Tafuta

Kila trehe 13 Juni ya kila mwaka ni siku kuu ya Mtakatifu Antoni wa Padua,Mfransiskani(OFM). Kila trehe 13 Juni ya kila mwaka ni siku kuu ya Mtakatifu Antoni wa Padua,Mfransiskani(OFM). 

Tarehe 13 Juni,Mama Kanisa anaadhimisha Siku kuu ya Mtakatifu Antoni wa Padua

Katika fursa ya Siku Kuu ya Mtakatifu wa Padua,kuna usiku wa mkesha tarehe 12 Juni,huko Arcella,ambao kiutamaduni ni ushiriki mkubwa wa waamini kutoka mahalia na mahujaji katika kukumbuka siku ya kifo cha Mtakatifu wa Antoni.Utamaduni huu ulianza tangu mwaka 1276.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Uwakilishi wa Mtakatifu Antoni wa Padua  katika  Madhabahu ya Arcella, mji wa kaskazini mwa Padua, umekuwa sherehe kubwa watu wa Padua ya wote kwa karibu karne nane. Kwa hakika, ilikuwa mwaka 1276 ambapo Manispaa ya Padova ilianzisha kwa sheria kwamba kwa kuanza tamasha la heshima kwa  Mtakatifu ilipaswa kufanyika baada ya saa 3  katika mkesha wa siku ya siku kuu, kwa hiyo  tarehe  12 Juni 2024.

Mapokeo ya mkesha wa Mtakatifu Antoni

Mwaka huu 2024 pia, mapokeo ya kale yatafuatwa na usiku wa Jumatano tarehe 12 Juni 2024  kuanzia saa 2:45 usiku,  a maandamano yatafanyika kutoka Camposampiero hadi Padua ambapo Mtakatifu Antoni akihisi kuwa karibu na kifo, aliomba kupelekwa kwenye nyumba pendwa ya Padova ya Maria Mater Domini, kitovu cha kwanza cha kile ambacho baadaye kilikuja kuwa Basilika ya Mtakatifu Antoni.

Karibu miaka 800 gari la ng'ombe lilibeba mwili wa Antoni

Mwaka 2024 kutokana na kazi inayoendelea kwenye uwanja wa Azzurri ya Italia, mahali pa kuanzia pamesogezwa kuwa karibu na Kanisa la  Mtakatifu  Carlo, huku njia ya maandamano haitabadilika. Mapadre, Watawa wa kike na kiume, vyama vya watu waliovalia mavazi, wakisindikizwa na taasisi za jiji na baadhi ya manispaa ambao walivuka, karibu miaka 800 iliyopita, na gari la ng'ombe na Mfransiskani aliyekuwa amekufa vivyo hivyo wataandamana kwenye mitaa ya jirani ili kukumbuka Kuwasili na kifo cha Antonio huko Arcella, kama ilivyosimuliwa na Assidua, wasifu wa kwanza ulioandikwa miaka michache baada ya kifo cha Mfransiskani, labda na shahidi aliyejionea, kati ya Luca Belludi, kaka yake mwaminifu.

Waamini na mahujaji

Kama ilivyo katika utamaduni wa kale, maelfu ya waamini watashiriki ili kutoa heshimia kwa sanamu ya Mtakatifu aliyekufa. Hii ni ibada maarufu  uliyojaa ishara  za ubinadamu wa dhati. Hii pia ni sehemu ambayo wanafanya kuhiji upya kihistoria, kwa kuimba, hata kugusa. Kwa hakika, ni wanahija ambao wanawakilisha umati wa watu ambao humiminika kwenye Kanisa la Arcella jioni hiyo tangu mnamo 1231 wakiongozwa na kilio cha watoto waliokuwa wakilia: “Baba Mtakatifu amekufa, Mtakatifu Antoni amekufa!”

Madhabahu ya Arcella

Kwa kawaida aidha kuwa uigizaji upya wa kihistoria na kiroho katika mavazi unaokamilika kwa kuwasili kwa gari kwenye patakatifu la Arcella na kwa tamasha la jadi la kengele za jiji zima saa 3.30 alasiri, kwa ushirikiano na parokia za jiji na Majimbo ya Padova. Tamasha la sherehe la kengele za Madhabahu ya Arcella linatangaza kwa jiji na kwa ulimwengu kuzaliwa kwa Antoni huko Mbinguni na kuibua historia za kengele za Lisbon, mahali alipozaliwa Mtakatifu Antoni ambapo inasemekana kuwa ililia kwa  hiari wakati huo huo akiwa anakufa huko Padua.

12 June 2024, 14:16