2024.03.14 Ospedale di Ngaoundal. Congregazione delle Suore della Carità di Santa Giovanna Antida. Galagala, Ngaoundal, Camerun

Kasese,Uganda:Watawa katika huduma za afya vijijini

Msaada na ufahamu juu ya huduma ya afya,watawa wamekuwa wakihudumia katika maeneo ya vijijini nchini Uganda.Ni kambi ya bure ya afya inayohamasishwa na Hospitali ya Mtakatifu Maria,Jimbo Katoliki la Kasese kwa ushirikiano na Chama cha Watawa wa Uganda(URU),katika muktadha wa mtandao wa kiafya unaoongozwa na mratibu wa kitaifa Sr.Maria Goretti Kabakaali wa Shirika la Mabinti wa Mtakatifu Teresa wa Mtoto Yesu(Banya-Theresa Sisters)huko Fort Portal.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kutokana na umaskini na matokeo yake kushindwa kulipia huduma za matibabu, katika maeneo ya vijijini nchini, Uganda upatikanaji wa vituo vya afya na madaktari ni mdogo sana na wenyeji huishia kufa kwa magonjwa yanayotibika kwa urahisi. Kwa hiyo wazo la kufungua  Ni kambi ya afya bure iyohamasishwa na Hospitali ya Mtakatifu Maria  Jimbo Katoliki la Kasese kwa ushirikiano na Chama cha Watawa wa Uganda (URU),katika muktadha wa mtandao wa kiafya unaoongozwa na mratibu wa kitaifa Sr Maria Goretti Kabakaali wa Shirika la  Mabinti wa Mtakatifu Teresa wa Mtoto Yesu(Banya-Theresa Sisters) wa Fort Portal. Gharama ya usafiri na matibabu - kulingana na kile ambacho mratibu aliripoti - inaweza kuwa ya juu na inajumuisha kipengele cha kukataa zaidi kutafuta matibabu. Zaidi ya hayo, ukosefu wa ufahamu na elimu ya afya inaweza kuzidisha tatizo hilo, na kusababisha matukio makubwa ya magonjwa na hali zinazoweza kuzuilika.”

Utambuzi wa changamoto za nje katika nyanja ya afya

Kama sehemu ya mtandao wa kiafya, watawa hawa nchini Uganda wanaojishughulisha na sekta tofauti za afya wanatambua changamoto zinazohusiana na afya katika jumuiya mbalimbali wanazohudumia kwa lengo la kutafuta njia za kuwafikia na, inapowezekana, kuwasaidia kuondokana na changamoto hizi.  Wazo la kambi za afya limeonekana kuwa na ufanisi katika kukuza huduma za matibabu katika maeneo ya vijijini na kujenga ufahamu kuhusu huduma za afya. Mbali na mtandao wa afya, ARU inasimamia pia  mitandao mbalimbali, ukiwemo ule wa kupinga biashara haramu ya binadamu, unaoongozwa na Shirika la Masista wa Msalaba Mtakatifu.

Shirika lenye haki kijimbo

Shirika la Masista wa Banya-Theresa linaundwa na watawa waliowekwa wakfu lenye haki Kijimbo ambalo lilianzishwa katika Jimbo la Fort Portal. Msimamizi wao ni Mtakatifu Teresa wa Mtoto Yesu, Mwalimu na msimamisi wa Wamisionari pamoja na Mtakatifu Francis Xavier, ambaye watawa wanaendeleza ibada ya pekee kwake kufuatia imani, upendo, uaminifu, unyenyekevu na moyo wa kujitolea. Kwa sasa wapo Rwanda, Kenya, Uganda na Sudan.

11 July 2024, 18:03