Tafuta

2024.05.14:Askofu Djitangar akitoa Sakramenti ya Kipaimara kwa vijana na watu wazima nchini Chad. 2024.05.14:Askofu Djitangar akitoa Sakramenti ya Kipaimara kwa vijana na watu wazima nchini Chad. 

Chad,Tafakari kwa vijana katika muktadha wa mivutano ya nchi!

Nafasi ya kutafakari,kubadilishana mawazo na uzoefu unaolenga ulimwengu wa vijana katika muktadha wa mivutano lilikuwa ni mojawapo ya mipango muhimu zaidi ya Uhuishaji wa Kimisionari,kwa ushirikiano wa karibu na sekta ya Haki,Amani na Uadilifu wa Uumbaji(JPIC)ya Wamisionari wa Comboni nchini Chad.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

“Sayari ya Dunia, urithi wa pamoja ni Jukwaa linalolenga vijana wa nchini Chad ambalo litafanyika katika Kituo cha vijana huko Abéché kuanzia tarehe 2 hadi 6 Septemba 2024. Jukwaa hilo limeandaliwa na wamisionari wa Comboni likiwa ni  toleo la Tatu ambalo litaongozwa na chaguo wazi kutaka kutoa nafasi ya kutafakari, kubadilishana mawazo na uzoefu unaolenga ulimwengu wa vijana.” Kama ilivyokuwa katika matoleo yaliyotangulia, waandaaji wanabainisha kuwa hili pia litatiwa moyo na kuongozwa na Waraka wa Laudato Sì wa Papa Francisko ili kuhamasisha ulinzi wa nyumba ya wote kwa kuzingatia hali za kutengwa unaojionesha nchini Chad. Washiriki wa tukio hilo wanatoka katika jumuiya za wenyeji, ambapo mwamko mkubwa umewahamasisha vijana na wazee, Wakristo na Waislamu wa Chad kwa mtazamo wa kujitolea upya kwa manufaa ya nchi nzima.

Mpango unakwenda zaidi ya vikwazo

Wahamasishaji aidha wana nia ya Mpango ambao unakwenda zaidi ya vikwazo vya kidini, na zaidi ya hayo, nchi inaendelea kukumbwa na mvutano na baada ya uchaguzi wa rais wa hivi karibuni, inatafuta uwiano kati ya mahitaji tofauti, awamu mpya ya mwendelezo. Kama ilivyo katika Sahel nzima, leo hii Chad pia inakabiliwa na mabadiliko ya kihistoria na pengine italazimika kurekebisha baadhi ya sera zake. Mwezi Mei Baraza la Katiba la Chad lilithibitisha matokeo ambayo yalimwona Mahamat Idriss Déby Itno kama mshindi, kama ilivyotarajiwa.

Migawanyiko ya ndani ya kikabila

Migawanyiko ya ndani ya kikabila pia lazima izingatiwe, ikithibitishwa na tofauti za kikanda katika mgawanyo wa kura, hasa katika nchi kama Chad, iliyoadhimishwa na miongo kadhaa ya vita kati ya kaskazini na kusini na yenye watu wachache muhimu wanaohusishwa na shughuli za makundi yenye silaha nchini Libya, Sudan na Afrika ya Kati. Tangu Aprili 2021 akiwa mkuu wa Baraza la Kijeshi la Mpito ambalo linaongoza nchi kufuatia kifo cha baba yake, mtangulizi wake, Idriss Déby Itno, ambaye aliuawa wakati akishiriki katika hatua ya askari wake dhidi ya harakati ya waasi wenye silaha, Mahamat Idriss Déby. Itno alitangazwa mshindi kwa 61%, akifuatiwa na waziri mkuu wa serikali ya mpito na mpinzani mkuu Succès Masra kwa 18.5% na waziri mkuu mwingine wa zamani karibu na ukoo wa Déby, Albert Pahimi Padacké, kwa 16.9%.

 

24 July 2024, 14:14