Maaskofu wa Nigeria. Maaskofu wa Nigeria. 

Nigeria:“Mkataba wa Samoa ni hatarishi kwa maadili yetu

Maaskofu Katoliki na Jukwaa la Kiislamu nchini Nigeria wamekataa Mkataba wa Samoa kwamba ni "Tishio kwa mamlaka na maadili ya Nigeria.Tuna wasiwasi kwamba mamlaka zetu za kiraia zinaweza kuwa hazifahamu kikamilifu athari za lugha potofu ya hati,ambayo inatishia uhuru wetu na maadili ya kitaifa." Aidha wanabainisha"Mkataba wa Samoa una marejeo 61 ya usawa wa kijinsia mitazamo ya kijinsia na ushirikiano wa kijinsia.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Maaskofu wa Nigeria na Jukwaa la Kiislamu la Nigeria walifafanua  Mkataba wa Samoa, uliokubaliwa tarehe 15 Novemba 2023, huko Apia (Visiwa vya Samoa) na Umoja wa Ulaya na nchi wanachama 27 na 79 za Umoja wa Mataifa ya Afrika, Caribbean na Pasifiki (OACPS)  kuwa ni “Tishio kwa uhuru na maadili ya Nigeria.” Makubaliano mapya, ambayo yatatumika kama mfumo wa jumla wa kisheria wa mahusiano yao katika kipindi cha miaka ishirini ijayo, yatachukua nafasi ya yale ya awali (makubaliano ya Lomé ya 1975 na makubaliano ya Cotonou ya 2000).

Kuna mchanganyiko wa itikadi mamboleo

Tarehe 28 Juni 2024, Balozi wa Nigeria mjini Brussels alitia saini makubaliano hayo kwa niaba ya serikali yake. Katika taarifa yenye vipengele 25, iliyochapishwa tarehe 10 Julai 2024 mwishoni mwa Mkutano wao, Maaskofu hao, wakijitambulisha kama "walinzi na waelekezi, waliojitolea kwa dhati katika ukuaji wa kimaadili, kidini na kiutamaduni wa nchi yetu pendwa", wanawaalika kwa dharura Serikali ya Nigeria ili "kupendekeza marekebisho ya makubaliano au kujiondoa". Hii ni kwa sababu kwa mujibu wa tamko hilo, lililotiwa saini na Askofu Mkuu Lucius Iwejuru Ugorji, wa Jimbo Kuu katoliki la Owerri, na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Nigeria(CBCN) na makubaliano hayo yanaonekana kuwa yasiyo na hatia na ya kuvutia kijuu juu tu, lakini chini yake, yamechanganywa kwa uangalifu na itikadi za kiulimwengu za baada ya mambo leo ambazo zinadhoofisha kwa kiasi kikubwa imani za kimaadili, kiutamaduni na kidini za raia wa Nigeria.”

Mamlaka zaweza kutotambua kikamilifu lugha potofu ya hati

Maaskofu hao kwa njia hiyo wanabainisha tena kuwa: “Tuna wasiwasi kwamba mamlaka zetu za kiraia zinaweza kuwa hazifahamu kikamilifu athari za lugha potofu ya hati, ambayo inatishia uhuru wetu na maadili ya kitaifa. Kadhalika wanabainisha kuwa: "Mkataba wa Samoa una marejeo 61 ya usawa wa kijinsia, mitazamo ya kijinsia na ushirikiano wa kijinsia,” wanaeleza Maaskofu. "La muhimu zaidi ni Kifungu cha 2.5: Wanachama lazima waendeleze kwa utaratibu mtazamo wa kijinsia na kuhakikisha kuwa usawa wa kijinsia unajumuishwa katika sera zote."

Kuna zaidi ya jinsia 110 zinazodai kupendezwa na neno usawa wa kijinsia

Kulingana na Baraza la Maaskofu wa Nigeria(CBCN) "Neno jinsia sio neno lisilo na hatia tena. Kuna zaidi ya jinsia 110 ambazo zinadai kupendezwa na neno usawa wa kijinsia. Kwa sababu hiyo Maaskofu wanaomba “serikali ipendekeze kujumuishwa kwa kifungu kikubwa katika Makubaliano ya Jumla na katika Itifaki ya Kikanda ya Afrika ambayo hakuna chochote katika Mkataba huu wa kisheria kinaweza kufasiriwa kwa njia ya kujumuisha majukumu yoyote kuhusu mwelekeo wa kijinsia, utambulisho wa kijinsia, elimu ya kina ya ngono, utoaji mimba, uzazi wa mpango, kuhalalisha ukahaba, ndoa za watu wa jinsia moja au haki za ngono za watoto." Vinginevyo, Maaskofu wanahitimisha wakisema: “Nigeria inapaswa kujiondoa katika mkataba wa Samoa ikiwa Umoja wa Ula (EU) utakataa marekebisho yaliyopendekezwa. Mfano tayari umewekwa na Afrika Kusini, ambayo ilijiondoa kwenye Mkataba wa Cotonou mnamo 2023.”

Wito kwa Serikali ya shirikisho kuondoa makubaliano ya Samoa

Katika Jukwaa la Kiislamu la Nigeria mwishoni mwa mkutano wake lilitoa wito kwa serikali ya shirikisho kujiondoa katika makubaliano ya Samoa bila kuchelewa zaidi. “Tunashauri serikali za shirikisho na serikali kushauriana na watu kuhusu mikataba yoyote muhimu inayohusiana na maisha yao ya kijamii, kielimu na kidini kabla ya kusaini makubaliano. Wazazi na walimu wanapaswa kuzingatia kwa makini elimu ya maadili ya watoto wao na kuwa waangalifu hasa kuhusu kile wanachotazama kwenye mitandao ya kijamii.”

12 July 2024, 16:46