Ireland:21 Agosti ni kumbukizi ya kutokea Maria huko Knock
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Zimekuwa siku za Novena katika Mdhabahu ya Maria huko Knock nchini Ireland mahali ambapi tarehe 21 Agosti ya kila mwaka ni kumbukizi ya ambayo inakumbusha mnamo Alhamisi yam waka 1879 alituokea Bikira Maria, Mtakatifu Yosef una Mtakatifu Yohane kwa watu kumi na tano. Kuanzia tarehe 14 hadi 22 Agosti ni siku za novena ambapo katika Madhabahu hayo inakumbusha kwamba tarehe 19 Machi 2021 Baba Mtakatifu Francisko aliitambua rasmi kuwa ni Madhabahu ya Maria na Ekaristi ya kimataifa kupitia Baraza la Kipapa la Uinjilishaji mpya, mfululizo wa sherehe na maadhimisho ya kila siku yamefanyika, na ambayo mwaka huu 2024 yameongozwa na kauli mbiu: “Kunong'ona na Mungu. Unasali namna gani.?”
Baadhi ya wageni maalum wametafakari mada miongozi mwa wato hauoni mwandishi wa Uingereza Austen Ivereigh, mwimbaji wa Ireland Donna Taggart, Mjesuit Richard Leonard, mhudumu wa kibinadamu, Toni Pyke na Askofu Kevin Doran wa Elphin ambao tayari walitembelea Knock. Katika tafakari yake, mwaliko wa kuketi kwenye meza ya Mungu ndiyo ilikuwa mwaliko wa uhusiano kama alivyoelezaAaskofu katika mahubiri yake Dominika tarehe 18 Agosti 2024 wakati, akitoa maoni juu ya mada ya kazi ya uumbaji. “Utunzaji wote na umakini kwa undani unaoingia katika uumbaji hutumika kuweka msingi wa uhusiano, alisema. Moyo wa ujumbe wa Mwanzo ni kwamba kila kitu tunachokiona karibu nasi kilitolewa kwetu ili kutusaidia kuishi kwa undani katika uhusiano wetu na Mungu, hata hivyo, ikiwa ni kweli kwamba Mwanzo haukukusudiwa kuwa kitabu cha historia ni tunda la kutafakari kwa sala juu ya uzoefu wa kuishi katika ulimwengu, bila kudhoofisha sayansi kwa njia yoyote.”
Askofu alisisitiza kuwa “ Hakika, sayansi inakaribia ukweli kwa kuchunguza ushahidi wa kimwili, wakati imani inatafuta majibu kwa maswali ambayo sayansi haishughulikii, maswali kuhusu maana na madhumuni ya kuwepo kwa mwanadamu. Lakini ukweli ni ukweli, iwe unatoka kwa sayansi au kwa kutafakari kwa maombi.”
Katika Siku ya pili ya Papa Francisko nchini Ireland, katika fursa ya Mkutano wa IX wa Familia Duniani tarehe 26 Agosti 2018 alitembelea madhabahu ya Bikira Maria wa Knock na kuongoza sala ya Malaika ya Bwana mbele ya waamini na mahujaji wapatao 45,000. Baba Mtakatifu wakati huo alisema: “Hakuna mtu yeyote asiye weza kuguswa na historia ya wadogo ambao wameteseka na manyanyaso na ambao wameibiwa udogo wao bila hatia au waliondolewa kwenda mbali na wazazi, kuachwa katika uchungu mkubwa. Hata katika Madhabahu ya Bikira Maria huko Knock kabla ya kusali sala ya malaika wa Bwana, Baba Mtakatifu alirudia kuzungumza juu ya janga lililofunguliwa wazi la manyanyaso yaliyo wakumba watoto kutokana na wahusika wa Kanisa nchini Ireland.
Baba Mtakatifu alisema, tunapaswa kuwa na msimamo halisi wa kutafuta ukweli na haki, ninaomba msamaha kwa Bwana kwa ajili ya dhambi hizi, fedheha, na usaliti ambao umeshitakiwa na familia nyingi za Mungu. Na kuthibitisha juu ya kutafuta suluhisho la pendekezo ya kutoruhusu janga ili lisitukie tena. Baba Mtakatifu aliomba kwa maombezi ya Bikira Maria, kwa ajili ya waathirika na ili wote walio husika waweze kuendelea daima katika haki na kufanya malipizi ya ghasia nyingi zilizotukia. Kwa hiyo katika ziara ya Kitume ya 24 ya Baba Mtakatifu Francisko nchini Ireland, na ikiwa ni fursa ya Mkutano wa Familia duniani, mara baada ya kufika Knock aliingia katika Kanisa dogo la Kutokea kwa Bikira Maria huko katika Kijiji cha Contea Mayo kinachojulikana duniani kote kutokana na Madhabahu hiyo na kusali.
Papa alifanya tendo la sala kabla ya kutoa zawadi ya Rosari ya dhahabu kwa Bikira Maria, kama utambuzi wa muhimu wa nchi ya Ireland wa kusali Rosari kama ilivyo utamaduni wake ndani ya familia. Baba Mtakatifu alisema, kwake Maria anayetambua furaha na ugumu wa uzoefu wa kila kitu katika nyumba, anamkabidhi familia zote dunia, ili Mama Maria uweze kuwasaidia katika shughuli zao za kueneza Ufalme wa Kristo na kuwatunza wale walio wa mwisho. Kati ya matukio na dhoruba ambazo zinasonga nyakati hizi, imani ndiyo iwe ngao na wema ambao kwa mujibu wa utamaduni wa taifa, wavumilie kila aina ya chochote ambacho kinataka kupunguza hadhi ya mwanaume na mwanamke walio umbwa kwa mfano wa Mungu, amewaalika katika kushiriki ukuu wa maisha ya milele.”