Tafuta

Mpango huu nchini Bolivia hautatusaidia kuendana na nyakati za kidijitali ambazo Kanisa linapitiatu,lakini pia utaimarisha utume wetu wa kutunza,kulinda na kuhifadhi urithi tajiri wa Kanisa nchini Bolivia Mpango huu nchini Bolivia hautatusaidia kuendana na nyakati za kidijitali ambazo Kanisa linapitiatu,lakini pia utaimarisha utume wetu wa kutunza,kulinda na kuhifadhi urithi tajiri wa Kanisa nchini Bolivia   (foto Giovanni Culmone GSF )

Maaskofu wa Bolivia waanzisha mchakato wa kidijitali katika majimbo!

Kwa kushirikiana na mojawapo ya programu kuu za usimamizi wa parokia(Ecclesiared,)Maaskofu nchini Bolivia waliamua kuzindua mpango wa kidigitali ili kusaidia majimbo na maparokia pia kutumia teknolojia ya digitali kama nyenzo za kazi zao na mipango ya kichungaji.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kuanzisha mchakato wa uboreshaji wa mfumo wa kidijitali na usasa katika majimbo ya nchi, hii ni moja ya kazi ambayo Askofu Eugenio Coter, na msimamizi wa  Kitume wa Pando, kaskazini mwa Bolivia, alifafananua. Kwa miju wake alisema: “Kupitishwa kwa programu maalum katika parokia zetu kunawakilisha hatua muhimu kuelekea Kanisa lenye ufanisi zaidi na lililounganishwa kwa uaminifu katika enzi ya kidijitali, hutuwezesha kuboresha michakato yetu ya utawala kuwa ya kisasa na hutupatia fursa ya kutoa huduma bora kwa jumuiya zetu nchini.”

Askofu Coter ambaye pia ni msimamizi wa kitume wa Reyes tena alisema: “Waamini wataweza kupata cheti chochote katika parokia zao, ili kuokoa muda na gharama.” Habari hii ilitolewa na Baraza la Maaskofu wa Bolivia ambao, kwa kushirikiana na mojawapo ya programu kuu za usimamizi wa parokia( Ecclesiared,) waliamua kuzindua mpango huu wa kidigitali ili kusaidia majimbo  na maparokia pia kutumia teknolojia ya digitali kama nyenzo za kazi zao na mipango ya kichungaji. “Mpango huu hautatusaidia tu kuendana na nyakati za kidijitali ambazo Kanisa linapitia, lakini pia utaimarisha utume wetu wa kutunza, kulinda na kuhifadhi urithi tajiri wa Kanisa nchini Bolivia kwa kutengeneza nakala za kidijitali za hifadhi zetu za kumbukumbu za parokia.

Maaskofu nchini Bolivia kuptia mwakilishi wake walieleza kuwa: “Tumejitolea kufikia mabadiliko ya kidijitali ambayo ni ya manufaa kwa waamini na washirika wote wa parokia zetu.” Mchakato wa uwekaji mfumo wa kidijitali utaanza katika Vikariati ya Pando na Vikariati ya Reyes, ili kupanua taratibu hadi majimbo ya Mtakatifu Ignacio de Velasco, Vikariate ya Kitume ya Ñuflo ya  Chávez, na Kanisa zima nchini Bolivia.

Mfumo wa kidigitali nchini Bolivia kusaidia waamini wa maparokia
10 June 2024, 15:25