2024.08.13:Camping ya Chama cha Matendo ya vijana Katoliki huko Savignano,Jimbo la Rimini Italia:"Unalo neno langu Yeremia" 2024.08.13:Camping ya Chama cha Matendo ya vijana Katoliki huko Savignano,Jimbo la Rimini Italia:"Unalo neno langu Yeremia" 

Italia,Savignano(ACR):Likizo ya kiangazi kwa watoto:“Unalo Neno langu Yeremia”

Parokia ya Mtakatifu Lucia huko Savignano,Jimbo la Rimini,Italia lilifanya likizo ya watoto wa Chama cha matendo ya Vijana Katoliki kuanzia Julai 28 hadi 4 Agosti katikati ya msitu wa Casentino,Toscana.Waliongozwa na mada:“Unalo neno langu Yeremia,”ili kumjua Mungu anavyosindikiza watu wake licha ya kumkataa.Walisindikizwa na wahuishaji pamoja na Padre Giorgio Farina,Paroko wa Parokia.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika ya Camping za kila mwaka zinazoandaliwa na Parokia ya Mtakatifu Lucia, huko Savignano Sul Rubicone, Jimbo Katoliki la Rimini nchini Italia, kuanzia watoto wa shule za msingi  hadi Vyuo Vikuu ni mojawapo ya vipindi muhimu sana katika makuzi ya kiroho kwa vijana kila mwaka! Hata kwa mwaka 2024, Parokia hiyo imeendeleza Camping mbali mbali  pia kwa Watoto wa shule ya Msingi katika Nyumba ya likizo za kiangazi  katika Mkoa wa Toscana kwenye msitu uitwao Casentino kuanzia tarehe 28 Julai hadi 4 Agosti 2024. Watoto hao wa  Chama cha Matendo ya vijana Katoliki, Savignano (ACR), walisindikizwa na wahuishaji wao wakiwa na Paroko wao wa Parokia, Padre Giorgio Farina. Kauli mbiu iliyoongoza likizo na mafunzo ya vijana 2024 ni :“Unalo Neno langu Yeremia” kwa njia hiyo, ni masomo kutoka kitabu cha Nabii Yeremia.

Safari ya kwenda Camping kwa ajili ya Watoto wa ACR Savignano Julai 28 hadi 4 Agosti
Safari ya kwenda Camping kwa ajili ya Watoto wa ACR Savignano Julai 28 hadi 4 Agosti

Katika siku hizo watoto kuanzia umri wa miaka 7 hadi 11 wamefanya uzoefu wa kuishi pamoja maisha ya kijumuiya. Siku ilikuwa ikianza mapema na mazoezi, kifungua kinywa na wakati wa tafakari fupi kupitia  maigizo kwa kuoongozwa na kitabu cha Nabii Yeremiah. Ni somo gumu lakini  kwa ubunifu wa viongozi wa watoto hao na usikivu, kila mwisho wa siku watoto walitoa muhtasari mzuri wa kushangaza kwa kile ambacho waliweza kukiishi kupitia somo hilo. Kwa njia hiyo mada ziligawanyika kwa siku kuanzia  Dominika tarehe 28 Julai 2024 ambayo ilikuwa ni Kukaribisha na kusikiliza. Ili kufanya kazi kuwa rahisi, watoto waligawanywa katika makundi madogo yaliyopewa majina ya Agano jipya ili kubaki katika mantiki ya somo lilioongoza siku hizo. Kwa hiyo kulikuwa na kundi la Wababilonia, Wasiria, Wamisiri na Wamedia katika kuharakisha shughuli zao ndogo ndogo za michezo na mafunzo yak ila siku.

Kutembea kuelekea milimani
Kutembea kuelekea milimani

Jumatatu tarehe 29 Julai 2024 mada ilikuwa ni mshangao na kutafuta (kwa kuongozwa na Somo la Yeremia 7,1-15. Siku hiyo iliwafundisha watoto kuwa na mshangao kwa kila kitu na kutafuta kutazamana wao kwa wao na kupokeana jinsi walivyo na kumtafuta Bwana. Baada ya chai na maigizo ilikuwa ni safari ya mlimani, wakiwa wanatembea walizungumza kati yao, na walitakiwa baadaye watazame mandhari ya msitu uliojaa mimea na miti na uzuri wa kazi ya uumbaji. Baadaye ilikuwa ni kutazamana uso kwa uso ili kujuana vizuri, na kuulizana maswali.

Vijana wa Chama cha matendo Katoliki wakiwa mlima Falterona
Vijana wa Chama cha matendo Katoliki wakiwa mlima Falterona

Tarehe 30 Julai 2024  kwa kuongozwa na Somo la Yeremia 17, 5-10, watoto walifundishwa kuamini Mungu hata wakati hatujuhi yote yale yanatotusibu. Mungu anao mpango kwa kila mmoja wetu na tunaweza kuamini Yeye kwa sababu anatujua vizuri zaidi ya mwingine yeyote yule. Tunapaswa kubaki kwa hiyo waaminifu, karibu na Yeye na kufanya kile cha haki hata kama  daima siyo jambo  rahisi.

Watoto waliweza kushangaa msitu mzuri
Watoto waliweza kushangaa msitu mzuri

Tarehe 31 Julai 2024, mada ilikuwa ni kushuru Mungu kupitia Somo la Yeremia, 23,1-8. Siku hiyo  watoto walijifunza namna ya kumshukuru Mungu. Kwa ishara ndogo ndogo wahuishaji kupitia maigizo walitafuta kuonesha jinsi neno llinaweza kufanya kuelewa umuhimu wa mchungaji  yaani kiongozi wa maisha yetu. Katika hilo Nabii Yeremiah aliwaeleza viongozi wa watu wa Israeli kile ambacho Mungu alisema kwao kwa kuwa hawakufuata Neno la Mungu na hawakuweza kutunza muungano wa watu. Katika wakati wetu tunaweza kifikiria Mungu kama Mcungaji ambaye tunamwamini. Ni Yeye ambaye anatuelekeza njia. Anatufanya tuhisi tumelindwa na anatusaidia kujikamilisha. Mungu anakabidhi watu tulio nao karibu kazi ya kutunza, na anatutazama na upendo na kwa njia hiyo lazima tumshukuru.

Ni kwa jinsi gani hali ya mazingira ya kutembea milimani
Ni kwa jinsi gani hali ya mazingira ya kutembea milimani

Tarehe 1 Agosti 2024, mada ya siku ilikuwa ni uwajibakaji na kutunzana. Watoto kupitia somo la Nabii Yeremija 29, 1-14, kama ilivyokuwa kwa wahuishaji vijana kupitia maigizo, somo lilikuwa ni kuona Mungu anavyotangazia watu wa Israeli wanavyopaswa kubaki katika Nchi ya Babilonia kwa miaka 70. Na wakati huo huo, leo hii hata sisi tunapaswa kujifunza kuwa na zawadi ya subira na wakati wa kusubiri kusiwe wakati wa kupoteza muda, bali ni muda wa kuishi kikamlilifu na uwepo wa kujionesha bora kila sekunde. Mungu katika subira hiyo hatuachi kamwe, hata katika hatua mbaya sana, ya maisha yetu, badala yake anatutunza, sisi kwa kutualika kuwajibika kwa ajili ya wengine kwa kuwasindikiza katika safari ndefu ya maisha yao.

Wakati mzuri pia wa kushirikishana katika Camping
Wakati mzuri pia wa kushirikishana katika Camping

Tarehe 2 Agosti 2024 siku hiyo iliongozwa na mada ya kushirikisha na kuona kupitia somo la Nabii Yeremia 31, 1-14. Hawa ni watoto wadogo, lakini kupitia maigizo wanalielewa somo vizuri kwamba kupitia Nabii Yeremiah Mungu anawalekea watu uhamishoni huko Babilonia ambao kwa mara nyingine watajua huruma yake na upendo mkubwa. Kiukweli licha ya ukosefu wa imani ya watu wake, Mungu hawaachi bali anapyaisha ahadi yake, na kuahidi wokovu wa Israeli. Bwana anatangaza kuwa kurudi kwa Waisraeli kutoka huko Babilonia kutakuwa ni mwanzo wa watu wote, mwanzo mpya ambao utapelekea Ushirikishwaji wa furaha kwa watu wote. Kwa njia hiyo watu wote wataweza kuona wale wanaowazunguka ishara za upendo wa Mungu.

Kutazama maua ya kondeni ambayo hakuna binadamu anayemwagilia maji bali Mungu tu
Kutazama maua ya kondeni ambayo hakuna binadamu anayemwagilia maji bali Mungu tu

Tarehe 3 Agosti 2024 kama kawaida siku ilianza na mazoezi na pia somo ambalo liliongoza siku nzima katika mafunzo na michezo ya kupanda na kushuka katika mlima. Mada kuu iliyoongoza ni Uwezekano. Yeremia alitangaza namna mpya ya kuishi, kutoka maneno yaliyochongwa katika mwamba, sasa yanapitia kwenye hisia zetu ambazo Mungu anatufanya kuhisi moja kwa moja katika moyo. Namna hiyo mpya ya kuwasiliana, lazima ikutane na uwezekano wa kusikiliza na kuwa tayari katika moyo wetu kwa Yule aliyetuzawadia, yaani Mungu. Kwa njia hiyo kwenda,  yaani kukubali kutumwa kwa sababu moyo uliojaa Roho Mtakatifu unasukuma kwenda kila mahali na kupeleka Habari Njema ya Agano jipya la Mungu. Hayo yalikuwa ni kupitia Somo la Nabii Yeremia 31,31-34 ambaye Bwana anathibitisha jinsi ambavyo “atasamehe dhambi zao za watu wake na hatakumbuka kamwe dhambi hizo.”

Kufika Mlima Falterona
Kufika Mlima Falterona

Katika siku hizo pia kulikuwa na matembezi ya kupanda na kushuka mlimani, ambapo watoto waliweza hata kufika  mlima wa Falco wenye urefu wa mita(1658) na kuendelea hadi Mlima Falterona(1654),karibu na Falco ambao ni wa pili katika vilima vya mkoa wa Toscana na Emilia Romagna nchini Italia. Kupanda na kushuka milima kunawawezesha watoto kupumua hewa nzuri katika mazingira tofauti na waliyozoea. Lakini vile vile hapakosi kuanguka, kujikwaa nk. Na katika maisha mambo hayo hayawezi kukosekana kuanzia udogo hadi ukubwa.

Watoto wakionesha chumba cha Mkaa pweke Mtakatifu Romwald
Watoto wakionesha chumba cha Mkaa pweke Mtakatifu Romwald
Monasteri ya Camaldoli
Monasteri ya Camaldoli

Katika uzoefu huo wa kutembea katika misitu na kupanda milima vile vile watoto walipata fursa ya kutembelea Monasteri ya Kibenedikitini ya Watawa Wacalmadoli, baada ya kutembea Km 8 kutoka nyumba ya likizo. Hapo walikutana na Padre Alessandro Barban (O.S.Bcam) akiwa pamoja na Shemasi, DonBosco Mligo (O.S.BCam)kutoka Tanzania ambaye ni mmoja wa Jumuiya hiyo. Padre Alessandro Barban kwa ukarimu wake aliwaomba watoto licha ya kuchoka wampamtie dakika 20 tu  za ukimya ili awaeleze historia kwa ufupi ya Monasteri hiyo. Padre alieleza juu ya Historia ya ishala zao na Kanisa la kwanza la Monasteri hiyo jinsi lilivyokuwa limejengwa kwa mbao tu na sasa limenakishiwa vizuri kwa namna mpya. Padre huyo, aidha alisimulia juu ya jengo la mwanzilishi wa Monasteri hiyo Mtakatifu Romwald na mahali alipokuwa akiishi. Watoto walifurahi sana lakini pia viongozi wao ambao walikuwa hawajapata  fursa ya kuingia ndani ya Monasteri hiyo.

Padre Alessandro Barban ak akielezea historia ya Monasteri hiyo
Padre Alessandro Barban ak akielezea historia ya Monasteri hiyo
Kutazama uzuri wa Kanisa la Camaldoli
Kutazama uzuri wa Kanisa la Camaldoli

Dominika tarehe 4 Agosti 2024 ilikuwa ni siku ya kuagana, mara baada ya misa Takatifu wakiwa na wazazi wao waliokuja kuwapokea. Hapo ilikuwa ni kuongozwa na masomo ya siku ambapo Somo la kwanza kutoka katika (Kut 16,2-4.12-15), lilisimulia jinsi Mungu alivyowalisha Waisraeli jangwani kwa kuwa baada ya kukombolewa utumwani Misri, Waisraeli walisafiri safari ndefu ya kuchosha. Walipofika jangwani, walitindikiwa chakula na wakakosa maji. Hivyo wakamnung’unikia Musa na Haruni wakiwaambia; “Laiti tungalikufa kwa mkono wa Bwana katika nchi ya Misri, hapo tulipoketi karibu na zile sufuria za nyama, tulipokula hata kushiba; kwani mmetutoa huko ili kutuua kwa njaa”. Mungu alisikia manung’uniko yao akamwambia Musa; “Tazama, mimi nitawanyeshea ninyi mvua ya mkate na nyama kutoka mbinguni; na hao watu watatoka nje na kuokota kila siku. Wakati wa jioni mtakula nyama, na wakati wa asubuhi mtashiba mkate; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.”

Siku moja kabla ya kuondoka watoto walifanya maigizo na michezo
Siku moja kabla ya kuondoka watoto walifanya maigizo na michezo

Katika Injili ilivyoandikwa na Yohane (Yh 6:24-35) ilikuwa inaeleza mafundisho ya Yesu juu ya habari za chakula kiletacho uzima wa milele, yaani Ekaristi Takatifu. Katika kusimulia ilibanisha kwamba  watu walimtafuta Yesu kwa shauku  kubwa, na walimkuta ng’ambo ya bahari, na kumuuliza Rabi, umekuja lini hapa? Yesu akijua mawazo yao, aliwaambia ukweli kwamba “ni kwa sababu walikula mikate wakashiba, ndiyo maana walimtafuta. Kwa namna hiyo Yesu aliwaonya wasikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali kile chakula kinachowaletea uzima wa milele.” Watoto wakati wa misa na hasa katika wakati wa maombi  walisoma maombi yao waliyoandika  vizuri kabisa wakimshukuru Mungu kwa uzoevu mzuri walioushi kwa siku hiyo saba za kiroho. Na zaidi hawakuwasahau wahushaji wao  Emanuel,Thomasi Davide, Sara, Giulia, Fiorella pia Padre Giorgio pamoja na wahudumu wote walioshiriki kuandaa kila siku chakula, chai na kila jambo kuwawezesha waishi vizuri kuanzia na Gabriele Vincenzi(Bebe) na wote.

Hapakukosa kumtakia heri ya kuzaliwa Padre Giorgio la Farina
Hapakukosa kumtakia heri ya kuzaliwa Padre Giorgio la Farina
Likizo ya kiroho kwa watoto wa ACR Savignano Jimbo la Rimini
13 August 2024, 11:14