Tafuta

2024.06.17 Kroatia 2024.06.17 Kroatia  (Riječka nadbiskupija)

Mikutano ya Kitaalimungu ya Rijeka,Sr.Becquart:Majadiliano ya Kanisa la Sinodi na kila mtu!

Katika toleo la tatu la Mikutano ya Kitaalimungu ya Mediterania na mada:“Ukristo na Uislamu:katika huduma ya udugu katika ulimwengu uliogawanyika,iliyoandaliwa na Jimbo kuu,ilihitimishwa 19 Julai 2024,huko Kroatia.Katibu Msaidizi wa Sinodi ya Maaskofu:Kanisa lazima lisiogope tofauti,sababu liko tayari linabeba ndani yake na halilazimishi usawa.

Alessandro Di Bussolo  na Angella Rwezaula – Vatican.

Kanisa la Sinodi linaitwa kufuata utamaduni wa kukutana na mazungumzo na waumini wa dini nyingine na mchakato wa Sinodi ya kisinodi, ambayo kuanzia kusanyiko la kwanza la mwaka 2023 itaongoza tena mkutano wa pili mnamo mwezi Oktoba 2024 ambapo itakuwa fursa ya kujifunza maana ya kupata umoja katika utofauti. Haya yalilisisitizwa na Sr. Nathalie Becquart, katibu Msaidizi wa Sinodi ya Maaskofu, katika hotuba yake kwenye toleo la Tatu la Mikutano ya Kitaalimungu ya Mediterania huko Rijeka, lililohitimishwa tarehe 19 Julai 2024 katika nyumba ya kichungaji ya Laurana, huko Lovran, kwenye pwani ya Adriatiki ya Kroatia.

Fundisho la “Sinodi, Uekumene na mazungumzo ya kidini”

Katika fundisho lake la mkutano wake Jumatano tarehe 17 Julai 2024 mbele ya wanafunzi 38 na wanafunzi wa udaktari katika Taalimungu ambao walikuwa wahusika wakuu wa Mikutano ya Kitalimungu iliyoandaliwa na Jimbo Kuu, walimu watano na umma waliojaza chumba cha mkutano, mtawa wa Ufaransa aliendeleza mada: Sinodi, uekumene na mazungumzo ya kidini. Sr. alifafanua kwamba Kanisa lazima "lisiogope utofauti, kwa sababu tayari linaibeba ndani yake yenyewe na hailazimishi usawa. Kwa hiyo limeitwa kutembea na kila mtu, si tu na Wakatoliki, Wakristo na watu wa imani nyingine," Sr. Becquart alisema, akiongeza kuwa Sinodi ni njia ya kuonesha hili, kwa sababu watu wote wana heshima sawa

Sinodi:Kanisa zima ni jumuiya inayojifunza

Katibu Msaidizi wa Sinodi alihitimisha kwa kueleza kwamba sinodi hurekebisha tofauti kati ya uongozi kama 'Eklesia docens'  yaani 'Kanisa la Kufundisha' na walei kama Eklesia inavyotambua (Kanisa la Kujifunza). Kwa njia hiyo Kanisa kwa ujumla linaweza kuwa Kanisa linalojifunza. Jioni hiyo Jumatano tarehe 17 Julai 2024 Sr  Becquart alishiriki katika meza ya Mduara ya  umma katika uaskofu mkuu wa Rijeka-Rijeka juu ya mada ya mikutano Ukristo na Uislamu: katika huduma ya udugu katika ulimwengu uliogawanyika.

Katika uzoefu kama huu,uhusiano wa kweli kati ya watu tofauti huzaliwa

Baada ya uingiliaji kati wa wataalimungu watano wa mafundisho, Wakatoliki, Waprotestanti, Waorthodox lakini pia kwa mara ya kwanza imamu Mwislamu, mtawa huyo alikumbusha kwamba kuna sehemu ambapo Wakatoliki ni wachache, kama huko Bangalore, India, ambako alitembelea wakati wa mchakato wa sinodi, ilikuwa ni jambo la kawaida kuwashirikisha wawakilishi wa dini nyingine katika mikutano mahalia ya sinodi, wakati fulani. Na alimalizia kwa kusisitiza kwamba uzoefu kama vile Mikutano ya Kitaalimungu ya Mediterania ni ya thamani zaidi ya maneno na maandishi elfu moja juu ya mazungumzo, kwa sababu watu wenye mapenzi mema wanaweza kuingia katika uhusiano na kuunda upatanisho wa kweli wa tofauti ili kujenga ulimwengu bora.

Abdelsalam na Hati juu ya Udugu wa Kibinadamu

Katika ufunguzi mkutano huo  Jumatatu tarehe 15 Julai 2024, ujumbe ulisomwa kutoka kwa jaji Mohamed Abdelsalam, katibu mkuu wa Tuzo ya Zayed ya Udugu wa Kibinadamu na shahidi wa mazungumzo yaliyopelekea kusainiwa kwa Hati hiyo mnamo tarehe 4 Februari 2019 huko Abu Dhabi. Kuhusu Udugu wa Kibinadamu na Papa Francisko na Imamu Mkuu wa Al-Azhar, Ahmad Al-Tayyeb. Hati iliyowatia moyo waandaaji wa Mikutano katika kuchagua mada ya toleo hili, kama ilivyokumbukwa na Askofu Mkuu wa Rijeka-Rijeka Mate Uzinić. Abdelsalam alifafanua Hati hiyo kama moja ya matamko muhimu zaidi katika historia ya kisasa ya mwanadamu, matunda ya juhudi za kukuza kuishi kwa wanadamu na udugu, sio tu kati ya Waislamu na Wakristo ambao kwa pamoja wanawakilisha zaidi ya nusu ya idadi ya watu duniani, lakini pia kati ya watu wote, bila kujali tofauti zao. Kisha alishirikisha mwanzo wa Hati, ambayo alishiriki kibinafsi.

Mwanzo wa Azimio la Abu Dhabi

Yote haya yalianza na  jaji wa Misri ambaye alikumbusha, mnamo 2018, mkutano huko Vatican kati ya Papa Francisko na Imamu Mkuu wa Al-Azhar. Mazungumzo kati ya watu hawa wawili wakubwa wa kidini yaligeuka kuwa mjadala kuhusu dhahania ya mtoto wa miaka mitano na jinsi anavyoweza kujiendesha na kuwatendea wengine ambao wana imani tofauti atakapokuwa mtu mzima na kwenda chuo kikuu,” alisema Abdelsalam. Papa na mgeni wake walijiuliza maswali ni nini kingetokea “ikiwa maswali mazito ya kiroho yatazuka kati ya mwanafunzi huyo na wanafunzi wenzake, kama vile swali la ni watu gani watakwenda mbinguni na ikiwa watu wa mapokeo mengine ya kidini wanaweza kuokolewa.”

Maadili ya Hati:dira kwa ubinadamu

Kwa hiyo wakawa na wazo la kutoa nyenzo kwa ajili ya mwanafunzi huyu, “ili maswali haya yanapotokea, apate usaidizi katika taarifa ya kugawana ubinadamu iliyotolewa kwa pamoja na watu wawili wakubwa wa kidini duniani, wanaowakilisha Ukristo na Uislamu”. Kwa kuzingatia changamoto zinazotokana na migogoro na migogoro isiyo na kifani ambayo dunia yetu inakabiliana nayo hivi leo, Abdelsalam alihitimisha katika ujumbe wake, "sote tunahitaji kutunza maadili ya udugu wa kibinadamu yaliyoainishwa katika hati hii ya kihistoria, ambayo lazima iwe kama dira utu kutuongoza tena katika njia ya amani, haki na heshima”.

Uzinić:Injili dhidi ya hofu ya Ulaya

Katika hotuba yake ya utangulizi, Askofu Mkuu Mate Uzinić alikumbuka kwamba baada ya Septemba 11, 2001, janga, vita vya Ukraine na vita huko Gaza, "Ulaya imekuwa bara la hofu na kutokuwa na uhakika. Kama wataalimungu tunapaswa kujiuliza jinsi habari njema ya Injili inavyoweza kuwa nguvu ya ukombozi, jinsi gani tunaweza kuwaleta watu wa kizazi chetu karibu na utamaduni wa kukutana na mawazo ya udugu.  Na alisisitiza kwamba, kwa kujilisha hofu hii, vyama vya watu wengi vinakua ambavyo vinaweka msingi wa utambulisho juu ya kukataa mshikamano na ubinafsi wa kitaifa. Wanajiita Wakristo, "wakisahau kwamba utambulisho wao ambao kiukweli wa Kikristo, ni lazima uwe wazi, na ambao umewekwa kwenye mahusiano na mazungumzo. Mungu, katika Kristo, "alitaka ushirika na watu, na ikiwa tunakataa ushirika na wengine, basi tumesaliti ujumbe wa msingi wa Ukristo.

Waislamu wahamiaji na fursa mpya

Katika bara letu, Uzinić aliendelea kusema, "Mahusiano ya Wakristo na Waislamu yamepitia awamu mbalimbali", lakini hivi karibuni "kufunguliwa kwa jumuiya za Ulaya kwa wahamiaji Waislamu kuanzia nusu ya pili ya karne ya 20 kumetokeza aina mpya ya kuishi pamoja ambayo inatoa fursa mpya.” Kuanzia Ufaransa hadi Italia, hadi Bosnia-Herzegovina ambapo uwepo ni wa muda mrefu zaidi na Uturuki, Albania na Kosovo, ambazo zina Waislamu wengi, muktadha huu wa ndani unaweza pia kutufundisha kile ambacho Wakristo na Waislamu wanafanana, badala ya siku zote. kusisitiza kile kinachotutenganisha. Uzoefu wa kuishi pamoja kwa karne nyingi na mifano ya mafanikio ya mazungumzo na udugu "inaweza kututia moyo kwa hekima ambayo hutuweka huru kutoka kwa hofu. Labda hapa ndipo penye cheche ya kuokoa ya utambulisho wetu uliozimwa.

Wataalimungu Vijana  dhidi ya tabia ya  kujipenda

Kuwa wafuasi wa Kristo, alifafanua askofu mkuu wa Rijeka-Fiume, leo kunamaanisha kugundua na kutambua mwelekeo wa kidini wa dini nyinginezo. Waamini wa siku hizi, na hasa hao wataalimungu vijana, wanapaswa kuwasaidia watu wa zama zao kujitenga na tabia za kujipenda sana, ambazo ni mzizi wa kutovumilia, dharau na kuwatenga wengine. Akimnukuu mtaalimungu Tomáš Halík, profesa katika Shule ya Taalimungu katika kiangazi huko Dubrovnik mwaka wa 2021, Uzinić alisisitiza kwamba Ulaya ya Kikristo haimaanishi Ulaya ambayo inazuia kuwasili kwa wasio Wakristo. Lakini, kinyume chake, Ulaya ambayo inahakikisha kwamba kila mtu katika eneo lake anaweza kusali kwa Mungu kwa maneno yake mwenyewe na anaweza kufanya hivyo pamoja na mtu anayesali kwa njia tofauti."

Kamwe wasibadilishe mipaka kuwa shimo linalotugawa

Mahusiano haya, kwa upnade wa askofu mkuu, ni muhimu kwa amani ya dunia, kwa ajili ya kujenga udugu na urafiki wa kijamii, kama vile Papa Francisko amekuwa akikumbuka mara kwa mara. Alikumbuka kwamba udugu na watu wa imani na imani nyingine ndio msingi wa Hati ya Abu Dhabi, inayohamasisha mada ya Mikutano hii ya Kitheolojia, kama vile uhuru na uwajibikaji, kama vile vurugu ambazo wengine wanadai kufanya zinalaaniwa katika jina la Mungu. Kukataa kufuata kanuni za msingi hakumaanishi kurekebisha tofauti, akamalizia Uzinić, kama vile kuwakaribisha wahamiaji hakuna maana ya kufuta mipaka na kudharau sheria za nchi wanazoingia. Lakini katika siasa, kama vile katika teolojia, hatupaswi kubadilisha mipaka kuwa sanamu na mashimo yanayotugawa, badala yake kuwa mahali pa kukutania na maonyesho ya kuheshimu tofauti.

TAALIMUNGU HUKO RIJEKA
22 July 2024, 12:39