kwenye uwanja kwa ajili ya kusaidia nchi ya Brazil iliyokumbwa na mafurikio makali mwanzoni mwa mwezi Mei 2024. Kwa njia hiyo Baraza la Kudumu la Maaskofu hao, wametoa taarifa kuwa limeamua kutoa msaada wa haraka wa dola za kimarekani 14.035,88 kwa Parokia ya Mtakatifu Martino (Páróquia São Martinho), katika serikali ya Rio Grande do Sul, ili weze kuendelea kusaidia wehitaji kwa chakula, nguo, na vifaa vya usafi, vitu ambavyo kwa sasa vinakosekana.

Makazi na miundo mbinu vimemeharibiwa kutokana na mvua kazi
Makazi na miundo mbinu vimemeharibiwa kutokana na mvua kazi

Kwa mujibu wa taarifa za utoaji msaada huo tunasaoma kuwa: “Tuna huruma nyingi na tunawabeba mioyoni mwetu wathiriwa na wale wote walioathiriwa na mafuriko ambayo yaliyoharibu huko Brazil mnamo Mei 2024.” Aidha wanabainisha kuwa  “Tangu mwanzoni mwa Mei, jimbo la kusini mwa Brazil limeathiriwa na mvua kubwa ambayo inasababisha mafuriko ambayo hayajawahi kuonekana hapo awali.”Kufikia sasa, maafa hayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 100, zaidi ya watu 100 wametoweka na mamia ya maelfu ya wakaazi wamelazimika kuacha nyumba zao, wakiwemo waamini wa Parokia ya Martin.”

Mji umeharibiwa vibaya na mafuriko huko Brazil
Mji umeharibiwa vibaya na mafuriko huko Brazil

Jumuiya hiyo ilianzishwa mnamo mwaka wa 1968 na Padre László Molnár, ambaye sasa ana umri wa miaka 93, Padre kutoka Hungaria aliyekimbilia Brazili wakati wa ukomunisti mnamo mwaka 1956. Tangu siku za kwanza za janga hilo, Parokia hiyo imekuwa ikikaribisha watu wengi ambao nyumba zao ziliharibiwa na mafuriko. Kwa hivyo, msaada wa haraka wa kukabiliana na dharura unahitajika. Mafuriko makubwa katika jimbo la kusini mwa Brazil la Rio Grande do Sul yalisababisha vifo vya watu wengi sana na wengine kupotea bila kujulikana walipo. Mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa zilizonyesha kwa siku kadhaa yaliyosababisha maporomoko ya udongo, kusomba barabara na kuvunja madaraja ya jimbo hilo.

Kanisa la Hungaria limetoa msaa huko Brazil
31 May 2024, 16:03