Tafuta

Mojawapo la Kanisa katoliki nchini Indonesia Mojawapo la Kanisa katoliki nchini Indonesia  (AFP or licensors)

Indonesia,Askofu Mkuu wa Kupang:Waamini kukutana na Papa ni fursa ya maridhiano!

Papa kukutana na waamini wa Indonesia watakao kwenda Timot Est itakuwa fursa ya maridhiano.Amesema hayo Askofu Mkuu Hironimus Pakaenoni wa Jimbo Kuu Katoliki la Kupang,tangu Machi 2024,katika fursa ya maandalizi ya kumpokea Baba Mtakatifu katika Ziara ya Kitume Nchini humu kuanzia tarehe 3 hadi 6 Septemba 2024,ikiwa ni kituo cha kwanza kati ya vituo vinne vya nchi tofauti.Indonesia ina visiwa elfu 17.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika Mlangoni mwa nyumba ya Hironimus Pakaenoni, Askofu Mkuu wa Metropolitan wa Kupang, tangu Machi 2024, mapadre, wamisionari na waamini wa Mungu wanaotaka kushiriki furaha au mateso hufika wakibisha hodi na kuingia bila utaratibu wowote. Kwa hiyo lango la makazi yake, nyumba ya ghorofa moja katikati ya jiji la Kupang, huwa wazi kila wakati, hata usiku. Padre Raymond Maurus Ngatu mwenye umri wa miaka 31 kutoka katika Shirika la  Wamisionari wa Mitume watakatifu alikwenda huko kuomba baraka katika mkesha wa adhimisho la misa yake ya kwanza katika Parokia ya Kupang, mji aliozaliwa, kisha ataondoka tena kwa ajili ya utume huko Pontianak, Indonesia Borneo. Askofu Mkuu alitoa tabasamu na ushauri, alitoa baraka, zaidi ya yote alisema neno na siri kwa ajili ya kazi hiyo ya kimisionari kwamba: “Daima ni kuwa na tumaini kwa Mungu, si ndani yetu wenyewe. Kuwa vyombo mikononi mwake.”

Kupang ni kitu cha mijijini 

Kupang ni kituo kikuu cha mijini kwenye sehemu ya magharibi ya kisiwa cha Timor (sehemu ya Indonesia, nusu nyingine ni jimbo huru la Timor ya Mashariki,), na ni mji mkuu wa jimbo la Indonesia la Nusa Tenggara Mashariki. Pamoja na wakazi zaidi ya elfu 430, ni mji wa bandari wa Asia wa kawaida, badala ya machafuko, mchanganyiko wa watu wenye shughuli nyingi kila wakati, mahali pa kupita, kati ya wafanyabiashara na wavuvi wanaoshughulikia msululu wa  bidhaa inayoelekezwa kwenye visiwa vingine vingi vya mashariki mwa Indonesia. Na Jimbo la Kupang (lenye jumla ya watu milioni 1.6 katika eneo lake lote) ni mojawapo ya majimbo machache ambayo nchini Indonesia taifa lenye visiwa elfu 17, ambalo ni nchi yenye Waislamu wengi zaidi duniani, inajumuisha idadi ya Wakristo wengi pia.  Wakazi wa eneo hilo ni asilimia 60% Wakristo wa Kiprotestanti, karibu 35% Wakatoliki na 3-4% tu ya Waislam. Askofu mkuu “Roni” kama  apendavyo kuitwa na mapadre na waamini anafuraha kuwa hivi karibuni amewapa daraja Takatifu la Upadre kwa vijana 14 ambao “Mungu akipenda watakuwa wengine mapadre hivi karibuni 12 kati yao Novemba.”  Aliliambia Shirika la habari za kimisionari Fides, akiwa katika makazi yake. Askofu akiendelea kuelezea alisema: “Na wanne kati yao tayari wanajua kuwa watakuwa 'wamisionari wa nyumbani', kama tunavyowaita mapadre waliotumwa kufanya huduma katika majimbo mengine ya Indonesia, ambapo kuna hitaji la mapadre na watawa, kama vile huko Sumatra, katika Kalimantan (Borneo ya Kiindonesia) au kwa Kiindonesia Papua,” alisema akizungumza kwa furaha juu ya mshikamano kati ya Majimbo ya Indonesia.”

Miito ya ukuhani na utawa

Parokia 35 katika eneo la Kupang (na makanisa mengine 9 ambayo yanaweza kuwa hivyo hivi karibuni), alisema Askofu Mkuu, “inarekodi utitiri na ushiriki mkubwa wa waamini katika maisha ya Kanisa na sakramenti. Imani ni hai, na sisi tunaina  juu ya yote kati ya vijana. Tunaiona kutokana na miito ya ukuhani ambayo Bwana anaendelea kutupatia: katika seminari ndogo tuna zaidi ya vijana 100, na 90 katika seminari kuu. Injili inaendelea kuvutia vijana, wakati Kanisa mahalia linasimamia zaidi ya shule 90 za Kikatoliki, kuanzia shule ya msingi hadi sekondari, pia kutokana na usaidizi wa mashrika 53 ya watawa wa kike na kiume, wanaofanya kazi katika eneo hilo. Kwa mujibu wa Askofu Mkuu alisema: “Naam, jumuiya hii, inabuni njia fupi ili kukutana na Baba Mtakatifu Francisko, ambaye atakuwa Indonesia kuanzia tarehe 3 hadi 6 Septemba 2024 na ambaye atakuwa Asia na Oceania kuanzia tarehe 2 hadi 13 Septemba 2024, iara ya Kitume na  kwamba kwa ujumla itaona mataifa manne (Indonesia, Papua New Guinea, Timor Mashariki, Singapore). “Hawatamwona sana huko Jakarta, mji mkuu, ambapo Papa atakaa kwa siku tatu  badala yake yake huko Dili, huko Timor Mashariki, upande mwingine wa mpaka. Kulingana na makadirio, karibu waamini elfu 10, kutoka majimbo ya Kupang na Atambua (mji mwingine karibu na mpaka), watahamia sehemu nyingine ya kisiwa, ili kushiriki katika misa kwenye Uwanjwa wa Tesimolu, huko Dili, alithibitisha Askofu Pakaenoni.

Umbali kutoka Timor Mashariki kwa ajili ya kuona Papa

Ni rahisi kufika Timor Mashariki, takriban saa 10 kwa basi kutoka Kupang, kuliko kuandaa safari ya gharama kubwa ya kwenda Jakarta ambako, pamoja na mambo mengine, shirika limekusanya takriban wajumbe 100 kutoka kila jimbo. Kwa hiyo, waamini wa Timor ya Magharibi wanafurahia fursa maalum: Papa Francisko atakuwa katika kisiwa kimoja nao, hata kama katika taifa dogo jirani. “Tunashirikiana na serikali ya Indonesia kusaidia wakatoliki kushiriki katika ziara ya Papa huko Dili. Tumewaomba mapadre, watawa na wamini kujiandikisha katika parokia. Na Jimbo limefanya utaratibu na ofisi ya uhamiaji kushughulikia hati za kusafiria. Waamini wengi hawana pasipoti na kibali maalum kitatayarishwa maalum kwa ajili yao, kwa ajili ya Hija tu. Na Maofisa walipandisha hadhi ya utaratibu maalum wa utoaji wa hati ya kusafiria ndani ya siku tatu, badala ya majumba mawili ya kawaida,” alifahamisha Mkuu wa Kanisa hilo. Waamini wengine pia watakuja kutoka visiwa vya karibu (Kiindonesia) vya Rote, Alor na Sabu. Kutoka Dili, mji mkuu wa Timor ya Mashariki - ambapo Papa Francisko atasimama tangu tarehe 9 hadi 11 Septemba, baada ya vituo vya Indonesia na Papua New Guinea,  uwepo wa waamini wa Indonesian pia unatarajiwa. Kuna makubaliano kamili na Baraza la Maaskofu la Timor Mashariki. Tutalazimika kutoa ukaribisho, kwa mahujaji wa Indonesia.” Alisisitiza Askofu Mkuu.

Misa ya Papa Septemba 10, nje kidogo ya mji wa Dili

Baba Mtakatifu Francisko ataadhimisha misa Septemba 10 katika eneo la Tesimolu, nje kidogo ya mji wa Dili, mahali ambapo Papa Yohane Paulo wa Pili aliadhimisha misa wakati wa ziara yake mwaka 1987, wakati Timor ya Mashariki ilipokuwa chini ya utawala wa Indonesia. Majeraha ya hapo awali yamekaribia kuponywa kabisa kwa njia ya upatanisho, kwa kuzingatia njia ambayo ni ya kisaikolojia, uponyaji wa kiwewe, na kiroho. Lakini bado kuna alama na makovu ambayo hutoka damu. Baada ya 1999, wakati Timor Mashariki ilipotangaza uhuru wake katika kura ya maoni chini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa, kulikuwa na wakati wa mvutano na mkanganyiko, uliodhihirishwa na vurugu na mauaji ya wanamgambo wanaounga mkono Indonesia. Hata katika miaka iliyofuata, msururu wa watu waliokimbia makazi yao walikimbia Timor Mashariki na kumiminika huko Atambua na Kupang, kutokana na machafuko. Wakimbizi walikuwa watu elfu 250 ambao walirudi Timor ya Mashariki polepole katika miaka iliyofuata. Katika wakati huo wa kihistoria, jumuiya ya Kikatoliki huko Kupang ikawa karibu na waliohamishwa na mipango ya mshikamano, usambazaji wa chakula na huduma za afya.

Uwepo wa Papa kufungua njia za ukaribu na upatanisho            

Kwa sasa, kulingana na Askofu Mkuu, alisema “Mungu anatoa fursa kwa tukio hilo la uchungu: Uwepo wa Papa utaweza kuidhinisha na kufungua njia ya ukaribu na upatanisho. Ziara yake sio tu kwa Wakatoliki bali kwa watu wote. Ni lazima kusema kwamba kati ya Makanisa ya Timor Magharibi na Timor ya Mashariki hakuna tatizo na sisi ni katika ushirika kamili. Baadhi ya shida na mateso bado yapo katika sehemu za idadi ya watu, katika familia ambazo zimepoteza wapendwa wao katika vurugu na bado wanaona wauaji wa upande mwingine wa mpaka. Ninaamini kwamba mtazamo wa Papa Francisko ni wa majaliwa. Inaweza kuwa wakati wa neema maalum, kairòs pia kwa upatanisho kati ya familia zilizo na alama ya misiba. Inaweza kuwa wakati wa kuomba na kukaribisha msamaha, kwa imani katika Mungu anayeponya majeraha. Ninaona kuna nia njema miongoni mwa watu na sisi Wakatoliki tunaweza kuwa wapatanishi na wawezeshaji katika mchakato huu ambao tunajua ni mgumu, kwani unahusisha mihemko na mambo ya ndani. Hii ndiyo sababu tunaomba msaada wa Mungu na kumtumaini.”

26 July 2024, 15:10