Tafuta

Ostia Takatifu Ostia Takatifu 

Marekani,Kongamano la X la Ekaristi:Uzoefu wa Kikatoliki tofauti na Mwingine Wowote!

"Mungu anasikia maombi yetu kwa ajili ya kufanywa upya kwa Kanisa letu.Atawajibu kupitia mabadiliko ya maisha ya mioyo yetu wenyewe."Ni mwaliko wa kushiriki Kongamano la 10 la Ekaristi Kitaifa nchini Marekani."Ni mwaliko wa kupata uamsho wa kina wa kibinafsi ili tuweze kutumwa kushiriki upendo wa Kristo na ulimwengu unaouhitaji sana.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Bwana Yesu aliwaambia, mitume wake kuwa “Mimi ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe,"(Yh 6,35). Kuanzia Jumatano tarehe 17 hadi 21 Julai 2024 litafanyika Kongamano la X la Ekaristi Takatifu Kitaifa, katika Uwanja wa Mpira wa Lucas Oil, huko Indiana Polis, nchini Marekani, litakaloudhuriwa na Mapadre, watawa wa kike na kiume na waamini Walei watu wa Mungu. Hili ni Kongamano Kitaifa ambapo wanatoa “mwaliko wa kupata uamsho wa kina, kibinafsi ili wote waweze kutumwa kushiriki upendo wa Kristo na ulimwengu unaouhitaji sana.” Katika muktadha huo aidha wanawaalika wakisema: “Njoo kwa imani na uondoke kwa matumaini”  na  wote wanakaribishwa kushiriki. Katika hilo wanasisistiza kuwa:“Mungu anasikia maombi yetu kwa ajili ya kufanywa upya kwa Kanisa letu. Atawajibu kupitia mabadiliko ya maisha ya mioyo yetu wenyewe.”

Kongamano la X la Ekaristi Takatifu Kitaifa nchini Marekani kuanzia 17-21 Julai 2024

Familia itakusanyika kupata uzoefu mpya wa kina

“Katika Kongamano la X la Ekaristi Kitaifa, familia yetu ya Kikatoliki itakusanyika ili kupata uzoefu wa upya wa kina, wa kibinafsi kupitia nguvu ya upendo wa Kristo. Kama Pentekoste mpya, mageuzi haya yatatoka Indianapolis kupata uamsho katika jumuiya zetu wakati Kanisa linaporudi kwenye upendo wake wa kwanza wa chimbuko na kilele cha imani yetu.”

Kila siku kwa siku tano zitakuwa na jambo jipya

Kila siku kwenye Kongamano aidha wanasisitiza kuwa “ imeundwa ili kuwezesha kukutana na Yesu kwa maisha haya ya kubadilisha maisha, bila kujali mahali ulipo kwenye safari yako ya imani. Watakaohudhuria watachagua mfululizo wa vipindi wanavyopendelea vya vipindi vya vipindi vizuri virefu vya asubuhi na vipindi vifupi vya alasiri. Kisha, wakikusanyika pamoja kama kitu kimoja, kusanyiko zima litapata vipindi vya uamsho vyenye nguvu katika Uwanja wa Lucas Oil kila jioni. Ikiwa unaweza kuja kwa siku moja au zote tano, jiunge nasi kwa wakati huu.” Ukitaka kujiandikisha bonyeza hapa: https://www.eucharisticcongress.org/register.

16 July 2024, 15:51