Majimbo matatu katika eneo la mashariki mwa DRC yameishi kwa miongo kadhaa katika hali ya kutokuwa na utulivu iliyosababishwa na kuwepo kwa mamia ya makundi yenye silaha. Majimbo matatu katika eneo la mashariki mwa DRC yameishi kwa miongo kadhaa katika hali ya kutokuwa na utulivu iliyosababishwa na kuwepo kwa mamia ya makundi yenye silaha. 

Limezinduliwa Jukwaa la amani linalohuishwa na wanawake wa dini tofauti mashariki mwa DRC

Katika semina iliyoandaliwa kuanzia tarehe 21 hadi 23 Agosti 2024 na Tume ya Haki na Amani ya Jimbo la Bukavu nchini DRC imeunda Jukwaa jipya kwa ajili ya amani litakaloongozwa na wanawake wa madhehebu tofauti.Lengo kuu ni kuimarishwa kwa mshikamano wa kijamii na kuishi pamoja kwa wanawake wa imani tofauti za kidini katika jimbo la kikanisa la Bukavu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Limeundwa Jukwaa la mabadiliko ya wanawake na amani liliundwa huko Kivu Kaskazini, Kivu Kusini na Maniema, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Kulingana na kile kilichowasilishwa kwa  Shirika la Habari za Kimisionari  Fides, uundaji wa ukweli mpya uliamuliwa wakati wa semina iliyoandaliwa kuanzia tarehe 21 hadi 23 Agosti 2024 na Tume ya Haki na Amani ya Jimbo la Bukavu. Lengo la mkutano huo ni kuimarishwa kwa mshikamano wa kijamii na kuishi pamoja kwa wanawake wa imani tofauti za kidini katika jimbo la kikanisa la Bukavu.

Wanawake wa Majimbo matatu kuunda jukwaa la amani

Jukwaa hilo linawaleta pamoja wanawake wa madhehebu tofauti ya kidini kutoka majimbo matatu ya mashariki mwa DRC, ili kushawishi ushiriki mkubwa wa wanawake katika kutafuta suluhisho la changamoto za uwiano wa kijamii. Kwa ajili hiyo, waanzilishi wa jukwaa hilo wanahimiza wanawake wa madhehebu mbalimbali ya kidini kutoa mchango wao katika kuleta amani kama mama, waelimishaji na walezi wa maisha. Pia wanawaalika wakazi wa eneo hilo kuonesha mshikamano na wakimbizi wa ndani wa Kivu Kaskazini, na kupinga mizozo inayosababisha vurugu ili kutoingia kwenye mtego wa wale wanaotaka kuendelea kupanda machafuko na kunyonya DRC.

Majimbo matatu mashariki wa DRC kwa miongo kadhaa hakuna utulivu

Majimbo hayo matatu katika eneo la mashariki mwa DRC yameishi kwa miongo kadhaa katika hali ya kutokuwa na utulivu iliyosababishwa na kuwepo kwa mamia ya makundi yenye silaha, ya ndani na ya kigeni. Kundi la M23 linaendesha shughuli zake zaidi katika Kivu Kaskazini, kundi lililojipanga vyema na lenye silaha, linaloungwa mkono na Rwanda, ambayo kulingana na uchunguzi wa Umoja wa Mataifa pia limepeleka jeshi lake katika ardhi ya Congo. Wanajihadi wenye asili ya Uganda kutoka ADF (Allied Democratic Forces) ambao wamejiunga na Dola ya Kiislam pia wanapamba moto kati ya Kivu Kaskazini na Ituri (mkoa mwingine wa Congo wenye matatizo). Kisha kuna makundi mengine kadhaa yenye silaha, yenye misingi ya kikabila, au kujilinda, ambayo huchangia kuongeza ukosefu wa usalama wa Kivu Kaskazini.

Vikundi 50 vya silaha vya ndani na nje

Inasadikika ni kama vikundi hamsini vyenye silaha vya ndani na nje (wenye asili ya Rwanda na Burundi) vinafanya kazi katika Kivu Kusini. Maeneo ambayo yameathiriwa zaidi na uwepo wao ni yale ya Uvira na Fizi-itombwe. Katika jimbo la Maniema, karibu makundi ishirini ya wenyeji yenye silaha yanaripotiwa. Kwa ujumla katika majimbo matano ya mashariki mwa DRC (Ituri, Kivu Kaskazini, Kivu Kusini, Maniema na Tanganyika) kuna angalau vikundi 266 vyenye silaha (252 vya ndani na 14 vya asili ya kigeni) kulingana na hesabu iliyofanywa mnamo 2023 na mratibu wa mpango wa kupokonya silaha, uondoaji wa silaha, Uokoaji wa Jamii na Uimarishaji (P-DDRCS). Uwepo wao unachochewa na usafirishaji wa utajiri mkubwa wa maeneo haya (coltan, dhahabu, bati, mbao na mengineyo) yanayonyonywa kinyume cha sheria bila ya kuwepo udhibiti mzuri wa eneo hilo na serikali ya Congo (ambao askari wake, zaidi ya hayo, wanatuhumiwa kushiriki katika biashara hizi).

29 August 2024, 14:09