Tafuta

Ziara ya Kipapa katika Ufalme wa Bahrain na misa katika Uwanja wa Kitaifa Bahrain 2022 Ziara ya Kipapa katika Ufalme wa Bahrain na misa katika Uwanja wa Kitaifa Bahrain 2022  (Vatican Media)

Bahrain:zaidi watoto na vijana elfu walishiriki tukio la ‘Uamsho 2024'

Jumuiya nzima ya Parokia ya Moyo Mtakatifu ihuko Bahran imejitolea kusaidia ukuaji wa kiroho na maendeleo ya vijana na inashukuru kwa ushirikiano na AFCYM wanapotarajia kuendelea kuandaa matukio ambayo yanakuza imani ya watoto na vijana wao.Ni katika siku nne za kushirikishwa,furaha,sala,muziki na shangwe kwa washiriki wa mafungo ya kiroho kwa watoto na barubaru 1,155 lililoongozwa na kauli mbiu:"amka 2024" huko nchini Bahrain.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kulikuwa na siku nne za kushiriki, furaha, sala, muziki na furaha kwa washiriki 1155 katika mafungo ya “Uamsho 2024.” Hili ni tukio lililoandaliwa na  Vicariate ya Kaskazini mwa Falme ya Arabia ambapo watoto na vijana kutoka parokia ya Manama ya Moyo Mtakatifu  na Kanisa Kuu la Mama Yetu wa Arabia huko Awali walishiriki mafungo ambapo washiriki waliweza kushirikisha imani na udugu, wakiongozwa na harakati ya Upako wa Moto wa Huduma ya vijana (AFCYM) wa Marekani, kati ya shughuli mbalimbali za kusisimua zilizoundwa kuendana na makundi tofauti ya umri. Wakiwa ndani ya Kanisa la  Moyo Mtakatifu, lengo la Uamsho 2024 lilikuwa  ni “kuandaa mazingira ya elimu ambapo watoto na vijana wangeweza kuchunguza imani yao katika maisha ya kila siku, kuungana na wenzao, kuimarisha uhusiano wao na mambo ya kiroho, na kuunda kumbukumbu za kudumu,” kama ilivyoelezwa kutoka vyanzo vya Vicariate na Askofu Aldo Berardi, O.SS.T.

Wakati wa Misa Takatifu huko Bahrain Papa akiwa kwenye ziara yake 2022
Wakati wa Misa Takatifu huko Bahrain Papa akiwa kwenye ziara yake 2022

“Programu za shughuli zilizoundwa kushirikisha akili na mioyo ya vijana ziliundwa wakati wa mafungo. Kivutio kilikuwa vikao vya nguvu vilivyoongozwa na viongozi wa vijana. Jumuiya nzima ya Parokia ya Moyo Mtakatifu imejitolea kusaidia ukuaji wa kiroho na maendeleo ya vijana wetu na inashukuru kwa ushirikiano na AFCYM tunapotarajia kuendelea kuandaa matukio ambayo yanakuza imani ya watoto na vijana wetu.” Alibanisha Kiongozi wa Kanisa huko Vicarieti ya Uarabuni.

Misa katika Uwanja wa Kitaifa wa Bahrain 2022
Misa katika Uwanja wa Kitaifa wa Bahrain 2022

Ikumbukwe Papa Francisko alitimiza ziara ya kitume katika nchi ya Ufalme wa Bahrain kuanzia tarehe 3 hadi 6 Novemba 2022 kwa kutembelea mji wa Manama na Awali katika fursa ya Jukwaa la Bahrain kwa ajili ya Mazungumzo: Mashariki na Magharibu kwa ajili ya ubinadamu wa kudumu. Papa  Francisko ndiye alikuwa Papa wa kwanza kwenda katika Ufalme wa Bahrain ambapo Vatican ilianza uhusiano wa kidiplomasia mnamo mwaka 2000, ulioalikwa na mamlaka ya kiraia na kikanisa.  Kwa hiyo ziara hiyo ilithibitisha jitihada za chaguzi ya familia ya kifalme ya Al Khalifa, nia ya kukubali msimamo wa Ufalme kuwa mahali pa mazungumzo, ukarimu wa uvumilivu na kuishi kwa amani kati ya tambulisho nyingi na jumuiya ya imani, katika ulimwengu ambao daima umezugwa na migogoro ya miibuko ya kidini na mabishano ya ustaarabu.

Wakati wa Misa Takatifu huko Bahrain 2022
Wakati wa Misa Takatifu huko Bahrain 2022

Historia ya ufalme wa Bahrain

Historia ya Bahrain inahusu eneo ambalo leo linaunda hakika ufalme wa Bahrain. Na Bahrain ndiyo makao ya ustaarabu wa Dilmun. Nchi hiyo ilipata umaarufu tangu zamani kwa kuvua lulu bora kuliko zote duniani hadi karne ya 19. Ufalme wa Bahrain ulikuwa kati ya maeneo ya kwanza kuongokea Uislamu mnamo mwaka 628 Bk. Baada ya kipindi cha utawala wa Waarabu, Bahrain ilitekwa na Wareno  mnamo mwaka 1521 hadi 1602 walipofukuzwa na Shah Abbas I chini ya Dola la Uajemi. Mnamo mwaka 1783, ukoo wa Bani Utbah uliteka Bahrain kutoka kwa Nasr Al-Madhkur na tangu hapo nchi ilitaawaliwa na ukoo wa Al Khalifa, Ahmed al Fateh akiwa hakimu wa kwanza wa Bahrain.

Misa huko Bahrain
Misa huko Bahrain

Tangu mwaka 1820 Visiwa hivyo pamoja na Qatar na Falme za Kiarabu vilikuwa na mikataba na Uingereza walipoahidi kuachana na uharamia na kupokea ulinzi wa Uingereza. Ulinzi huo ulizuia uvamizi wa Saudia katika karne ya 20. Falme hizo zilikuwa chini ya usimamizi wa   Uingereza hadi mwaka 1971, ambapo madola hayo madogo yalipata uhuru.

Wakati wa mkutano huko Baharain
Wakati wa mkutano huko Baharain
11 July 2024, 16:53