Juma la 50 Kijamii,Italia:Katika moyo wa demokrasia.Kushiriki kati ya historia na wakati ujao
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kuanzia tarehe 3 hadi 7 Julai 2024 litafanyika Juma la 50 la Mafundisho Jamii ya Kikatoliki, nchini Italia kwa kuongozwa na kauli mbiu: Katika moyo wa demokrasia. Kushiriki kati ya Historia na wakati ujao. Tukio hili linatawaona katika Makao makuu ya Mkoa wa Friuli Venezia Giulia ,washiriki 1,100 kutoka majimbo yote, vyama, harakati na sehemu kubwa ya washiriki wa Italia yote, (hasa kati ya vijana zaidi) takwimu za kumbukumbu, zenye uwezo wa kuweka tumaini na uaminifu, lakini pia kuelekeza mabadiliko kuelekea chaguzi ambazo ni muhimu leo hii kwa faida ya nchi. Lakini pia wataona ushiriki wa Rais wa Jamhuri ya Italia, Bwana Sergio Mattarella katika ufunguzi wake tarehe 3 Julai 2024 na Baba Mtakatifu Francisko ambaye atafunga kazi hiyo kwa Maadhimisho ya Misa Takatifu tarehe 7 Julai 2024.
“Huko Trieste, karibu wajumbe 1,100 watafanya kazi bega kwa bega kwa siku 5, wakilinganisha uzoefu wao na kutafuta majibu na mapendekezo kwa pamoja kwa manufaa ya nchi. Nguvu mpya kabisa, ambayo kiukweli, ni jaribio kubwa la kijamii la kukutana na kushiriki. Wakatoliki wanaitwa kuwa sehemu hai za jumuiya iliyo wazi, ya ulimwengu mzima ambayo inakaa eneo fulani lakini inapumua maisha ya ulimwengu mzima. Ndiyo maana tunaamini kwamba leo, katika msimu huu, Wakatoliki bado wana mengi ya kusema na kutoa kwa ajili ya maisha ya nchi”. Sebastiano Nerozzi, profesa wa Historia ya Mawazo ya Kiuchumi katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Moyo Mtakatifu na katibu wa kamati ya kisayansi na maandalizi ya Juma la Jamii ya Wakatoliki nchini Italia alisema hayo maudhui na malengo ya Juma la 50 ya Kijamii ya Wakatoliki nchini Italia katika Vyombo vya Habari za Kidini la Baraza la Maaskofu Italia ( SIR) kuhusiana na tukio hilo la Juma.
Profesa Nerozzi aliendelea kusema kuwa: “Matarajio ya Juma la Kijamii yanaongezeka na tunaona ishara zote kwenye vyombo vya habari, vyombo vya habari vya kijadi na kijamii, lakini juu ya yote katika maswali tunayokusanya kwa kuzunguka maeneo na kuzungumza na watu hata mbali na Kanisa ambao wanatuuliza habari juu ya nini kitatokea huko Trieste. Kiukweli, sisi pia tuna hamu ya kujua ni nini kitakachotolewa katika Trieste kati ya maelfu ya watu ambao watafanya kazi bega kwa bega kwa siku 5, kulinganisha uzoefu wao na kutafuta pamoja majibu na mapendekezo kwa manufaa ya nchi. Nguvu mpya kabisa, ambayo ni kweli,” Nguvu ambayo tayari imeanza katika mchakato wa maandalizi na ambayo tunatarajia itaendelea, baada ya Juma la Jamii, katika maeneo Kutoka Trieste kwenda chini. Ni Kanisa ambalo linazidi kujifunza kusikiliza na kujisikiliza lenyewe.
Mchakato wa njia ya Sinodi umeibua michakato ya mazungumzo ya kina kati ya watu, michakato ambayo, ikizingatiwa kwa umakini, inaweza kuzaa matunda ya kudumu kwa maisha ya Kanisa kuanzia katika maeneo. Njia ya maandalizi ya Juma la Kijamii, iliyoanza Septemba 2023, ilikuwa sehemu ya njia ya sinodi, inayohusisha maeneo ya ujenzi wa barabara na vijiji, lakini pia vyama na vikundi vya hiari. Aina ya utafiti mkubwa kuhusu faida na ugumu wa ushiriki ambao ulivutia ushiriki wa zaidi ya vikundi 200 kwa zaidi ya watu 2,000. Matokeo yake yalikuwa hati ya kurasa chache Kushiriki nchini Italia, iliyohaririwa na prof. Giovanni Grandi (mjumbe wa Kamati) na timu yake, ambayo mambo ya kuvutia sana yanaibuka kuhusu mienendo ya ushiriki.
Ni katika Muktadha huo tarehe 2 Julai 2024 saa 10 jioni huko Trieste katika Ukumbi wa Jumba la Mkoa umefanyika Mkutano wa vyombo vya habari ili kuwakilisha Juma la 50 ya Kijamii Katoliki nchini Italia. Katika mkutano na vyombo vya habari washiriki: ni Askofu Mkuu Luigi Renna, wa Catania na Rais wa Kamati ya Kisayansi na maandalizi ya Juma la Kijamii Katoliki, Italia; Askofu Enrico Trevisi, wa Trieste; Elena Granata, Makamu Rais wa Kamati ya ya Kisayansi na maandalizi; Mario Anzil, makamu rais na mjimbe wa Utamaduni na Michezo wa Mkoa unaojitegemea wa Friuli Venezia Giulia; Giorgio Rossi, Mjumbe wa sera za kisiasa za Utamaduni na Utalii katika Wilaya ya Trieste. Mratibu wa Uwakilishi huo ni Stefania Careddu, mwandishi wa Ofisi ya Kitaifa kwa ajili ya Mawasiliano kijamii ya Baraza la Maaskofu Katiliki nchini Italia (CEI).