Kard.Zuppi,Trieste:wakatoliki ni wahusika wa ujenzi wa demokrasia!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika ufunguzi wa Toleo la 50 la Kijamii Katoliki nchini Italia katika jiji la Trieste, tarehe 3 Julai 2024, Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Italia Kardinali Matteo Zuppi na Askofu Mkuu wa Jimbo katoliki la Bologna alitoa hotuba yake ambayo aliyoibua mambo kadhaa. Kati ya hayo ni kukataa no a “populismi,” lakini ili Ndiyo ushiriki, kujenga demokrasia shirikishi, ambapo leo hii demokrasia inateseka kwa sababu jamii zinazidi kuwa na mgawanyiko. Kardinali Zuppi alitoa mfano wa tukio la hivi karibuni nchini Italia kuhusu Satnam Singh muhamiaji aliyekufa shambani kwamba ni mmoja wa kusema hapana (Kufanyisha kazi za suruba na ukosefu wa hadhi ya ubinadamu., na kwa hiyo: “Kanisa halidai mapendeleo.
Katika Hotuba hiyo Kardinali pia alitaja juu ya kushuka kwa idadi ya watu yaani kuzaliwa na ukosefu wa usawa, kutopendezwa na ushiriki wa kidemokrasia (Watu hawapigi kura) na kwa kusisitiza alisema: “Kanisa linazungumza kwa sababu liko huru, na demokrasia yetu inaweza na lazima iwe bora zaidi na jumuishi zaidi. Amani na ustawi ni wema wa kutafuta mara moja tu kwa wote lakini ili kufanya hivyo upendo wa kisiasa unahitajika. “ Kardinali Zuppi alisisitiza kwamba “Wakristo lazima wachukulie kwa uzito, uzalendo wao, kwani “wakristo wa leo hii hawawezi kujiondoa katika uwajibikaji wao, na hatutaki kuona mipaka inakuwa kuta na mbaya zaidi mitaro na kwa hiyo ukatoliki wa kiitalia uwesifungiwe katika Sakrestia.”
Kwa njia hiyo Kardinali Matteo Zuppi alisema Wakatoliki Italia wanatamani kuwa wahusika wakuu wa ujenzi wa demokrazia shirikishi, mahali ambapo hakuna anayebaguliwa au anaachwa nyuma. Akiwa mbele ya Mkuu wa Nchi. Kardinali Zuppi, alishukuru Mkuu wa Nchi Sergio Mattarella kwa huduma yake kama mlezi na mdhamini wa demokrasia na maadili ya Jamhuri yetu na Ulaya. Na ni matumaini, kutoka kwa mji wa mpakani kama Trieste, wa kujenga mustakabali wa nchi kwa kila mtu, na kuweka hadhi ya binadamu katikati. “Tangu 1907 hadi leo, Ukatoliki wa Italia haujasimama na kutazama, haujajifungia ndani ya sacristia, umefikiria na kufanya kazi sio kwa ajili yake yenyewe, bali kwa manufaa ya watu wote wa Italia.”
Katika salamu zake Askofu Enrico Trevisi, wa Jimbo katoliki la Trieste wakati wa ufungunzi, alifafanua juu ya maneno ya “Ushiriki na ushirikishwaji. Kwa kuongozwa na ufubunifu wa Roho Mtakatifu (Yh 3,8), Askofu alisimulia ulinganisho kati ya ulimwengu wa shule na tukio la Juma la kijamii. Kuna baadhi ya walimu ambao walijiuliza swali: tunawezaje kusaidia madarasa yetu kufanyia kazi mada ya Juma la Kijamii ya Kikatoliki? Bila shaka tunaweza kufikiria kuhusu ushiriki na demokrasia, lakini tunaweza pia kufanya majaribio ya ushiriki. Swali ambalo liliishi katika mantiki ya elimu ya rika, wanafunzi wa shule ya Sekondari walikwenda kusaidia wanafunzi wa shule ya Msingi na wanafunzi wa shule ya Msingi walikwenda watoto wa shule ya Chekechea. Harakati ya mawazo na hatua ambayo iliruhusu kuundwa kwa “nguo ndefu sana ya meza. Na kuifanikisha “tulianza kutoka katika familia, majumbani.
Rais wa Jamhuri ya Italia Bwana Sergio Mattarella, katika hotuba yake kwenye sherehe za ufunguzi wa Juma la 50 la Kijamii la Wakatoliki nchini Italia, iliyoandaliwa katika Kituo cha Mikutano huko Trieste kwa kuongozwa na tema: “Katika kiini cha demokrasia. Ushiriki kati ya historia na siku zijazo,” alisema: “Demokrasia haishindwi milele. Jumuiya zetu zinazidi kuonekana kuwa hatari. Katika mabadiliko ya enzi tunayoishi, tunahisi shida zote, na wakati mwingine hata wasiwasi fulani, katika utendakazi wa demokrasia. Mkuu wa Italia alibainisha kwamba “ leo tunaona masuala muhimu ambayo hayajawahi kutokea, ambayo yanaongezea katika matatizo ya zamani. Hakika, mfuatano wa hali tofauti za kihistoria na tabia zao zinazobadilika zinahitaji utambuzi wa uangalifu na mara kwa mara wa hali hizo.”