Tafuta

2024.07.02 Askofu Giorgio Biguzzi, Mmisionari wa Xaveri, Askofu Mstaafu wa Makeni nchini Sierra Leone ameafariki Jukau Mosi. 2024.07.02 Askofu Giorgio Biguzzi, Mmisionari wa Xaveri, Askofu Mstaafu wa Makeni nchini Sierra Leone ameafariki Jukau Mosi.  (© Missionari saveriani)

Askofu Biguzzi alikuwa shuhuda wa kweli wa Injili nchini Sierra Leone

Mmisionari wa Xaverian,Askofu wa jimbo la Makeni,nchini Sierra Leone,kuanzia 1987 hadi 2012,alifanya kazi kwa ajili ya kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe na ukarabati wa askari watoto na kukemea ufisadi na biashara haramu ya almasi kwa uuzaji wa silaha.Padre Giulio Albanese:aliamini katika mazungumzo ya amani.

Vatican News

Askofu Giorgio Biguzzi, mmisionari wa Wamisionari wa Xaveri na Askofu mstaafu wa Makeni nchini Sierra Leone, alifariki dunia tarehe 1 Julai 2024 mjini Parma nchini Italia, akiwa na umri wa miaka 88. Mtawa huyo alikuwa amelazwa hospitalini baada ya miezi miwili kukaa katika nyumba mama ya Shirika katika jiji hilo hilo Mkoa wa  Emilia Romagna. Padre Giulio Albanese, Mkomboniani, mwandishi wa habari, mwanzilishi wa shirika la habari la Misna, mshiriki wa magazeti mengi na leo hii pia mkurugenzi wa Ofisi ya Mawasiliano ya Kijamii - Jimbo la Roma, alimfahamu vyema na ambaye akizungumza na Radio Vatican - Vatican News kuhusu urafiki mzuri ulioanzishwa na yeye alisema alikuwa na dhamira yake iliyoamua katika kupendelea haki nchini Sierra Leone, katika miaka ya vita vya almasi. Padre Albanese alimfafanua, kuwa alikuwa mchungaji asiye wa kawaidia  akiwa makini kwa mdogo na pamoja na vijana, “shahidi wa kweli wa Injili” ambaye alitekeleza kwa vitendo kile ambacho Papa Francisko anashauri kila mara: kuwa upande wa maskini.

Askofu Mstaafu wa Makeni Nchini Sierra Leone ameaga dunia
Askofu Mstaafu wa Makeni Nchini Sierra Leone ameaga dunia

Huduma katika Kanisa

Askofu Giorgio Biguzzi ni mzaliwa wa Calisese, katika jimbo la Cesena, Italia, tarehe 4 Februari 1936, na alijiunga na Seminari Ndogo mwaka 1947 na kuendelea na masomo yake katika Seminari ya Mkoa wa Bologna, akiacha miaka kumi baadaye kuingia Upadre wa Shirila la Wa Xaveri. Aliwekwa Daraja la Upade mnamo mwaka wa 1960, baada ya miezi michache kukaa katika jumuiya ya Xaveri ya Udine na miezi miwili na familia yake, alitumwa kwa Circumscription ya Marekani, ambako alikaa hadi 1973 akishughulikia majukumu mbalimbali. Alikuwa ametumwa Sierra Leone mnamo mwaka wa 1974 na miaka kumi baadaye aliitwa tena Italia.

Padre Giorgio Biguzzi Askofu mstaafu wa Makeni , Sierra leoni ameaga dunia
Padre Giorgio Biguzzi Askofu mstaafu wa Makeni , Sierra leoni ameaga dunia

Mnamo Mwaka 1987 alichaguliwa kuwa askofu wa Makeni. Aliwekwa wakfu tarehe 6 Januari na Mtakatifu Papa Yohane Paulo II katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Roma,  na alitekeleza huduma yake ya uaskofu hadi mnamo mwaka 2012. Baada ya kurejea Italia alijishughulisha na huduma mbalimbali na hivi karibuni  zaidi, kutokana na hali yake ya kiafya iliyozidi kuwa hatarini, alihamishiwa kwenye makao ya wazee ya Fraternità San Lorenzo huko Mtakatifu  Pietro huko Vincoli. Tarehe 29 Aprili 2024, kulingana na ombi lake, alipelekwa Nyumba mama kisha kulazwa hospitalini.

Upendo kwa Sierra Leone

Askofu Biguzzi alipenda sana Makeni na watu wake na aliporejea Italia alishirikisha watu na vikundi kutafuta msaada wa kila aina. “Bwana, anayechagua vitu vidogo na visivyofaa kwa ajili ya mipango yake, aliniita niwe Shahidi wa Kristo Mfufuka katika Kanisa la Makeni. Ni kazi ambayo kabla yake ninahisi kupotea na ambayo, hata hivyo, naiona kama wito wa huduma ya ukarimu zaidi na upendo mkubwa zaidi kwa Kristo na kwa ndugu zetu,” aliandika katika barua kwa Mkuu wa Shirika  mara tu alipoteuliwa kuwa askofu. Katika Utume huko Sierra Leone, ambapo Wanashirika wa  Xaveriani wameunda makanisa na shule, pia wanafanya kazi katika huduma ya afya, Askofu Biguzzi, aliye kuwa na akili sana na mfuatiliaji makini wa michakato ya kiutamaduni inayofanyika ulimwenguni, alihimiza kuzaliwa kwa Chuo Kikuu cha Kikatoliki na alifanya kila awezalo, hasa, katika upatanishi wa migogoro na ukarabati wa askari watoto ambao aliwaleta kwenye uwanja wa Mtakatifu Petro mnamo  2000. Alizungumza na kuandika juu ya utisho wa vita vya almasi na ufisadi na pia alikuwa mtu wa uhusiano na Wakristo wa Makanisa na imani zingine.

Kujitolea kwa amani

Akiwa mjumbe wa Baraza la Kidini la Sierra Leone, alifuata mazungumzo ya makubaliano ya amani kati ya Rais Ahmed Tejan Kabbah na kiongozi wa RUF (Revolutionary United Front) Fodai Sankoh, na kwa hili mwaka 1999 alitunukiwa Tuzo ya Moyo wa Kirafiki. Kutokana na mamlaka yake pia alichukua nafasi kubwa katika ukombozi wa Wamisionari wa Maria waliotekwa nyara na waasi mwaka 1995; yeye mwenyewe alishambuliwa na kuwekwa kizuizini kwa siku chache. Mwaka 2023, akiwa tayari kwenye kiti cha magurudumu, alitaka kurudi Makeni ili kushiriki katika kumweka wakfu Bob John Hassan Koroma, Askofu wa kwanza wa Sierra Leone baada ya miaka sitini ya Mapadre  wa kawaida wa Shirika la  Xaverian. Kuanzia miaka yake huko Sierra Leone, Padre Albanese anakumbuka, hasa, mkutano na waasi wa RUF na anaelezea juu ya wavulana wawili waliochukuliwa kutoka kwa waasi na kukomboa shukrani kwa msaada wa Askofu Biguzzi na wanshirika wake  WaXaverian.

03 July 2024, 17:48