Maadhimisho ya miaka 80 ya ibada kwa Bikira Maria Afya ya Waroma!
Vatican News
Mnamo mwaka 1944 jijini roma, vita vilikuwa vikipamba moto na wakati huo, Waroma walijikuta wakiwa pamoja katika sala mbele ya Picha Takatifu. Na hasa katika ile picha pendwa sana ya Upendo wa Kimungu, (Divino Amore) juu ya Mnara ulioharibiwa. Papa Pio XII, alikuwa akihofia kuwa ingeweza kuharibiwa na mabomu hivyo, ili kuhifadhi, alifanya ihamishwe kutoka Madhabahu ya Nyumba ya Kifalme ya Leva hadi katikati mwa jiji la Roma. Kwanza ilikaribishwa katika Kanisa dogo katika Uwanja wa Fontanella Borghese; kisha, mnamo mwezi wa Mei, kutokana na kufurika kwa wingi kwa waamini, iliamuliwa kuihamishia Mtakatifu Lorenzo, huko Lucina na tena hadi Mtakatifu Ignatius wa Loyola huko Campo Marzio.
Hapo, mnamo tarehe 4 Juni 1944, maelfu ya watu, miongoni mwao ni pamoja na waamini na makuhani, walitamka kiapo cha kiraia ibada kwa Mama Maria, ili jiji liepushwe na vita. Na ndivyo hasa inavyotokea, kwani kwa karibu ya saa 1 za jioni kundi la askari washirika, waliingia Roma bila kupata upinzani hata kidogo kutoka kwa Wajerumani, ambao waliondoka na kuacha mji wa kaskazini. Siku iliyofuata, mnamo tarehe 5 Juni 1944, umati ulimiminika kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro, mjini Vatican ambapo Papa Pio XII alitamka maneno haya: “Kwa shukrani isiyoelezeka tunamheshimu Mama Mtakatifu wa Mungu na Mama yetu, Maria, ambaye anawapatie yeye na utukufu wa(Salus Populi Romani)Afya ya Watu waroma, uthibitisho mpya wa wema wake wa uzazi, ambao utabaki katika kumbukumbu ya kudumu katika kumbukumbu za Jiji.”
Sherehe katika maeneo manne katika mji mkuu yamepangwa
Ni katika sehemu zile zile husika za kihistoria wakati wa kuweka kiapo au ibada mnamo mwaka 1944. Maadhimisho hayo yataanza Jumamosi tarehe 1 Juni 2024 katika Kituo cha Padre Orione kupitia njia ya Camilluccia, Roma ambapo inatarajiwa saa 11.00 jioni, kufanyika ukumbusho wa kihistoria katika parokia ya Mtakatifu Maria Mama wa Mungu kwa kuongozwa na Padre Flavio Peloso, Msimamizi Mkuu wa Shirika ; saa 12.00 jioni kutakuwa na maandamano kuelekea Kwa mana na sala ya Rozari; wakati huo huo tena, saa 1 usiku kutakuwa na maadhimisho ya Ekaristi Takatifu, itakayohushwa na Kwaya ya Jimbo kuu la Roma na kuongozwa na Kardinali Enrico Feroci, Msimamizi Mkuu wa Madhabahu ya Upendo wa Mungu. Mwishoni mwa Misa Takatifu kutakuwa na zawadi ya kutoa maua kwa Bikira Maria , ambayo yalitengenezwa mnamo mwaka wa 1953 kwa ajili ya kumbukumbu ya matukio ya mwaka 1944, ili yaweze kuonekana kwa jiji lote.
Tena, Jumanne tarehe 4 Juni 2024 kutakua na kukumbukwa kwa ibada maalumu katika Kanisa la Mtakatifu Ignazio huko Campo Marzio: saa 12.00 jioni ambapo Makamu wa jimbo la Roma, Askofu Baldo Reina, ataongoza Sala ya Rozari itakayoongozwa na Jumuiya ya Upendo wa Mungu na saa 12,30 jioni ataadhimishwa Misa takatifu. Jumamosi tarehe 8 Juni 2024, katika Kanisa la Mtakatifu Maria Mkuu kutakuwa na , maadhimisho ya Ekaristi Takatifu saa 12.00 jini ambayo itaongozwa na Kardinali Stanislaw Rylko, Askofu Mkuu wa Kanisa kuu la Liberia; saa 1.30 jioni, inatarajia sala ya Rozari takatifu pamoja na Askofu Mkuu Rolandas Makrickas, Msimamizi wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu.
Hitimisho tukio hili litakuwa Dominika tarehe 9 Juni 2024 katika Madhabahu ya Mungu Upendo (DIVINO AMORE) huko Castel di Leva. Hapo, saa 5.00 asubuhi, Kardinali Feroci ataongoza Ibada ya Misa Takatifu itakayohitimisha, kumbukizi hili ambapo miongoni mwa wale watakaokuwapo ni pamoja na Askofu Dario Gervasi, Askofu msaidizi wa Kitengo cha Kusini, jijini Roma. Kisha kutakuwa na maandamano yenye heshima ya maua kwenye Mnara wa Muujiza wa Kwanza, yakisindikizwa na bendi ya muziki ya Upendo wa Mungu.