Jumuiya ya Mt.Egidio:Kuna wazee milioni 9 wanakabiliwa upweke na joto
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kuna uzoefu mzuri na wa ubunifu uliopendekezwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio wa kuishi pamoja kati ya watu wazee wajane au walio peke yao ambao wanaamua kuishi pamoja na kugawana gharama za pango. Rais wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, Bwana Marco Impagliazzo, alisema hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari tarehe 12 Julai 2024 akiwasilisha mpango wa ufuatiliaji wa watu zaidi ya miaka 80. “Tumehimiza ufuatiliaji wa kitaifa wa watu 2,500 wenye umri wa zaidi ya miaka themanini na kugundua kuwa 80%, hawaendi likizo, na wanakabiliwa na matokeo ya joto na upweke katika miji ambayo inasalia karibu tupu. Na kwa wazee waishio kwa muda mrefu, huku Roma tumejenga nyumba 165, ambapo wazee 1100 wanaishi uzoefu huu wa kushiriki miaka yao ya mwisho wa maisha. Suluhisho hili lina mafanikio makubwa na pia linaonesha ukomavu mkubwa wa idadi ya wazee. Tunatoa wito kwa serikali kuhimiza utekelezaji wa haraka wa Sheria ya 33, iliyoidhinishwa kwa misingi ya majaribio tu katika maeneo mawili ya Italia, ambayo hutoa mabadiliko ya utunzaji na uangalizi wa nyumbani,” alieleza Bwana Impagliazo.
“Pia niruhusu tafakari ndogo juu ya uhusiano kati ya wazee na wanyama wapendwa. Miaka miwili iliyopita tuliwasiliana na Lav (Ligi ya Anti Vivisection), ambayo ilitaka kushirikiana na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio kusaidia watu wazee ambao wana wanyama wao wapendwa na mara nyingi kampuni yao pekee, husaidia uwepo wao nyumbani kwa ajili ya kutunza gharama za chakula, huduma ya mifugo au kutafuta nyumba kwa ajili ya mnyama ili kuruhusu mtu mzee kupata matibabu.” Alisemaa. “Hii ni mifano ya uzoefu mdogo lakini muhimu kwa lengo la kuchochea mabadiliko kuelekea utunzaji wa nyumbani, ambayo sio tu unaruhusu akiba kwa Serikali na kwa familia, lakini pia unaruhusu wazee kupewa maisha ya furaha zaidi, yenye heshima zaidi, pamoja na uwezo mkubwa zaidi kwa ujasiri,” alisisitiza mkuu huyo wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio.
Zaidi ya wazee elfu 18 wa zaidi ya miaka 80 wanasimamiwa na mtandao
Muktadha huu unajumuisha mradi wa ufuatiliaji wa zaidi ya watu 80 ambao ni Wazee waishio kwa muda mrefu unaohamasishwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio kwa usaidizi wa Enel Cuore onlus yaani chama kisiocho cha kiserikali na Wizara ya Kazi na Sera za Kijamii nchini Italia. “Mradi huo ulianza kutumika tangu 2004 na kujumuishwa na Umoja wa Mataifa kati ya Hatua Chanya katika neema ya wazee kwa kuzeeka hai, mradi unahusisha miji 11 ya Italia, kwa jumla ya wazee zaidi ya elfu 18 zaidi ya miaka themanini, wapo katika mtandao wa ulinzi”. Na “kupitia mradi huu tumepata matokeo muhimu kwa kuthibiti vifo, kulazwa hospitalini na kuanzishwa kwa taasisi, ambayo inaweza kuzuia na kuleta huduma za nyumbani na kuendelee kwa wazee kuishi katika nyumba yao mwenyewe.” Alieleza.
Familia zisaidiwe kifedha na serikali
“Matumizi ambayo familia za Italia hutumia kwa ajili ya watunzaji wa wazee ni sawa na euro bilioni 8 kwa mwaka ambazo, kulingana na makadirio yetu, huchangia kupunguza matumizi ya umma yanayoungwa mkono na serikali kwa mipango inayolenga wazee kwa bilioni 13 kwa mwaka.” Kwa kusisitiza zaidi Bwana Impagliazzo aliomba kuwa: “familia zinaweza kusaidiwa kifedha na serikali kupunguza gharama hizi: makadirio ya 2025 yanaonesha kuwa katika nchi yetu kutakuwa na hitaji la wafanyakazi wa nyumbani milioni 1.2 na walezi milioni 1. Pia tunaomba kuongezwa kwa makato ya (Kodi ya mapato ya kibinafsi-Irpef )kwa familia zinazosaidia gharama za mlezi na posho ya jumla ya kutojitosheleza,” alihitimisha.