Tafuta

Katika Semina kuhusu Utadunisho wageni wapatao 100,wakiwemo mapadre, wasomi na walei,walishiriki katika vipindi mbalimbali vya masomo na kutembelea Xiamen, mji wa Zhangzhou. Katika Semina kuhusu Utadunisho wageni wapatao 100,wakiwemo mapadre, wasomi na walei,walishiriki katika vipindi mbalimbali vya masomo na kutembelea Xiamen, mji wa Zhangzhou. 

China:Kanisa la Taiwan na China bara wafanya Semina kuhusu utamadunisho!

Semina kuhusu utamadunisho imefanyika iliyotayarishwa kwa pamoja na Maaskofu na wasomi wa Kanisa la Taiwan na Kanisa la China Bara kuanzia tarehe 22 -25 Mei 2024.Walioshiriki walikuwa na uingiliaji kati wa mijadala kuhusu mada kuu:“Asili ya kihistoria,maendeleo ya Kanisa na mchakato wa kukuza Ukatoliki huko Fujian na Taiwan.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kutembea pamoja kwa upendo, mkono kwa mkono: ndiyo  mada ya Semina ya Utamadunisho  iliyofanywa kwa pamoja na Maaskofu na wasomi wa Kanisa la Taiwan na Kanisa la China Bara. Semina hiyo ilifanyika katika Jimbo la  Xiamen kuanzia tarehe 22 hadi 25 Mei 2024.  Askofu Giuseppe Cai Bingrui, wa  Jimbo katoliki la  Xiamen, aliwakaribisha kwa uchangamfu kaka  na dada wa ujumbe mkubwa kutoka Taiwan, wakiongozwa na Askofu  John Baptist Huang Min-Cheng, (O.F.M.)  wa Jimbo la Tainan na Askofu Mkuu Thomas Chung Anzhu, wa Jimbo Kuu la  Taipei. Kwa mara ya kwanza jumuiya za Kikatoliki za Fujian na Taiwan zilishiriki uzoefu sawa wa kubadilishana na ushirikiano katika mfumo wa semina ya kitaaluma.

Njia ya Kanisa kuanzia Tangazo la Injili hadi maisha ya kawaida

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirika la Kipapa la Habari za Kimisionari Fides, lilibanisha kuwa wageni wapatao 100, wakiwemo mapadre, wasomi na walei, walishiriki katika vipindi mbalimbali vya masomo na kutembelea Xiamen, mji wa Zhangzhou na maeneo mengine kwa pamoja. Katika wakati huu wa Ushirika, mapadre 15, wasomi, wataalam kutoka majimbo ya Xiamen, Tainan na Kiayi, pamoja na wasomi kutoka Chuo Kikuu cha Xiamen, Chuo Kikuu cha Huaqiao na Chuo Kikuu cha Furen (chenye makao yake huko Taipei) walishiriki uingiliaji kati na mijadala kuhusu mada kuu ya “Asili ya kihistoria, maendeleo ya Kanisa na mchakato wa kukuza Ukatoliki huko Fujian na Taiwan.” Kuanzia tangazo la Injili, maisha ya ushirika na pia mazoezi ya imani, washiriki wa Semina hiyo waliifuata tena njia ya Kanisa kuanzia asili ya kihistoria ya Ukatoliki katika pande zote za Mlango wa Bahari wa Taiwan, wakikumbuka pia mwingiliano baina ya pande hizo mbili na matokeo yaliyopatikana na Makanisa husika katika mchakato wa kuelimisha iliyoiliyohamasishwa katika muktadha wa Kichina, kuanzia mizizi yake katika Mapokeo.

Hija katika maeno muhimu katika siku kuu ya Maria Msaada wa Wakristo

Tarehe 24 Mei, ilikuwa ni Siku kuu ya Mtakatifu Maria Msaada wa Wakristo na tarehe ambayo uhadhimishwa  Siku ya Kuombea Kanisa nchini China, duniani, wajumbe wa Taiwan walifanya hija huko Gaopu, Jimbo kuu la Xiamen, alikozaliwa Askofu Joseph Cheng Zaifa, ambaye alifariki mnamo mwaka 2022, ambaye pia alikuwa ameongoza Jimbo Kuu la Taipei kuanzia mwaka 2004 hadi 2007. Baada ya kutembelea makanisa na bandari ya kibiashara, tukio lilihitimishwa kwa ibada ya Ekaristi iliyohitimishwa katika Kanisa la Hou Ban, mahali alipozaliwa Mkatoliki Li Buchi, ambaye aliwasili Taiwan mnamo mwaka 1859 na anatambulika kama mwanzilishi wa awamu ya pili ya uinjilishaji wa kisiwa hicho pamoja na Wadominikani wa Hispania, ambao walikuwa wakifanya kazi katika jimbo la Fujian kwa karne mbili.

Semina ya Utamadunisho China
01 June 2024, 10:42