Kozi kwa ajili ya mapadre,watawa na walei,njia ya kujifunza mtindo na desturi za Sinodi
Vatican News
“Njia ya Kisinodi ni njia ambayo Mungu anatarajia kutoka katika Kanisa la milenia ya tatu.” Haya ni maeno ambayo alisisitiza mara kadhaa Papa Francisko, lakini je tunawezaje kuwasaidia watu wa Mungu kuanza njia hii? Kuna changamoto nyingi, kuanzia na kuelewa maana ya sinodi na kisha kuendelea na mafunzo ya vipengele vyake vyote kwa njia hiyo ya kuwa Kanisa. Jitihada mbalimbali hata hivyo zimejitokeza na baadhi zaidi katika ngazi ya kitaaluma, nyingine zaidi ya kichungaji, kila moja kwa lengo la kuunga mkono mabadiliko ya mawazo ambayo mtindo wa sinodi unahitaji.
Kozi inayotolewa na Kituo cha Evangelii Gaudium
Miongoni mwa mipango hiyo ni kozi ya Sinodi iliyohamasishwa, kwa mwaka wa tatu mfululizo,na Kituo cha Elimu ya Juu cha Evangelii Gaudium (CEG -Injili ya Furaha) cha Taasisi ya Chuo Kikuu cha Sophia cha Loppiano(Florence),(Cha Wafokolari, nchini Italia kwa ushirikiano na Sekretarieti Kuu ya Sinodi. Ratiba inayopendekezwa ya mafunzo ya Taalimungu na kichungaji kwa lugha nyingi inalenga mapadre, mashemasi, watawa wa kike na kiume, Walei- wahudumu wa kichungaji wa kike na kiume. Somo la kwanza litaaanza siku ya Jumatatu tarehe 4 Novemba 2024 kuanzia saa kumi na mbili jioni (12.00) hadi saa Mbili ( 2.00) usiku.
Uchambuzi wa kina wa vipengele vya kitaalimungu na kichungaji
Kupitia mfululizo wa mihadhara na kazi ya kikundi ndani ya muktadha wa tamaduni na taaluma mbalimbali, kozi hii inataka kutoa zana za kichungaji na kitaalimungu kwa ajili ya utekelezaji wa mtindo na utendaji wa sinodi, katika ngazi ya kibinafsi na ya jumuiya, katika njia ya kuishi na kuwa Kanisa. Kuna hatua 4 za masaa 21 kila moja ambayo kozi imeundwa, lakini pia inawezekana kushiriki katika hatua moja tu. Ya kwanza ina mada yake: “Njia zilizofunguliwa na Mkutano wa Kawaida wa XVI wa Sinodi kuanzia (Novemba/Desemba 2024).” Hatua ya pili itashughulikia “mazoea mapya katika sinodi na Kanisa la kimisionari kuanzia (Januari/Februari 2025).
Kichwa cha hatua ya tatu ni “uanzishaji wa Kikristo na uenezaji wa imani kwa mtindo wa sinodi kuanzia(Machi/Aprili 2025).” Na hatimaye hatua ya nne inajumuisha “warsha za kisinodi, kibinafsi na kupitia mtandaoni kuanzia (Mei 2025).” Aidha Taasisi ya Chuo Kikuu cha Sophia, itatoa katika shule ya sinodi juu ya mada: “Kuitwa katika utume,” ambapo masomo kupitia mtandaoni yenye tafsiri katika lugha nyingi.
Kwa njia hiyo masomo yatafanyika kuanzia Jumatatu saa 10.00 jioni hadi saa 3.00 usiku, mtandaoni kwenye jukwaa la Zoom (moja kwa moja na kuahirishwa) na tafsiri katika Kiingereza, Kihispania na Kireno. Wanafunzi wataweza kupata ECTS 3 kwa kila hatua(kwa wajibu wa saa nyingine za kusoma na kufanyia kazi ya mwisho). Kwa wasikilizaji bila kufanyia kazi badala yake watapata cheti cha ushiriki. Usajili ulifunguliwa mnamo tarehe 17 Juni 2024 na kwa maelezo zaidi unaweza kuingia katika tovuti ya (Evangelii Gaudium Center,) yaani Kituo cha Evangelium Gudium-Furaha ya Injili): https://www.sophiauniversity.org/en/centro-evangelii-gaudium/;
https://www.sophiauniversity.org/en/news/synodality-course-last-workshop-module/
Kwa lugha ya kiingereza: https://www.sophiauniversity.org/en/