Pizzaballa:Tunaishi usiku mrefu,tuko na kila mtu anayefanya kazi kwa ajili ya wema
ANDREA TORNIELLI
“Wakati huu ni mchungu sana, tunaishi usiku mrefu sana. Lakini pia tunajua kuwa usiku huisha. Ni wakati ambapo Kanisa lazima lifanye kazi pamoja na wale wote walio tayari kufanya jambo zuri na jema kwa kila mtu…”. Akiptia jijini Roma Kardinali Pierbattista Pizzaballa, aliviambia vyombo vya habari vya Vatican kuhusu hali ya Israeli, Gaza na Ukanda wa Magharibi.
Je, hali ikoje siku hizi, katika Israeli na hasa huko Gaza?
Hali haijabadilika sana ikilinganishwa na siku za hivi karibuni katika miezi ya hivi karibuni na kupanda na kushuka. Gaza sasa imegawanywa kati ya Kaskazini na Kusini, Rafah na mji wa Gaza. Ilikuwa ni kipindi ambacho, hasa Kaskazini, misaada zaidi ya kibinadamu ilikuwa ikiwasili. Sasa imekuwa ngumu kidogo tena. Kwa mfano tu nyama hakuna. Maji ni shida na tuseme kwa ujumla kwamba, hali inabaki kuwa mbaya sana na ni ngumu sana kuona njia za kutokea. Kwa upande wangu haionekani mazungumzo yanaongoza popote na kwamba kuna hamu ya kweli kwa wahusika kufikia hitimisho. Na hili ndilo tunaloliona, pia tukizingatia mstari wa mbele wa matarajio ya Lebanon ambao unazidi kupamba moto si hasa wa kusisimua.
Je, kuna wathiriwa wangapi? Wapo wanaojadili idadi zinazotolewa lakini picha zinazofika zinaonesha uharibifu...
Uharibifu kamili. Mji wa Gaza umeharibiwa kabisa hivyo kuna wahanga wengi. Ni vigumu kutoa idadi lakini ni wengi sana, na hii ni dhahiri. Ni ukweli kwamba wahanga wa raia siku zote ni wengi.
Tunawezaje kujenga upya muundo wa kijamii na kuishi pamoja kwa kuzingatia kile kilichotokea, lakini wakati huo huo kushinda kile kilichotokea?
Nadhani ni mapema sana kuzungumzia hili, sasa kuna vita vinavyoendelea na kiwewe. Itachukua muda kuelewa ukubwa wa kiwewe ambacho kimeathiri kila mtu na matokeo yake. Ni wazi kwamba itabidi ijengwe upya. Kuna dhamira ya kutaka kujenga upya, niliona hili kwa uwazi sana. Lakini kwa jinsi gani, kwa vigezo gani na na nani? Bado ni mapema sana kusema.
Na hali katika Ukanda wa Magharibi?
Ukanda wa Magharibi daima uko ukingoni mwa mlipuko, matatizo ni endelevu, kwa vitendo kila siku, hasa katika baadhi ya maeneo kuelekea kaskazini, katika maeneo ya Jenin na Nablus. Mapigano kati ya walowezi na wenyeji wa vijiji vya Waarabu ni ya kuendelea, hii inaleta hali ya ugomvi ambayo haitaleta chochote kizuri.
Ulitaja mapema ufunguzi wa mbele ya kaskazini. Tumeshuhudia mjadala mkali sana ndani ya Israeli kuhusu matarajio ya siku zijazo. Unaweza kutarajia nini?
Mjadala wa ndani upo Israeli na pia Lebanon: hakuna anayetaka vita lakini inaonekana hakuna anayeweza kuizuia na hili ndilo tatizo. Bila shaka, kama eneo la kaskazini lingefunguliwa, hakika hili litakuwa janga, hasa kwa Lebanon, ambayo inahatarisha kuwa Gaza nyingine, angalau katika sehemu ya kusini. Mimi si mtaalam wa masuala ya kijeshi, lakini kwa ujumbla wake inabaki kuwa ya wasiwasi, kila wakati iko kwenye hatihati ya kuongezeka zaidi.
Je, maisha ya Wakristo yakoje katika muktadha kama huu?
Wakristo si watu waliotengana, wanaishi yale ambayo kila mtu anaishi. Kwa bahati mbaya tunajua hali ya Gaza, lakini pia ni tatizo sana katika Ukingo wa Magharibi, hasa kutokana na mtazamo wa kiuchumi. Kuna hali ya kupooza, kuna kazi kidogo au hakuna kabisa na hii inafanya matarajio ya kuhama kuzidi kuvutia, kwa bahati mbaya hasa kwa Wakristo.
Tuangalie matokeo ya mwisho wa vita. Je, Jumuiya ya Kimataifa inaweza kufanya nini? Ni nani angeweza kusaidia zaidi kupata amani?
Kuwa na amani, kwa wakati huu, inaonekana kwangu kuwa lengo lililo mbali sana. Sasa siasa, Jumuiya ya kimataifa, lazima ifanye kazi zaidi ya yote kukomesha mzozo huo. Kufanya amani na kufikia matazamio mazito zaidi ya kisiasa bila shaka kutachukua muda mrefu. Jumuiya ya kimataifa lazima itafute njia ya kuhakikisha kuwa Israel na Hamas zinasimamisha mzozo huo na kufikia usitishaji mapigano unaowakilisha hatua ya kwanza kuelekea kitu thabiti zaidi, dhabiti na imara
Matokeo ya uchaguzi ujao wa Marekani pia yataathiri hali hii...
Uchaguzi wa Marekani hakika utakuwa na ushawishi. Walakini, ninaamini kuwa suluhisho lazima lipatikane ndani. Kati ya vyama viwili. Kati ya Israeli na Hamas.
Je, inawezekana kupata msaada Gaza?
Tunafanyia kazi hili, pia kwamba Upatriaki wa Kilatini umejitolea kuhakikisha misaada inafika. Hifadhi ya kwanza ya tani chache za chakula na mahitaji ya kimsingi napaswa kuwasili kesho. Kuna kazi nyingi ya kufanywa, kuna zaidi ya watu milioni mbili.
Je! Patriaki wa Kilatini wa Yerusalemu unatazamaj kile kinachotokea? Je, ni mtazamo gani wa mtu wa imani katika uso wa haya yote?
Tumaini ni binti wa imani. Wakati huu ni mchungu sana, tunaishi usiku mrefu sana. Lakini pia tunajua kuwa usiku huisha. Ni wakati ambao Kanisa lazima liwepo katika eneo, kuwa karibu, kufanya kazi na wale wote ambao wako tayari kufanya kitu kizuri na kizuri kwa kila mtu. Kila mtu anapoweka vizuizi dhidi ya mwenzake, Kanisa lazima liendelee daima kunyoosha mkono wake kuelekea lingine. Hii ndiyo kazi yetu inayotokana na uzoefu wetu wa imani, ni kile tunachoitwa kufanya wakati huu.
Je, unahisi kuwa unasindikizwa na Kanisa la Ulimwengu wote?
Ndiyo, Baba Mtakatifu daima amekuwa karibu sana nasi na anaendelea kuwa karibu sana nasi. Kama ilivyo kwa majimbo mengi sana Ulimwenguni.