Tafuta

Mons.Corrado Maggioni,Rais wa Kamati ya Kipapa ya Makongamano ya Kimataifa ya Ekaristi. Mons.Corrado Maggioni,Rais wa Kamati ya Kipapa ya Makongamano ya Kimataifa ya Ekaristi. 

Kongamano la 53 la Ekaristi Kimataifa,Ecuador,Septemba 8-15:Ekaristi inainamia udugu!

Mtazamo wa kiutamaduni wa Kongamano 52 zilizofanyika hadi sasa zinatuwezesha kufahamu maono ya kihistoria ya Kanisa,yaani taalimungu,liturujia na hali ya kiroho ya Ekaristi imekuwaje kwa muda na mahali.Sasa Kongamano la 53,katika nusu ya ulimwengu,linasikika kama wito uliosadikishwa kwa udugu unaoonekana kama zawadi kutoka Mbinguni.

Na Corrado Maggioni

Wazo la kuwaita watu kutoka nchi mbalimbali kwenye Kongamano la kuadhimisha Ekaristi na kutafakari umuhimu wake kikanisa na kijamii limekuwa na nia tangu mwanzo ya kufufua ufahamu kwamba uwepo wa Kristo kati yetu na kupitia kwetu ni moyo wa Kanisa na utume wake. Fumbo la Ekaristi kwa hakika linahusu Makanisa yote, kila parokia, katika Mwili wa Kristo kwenye jiografia ya sayari ya dunia. Kuwa pamoja, pamoja na historia, hisia, tamaduni, lugha mbalimbali, labda na majeraha ambayo bado yamefunguliwa kutokana na uadui, humaanisha kukazia fikira pekee inayoweza kutia chachu historia ya mwanadamu kiukweli na kuifanya kuwa unga mpya wa Ufalme wa mbinguni.

Mtazamo katika historia

Mapokeo ya Kongamano la Kimataifa la Ekaristi, pamoja na yale waliyoyahamasisha kati ya Watu wa Mungu, yanathibitisha matokeo ya matukio haya katika miji na Mataifa yaliyoyakaribisha na kwa vizazi vya mapadre, watawa na walei walioshiriki. Mtazamo wa kiutamaduni wa Kongamano 52 zilizofanyika hadi sasa zinatuwezesha kufahamu maono ya kihistoria ya Kanisa, yaani, taalimungu, liturujia na hali ya kiroho ya Ekaristi imekuwaje kwa muda na mahali. Kuanzia Kongamano la kwanza lililofanyika huko Lille, mnamo mwaka 1881, yote yafuatayo yalidhihirishwa na maonesho ya hadhara ya kuvutia yaliyolenga kuthibitisha imani katika “uwepo halisi” wa Kristo katika Ekaristi na kuongeza ibada ya Kiekaristi. Harakati za Kongamano zilikomaa nchini Ufaransa kufuatia hali ya kiroho ya Mtakatifu Pierre-Julien Eymard (+1868), ya mapadre mashuhuri kama vile Mwenyeheri Antoine Chevrier (+1879) na Gaston-Adrien de Ségur (+1880), kwa walei wengi watu, akiwemo Léon Dupont (+1876) na hasa Émilie Tamisier (+1910), Mhuishaji wa Makondamano. Ikumbukwe kwamba, tangu mwanzo, jukumu la walei, wanawake na wanaume, ambao waliweka nguvu na wakati wao  ili kuweka maslahi hai na kuandaa, ilikuwa ya maamuzi. Mahali halisi la Kongamano la Ekaristi paliendelea kuwa ya kimataifa na ya kimisionari, ikivuka mipaka ya nchi za Ulaya: hii inaoneshwa na Kongamano la huko  Montreal (1910), Chicago (1926), Sydney (1928), Carthage (1930), Buenos Aires ( 1934), Manila (1937), Rio de Janeiro (1952), Bombay (1964), Bogotá (1968), Melbourne (1973), Philadelphia (1976), Nairobi (1985), Seoul (1989), Guadalajara (2004), Quebec (2008) na Cebu (2016).

Matukio mbali mbali ya makongamano

Yalikuwa ni matukio ambayo “kiekaristi” yaliashiria njia ya Kanisa katika nchi hizi na katika mabara yao. Kwa kuzingatia Amerika ya Kusini, ni lazima tukumbuke Kongamano la Buenos Aires nchini Argentina, lilioongozwa na mada “Ufalme wa Kijamii wa Kristo kwa njia ya Ekaristi” (1934), la Rio de Janeiro huko Brazili juu ya mada “Ufalme wa Ekaristi wa Kristo Mkombozi.” (1955), kutoka Bogotà Colombia juu ya mada: “Vinculum charitatis “Dhamana ya Upando” na ziara ya Paulo VI na mkutano wake wa kihistoria na Wakulima 300,000 wa Amerika ya Kusini (1968), kutoka Guadalajara nchini  Mexico juu ya mada: Ekaristi, mwanga na maisha ya milenia mpya” (2004). Sasa Kongamano la 53 huko Quito, nchini  Ecuador, katika “nusu ya ulimwengu”, linasikika kama wito uliosadikishwa kwa “udugu” unaoonekana kama zawadi kutoka Mbinguni na wakati huo huo dhamira ya kibinadamu ya kubadilisha uhusiano mbaya kuwa dhamana ya kidugu, ndani ya matatizo ya dunia ya leo hii. Mabadiliko ya enzi tunayokabiliana nayo yamesababisha kila mtu, ingawa katika njia tofauti, kukuza imani kwamba hakuna anayejiokoa peke yake, kama Papa Francisko  anavyopenda kurudia.

Kongamano la Ekaristi leo hii

Uelewa upya wa fumbo la Ekaristi linalochochewa na harakati za kiliturujia na kukomazwa na Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican, umeelekeza pia Kongamano la Ekaristi ili kukuza uhusiano usiotenganishwa kati ya adhimisho la Misa na ibada ya Ekaristi nje yake, kuhusiana na mang’amuzi ya watu na jamii. Kongamano la Ekaristi Takatifu hivyo limekuwa ni fursa na sababu ya kueleza Kanisa la Ekaristi, kwa kuzingatia Mtaguso wa II wa Vatican na mageuzi ya kiliturujia yaliyotokana nayo. Katika Hati ya sasa iliyopyawishwa ya De sacra Communion et de cultu Mysterii Eucharisti extra Missam yaani, “Ya Ushirika Mtakatifu na ya Ibada ya Fumbo la Ekaristi nje ya Misa”(1973) ilitilia maanani hili, likiweka wakfu namba 109-112 kwa Kongamano la Ekaristi, ikitoa maelezo juu ya maana ya Kongamano kama “kukujikita katika sala, kujitolea na kuonesha mambo ya kuzingatia katika maandalizi yake: kama vile katekesi juu ya Ekaristi, hasa ​​kama fumbo la Kristo anayeishi na kufanya kazi ndani ya Kanisa; kushiriki katika liturujia ambayo inakuza usikilizaji wa kidini kwa neno la Mungu na hisia ya kidugu ya jumuiya; mipango ya chachu ya kiinjili na utekelezaji wa kazi za kijamii zinazopendelea ukuzaji wa watu na ugawaji unaostahili wa bidhaa, pamoja na bidhaa za muda; hatimaye, tunakumbuka vigezo vya msukumo wa Kongamano: “adhimisho la Ekaristi ni kitovu na kilele cha madhihirisho na aina mbalimbali za uchaji Mungu”; utafiti wa kina wa mada iliyopendekezwa unahimiza ushiriki wa vitendo; mikutano ya maombi na kuabudu kwa muda mrefu Sakramenti Takatifu katika makanisa fulani jijini; maandamano na Sakramenti Takatifu lazima yawe ya kielelezo.

Ushirikiano wa kimataifa wa Kongamano

Ushirikiano wa kimataifa wa Kongamano unadhihirisha umoja wa fumbo la Ekaristi ambalo hutengeneza kila mbatizwa, kila mmoja katika hali yake ya maisha, kama kila familia ya Kikristo, jumuiya ya kidini, parokia, jimbo. Kongamano za Ekaristi zinazoadhimishwa hadi sasa zinadhihirisha hili kwa sifa zao wenyewe. Quito 2024 na mada ya marejeleo. Uchaguzi wa mji wa Quito, Ecuador, kama mahali pa Kongamano la 2024 (8-15 Septemba) umechochewa na miaka 150 ya kuwekwa wakfu kwa taifa la Amerika Kusini kwa Moyo Mtakatifu wa Yesu (25 Machi 1874). Ilikuwa ni kitendo kilichokuzwa na rais wa wakati huo wa nchi ili kuweka historia ya Ecuador mikononi mwa Yeye anayependa ubinadamu bila mipaka na masharti. Kumbukumbu ya tukio hilo la kijamii iliwekwa katika nadhiri ya kujenga hekalu adhimu kwa Moyo wa Yesu, ambayo leo imekuwa moja ya alama za mji wa Quito. Kwa ajili ya maadhimisho haya, maaskofu wa Ecuador wamechagua kuwa mwenyeji wa Kongamano la Kimataifa la Ekaristi 2024 Zaidi ya hayo, kama Paulo VI alivyosema, “zawadi kuu ya Moyo wa Yesu ni Ekaristi” (tazama Investigabiles divitias Christi). Kuamini Moyo wa Kristo uliojeruhiwa kunamaanisha kujiweka katika shule ya Upendo ambayo inatiririka kwa uhuru kwa ajili ya maisha ya wengine, yenye nguvu kuliko ubinafsi wetu wote, chuki na migawanyiko. Mandhari ya Kongamano la Quito ni hili lifuatalo: “Udugu wa kuponya ulimwengu», ukiangaziwa na maneno ya Yesu ya kichochezi “Nyinyi nyote ni ndugu” (Mathayo, 23, 28).

Utume wa uponyaji  ulimwenguni

Kauli ya mada inang'aa kwa nuru ya Ekaristi iliyo wazi mara moja: inaunganisha udugu ndani ya Kanisa, unaojengwa na Ekaristi, na utume wake wa uponyaji ulimwenguni, kama kurefusha uwepo wa Kristo, Mwokozi wa watu wote. , roho , nafsi na mwili. Wito wa Ekaristi kwa udugu unavuka mipaka kati ya mataifa na watu wanaowatunga, kwa lugha na tamaduni zao, ikiwa ni pamoja na kukutana na mapigano ya jana na leo. Tukifikiwa kiekaristi kwa upendo unaobubujika kutoka kwa Moyo wa Kristo, tunajitambua kuwa ni ndugu, watoto wa Baba mmoja, wajenzi wa udugu unaoponya mahusiano kati ya wanadamu, na dunia na mazingira muhimu. Ekaristi ni wito endelevu, kila tunapoadhimisha, kuishi kama watoto wa Baba wa mbinguni ndani ya Mwana ambaye ni Kristo, na kuishi kama ndugu, bila kumtenga mtu yeyote. Ni matibabu kwa ugumu ambao kila mtu hubeba ndani yake mwenyewe na ni agizo la uponyaji kwa majeraha ya ulimwengu tunamoishi. Mada ya Kongamano inavuka njia mbalimbali zilizooneshwa na hati za  Papa: Kwanza kabisa sinodi, ambayo ni uzoefu wa kuishi badala ya dhana ya kueleweka, kama Francisko anavyotukumbusha mara nyingi. Njia ya sinodi tunayopitia, katika ngazi ya kijimbo, kitaifa na kiulimwengu, ni dhahiri pia inaangazia Kongamano la Kimataifa la Ekaristi. Waraka huo huo wa Fratelli tutti, juu ya udugu na urafiki wa kijamii, unatilia shaka moja kwa moja kazi ya kongamano, tukio la kufurahisha la kuleta uadilifu wa Papa katika kitambaa cha kikanisa .

Vyanzo vya msukumo wa hati ya msingi

Mada ya udugu katika Kongamano la Quito ilichunguzwa kwa kina katika hati maalum, inayoitwa Maandishi ya Msingi. Iliyochapishwa mnamo 2023, na inapatikana katika lugha mbali mbali, ambayo inaweka miongozo ya kujiandaa kwa Kongamano, nchini Ecuador kwanza kabisa kama ilivyo katika nchi zingine, na inakumbuka sababu za kutafakari zinazoashiria siku za kusherehekea za kongamano. Maandishi huzingatia vipengele viwili vya kutia moyo. Ya kwanza inawakilishwa na vyanzo halali kwa wote, zaidi ya shule halali za Kitaalimunungu na kiutamaduni: Maandiko matakatifu, hati za Mtaguso wa Pili wa Vattican, vitabu vya kiliturujia (Missale Romanum, pamoja na Institutio generalis na Praenotanda ya Ordo lectionum Missae; De sacra Communion et de cultu Mysterii Eucharisti extra Missam), kuhusu  mapapa na maaskofu, hasa uaskofu wa Amerika ya Kusini, Katekisimu ya Kanisa Katoliki; kwa kuwa fumbo la Ekaristi pia linahusu utauwa maarufu, Orodha ya utauwa na liturujia maarufu inakumbukwa. Kwa kuwa si risala juu ya Ekaristi, vyanzo vya msukumo vimetajwa kwa msisitizo wa mada.

Nyaraka za kitume za Papa 

Kwa mfano, kutoka kwa Papa Francisko kuna marejeo ya barua za kitume: Evangelii gaudium na Fratelli tutti, ya kitume ya Desiderio inayotaka, katika vifungu kutoka kstika mahubiri na hotuba. Waraka wa Ecclesia de Eucharistia umenukuliwa na Mtakatifu Yohane Paulo II, wakati Wataka wa kitume wa  Sacramentum caritatis na waraka wa Deus caritas est wa Papa Benedikto XVI. Upande wa pili, muhimu kwa kuunganisha Ekaristi na mang’amuzi ya maisha, unawakilishwa na ushuhuda wa watu walioweza kutafsiri fumbo lililoadhimishwa Altareni katika uchaguzi wa maisha ya Kikristo. Takwimu za Mtakatifu Oscar Romero († 1980), padre wa Mdominikani Antonio de Montesinos na Leonidas Proaño Villalba, Askofu wa Riobamba, eneo lenye wakazi wengi wa kiasili nchini Ecuador zimetolewa. Ushuhuda wa Wakristo walioitumikia Injili kwa uhuru wa upendo ni fasaha zaidi kuliko maneno ya kuwasilisha nguvu ya Ekaristi inayojenga udugu, ukaribu, mshikamano, uponyaji wa madonda ya ulimwengu. Hati ya msingi, kwa hivyo, ni dirisha wazi juu ya mada ya Kongamano la Quito. Inasaidia kujua tutazungumzia nini, mada gani zitashughulikiwa, ni masuala gani yanayotuhusu na changamoto gani zinazotungoja.

Monsinyo Corrado Maggioni, Rais wa Kamati ya Kipapa ya Makongamano ya Kimataifa ya Ekaristi.

30 August 2024, 12:10