Tafuta

Ekaristi ni kitovu cha maisha ya Mkristo. Ekaristi ni kitovu cha maisha ya Mkristo. 

Madagascar:Shukrani na kujitoa,waamini 30elfu walifika katika Kongamano la III la Ekaristi Kitaifa

Askofu Mkuu Benjamin Marc Balthason Ramaroson,wa Antsiranana,wakati tafakari kwenye Kongamano la III la Ekaristi Kitaifa alikazia mambo mawili:kwanza kabisa,Ekaristi inawakilisha shukrani.Na lengo lingine ni umuhimu wa sadaka,kwa sababu Ekaristi ni sadaka.Yesu mwenyewe anatufundisha kujitoa sadaka.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Jimbo la Antsiranana lilikuwa mwenyeji wa Kongamano la tatu la Kitaifa la Ekaristi Takatifu la Madagascar, lililofanyika katika mji wa Antsiranana ulioko kaskazini mwa kisiwa hicho katika siku za hivi karibuni kuanzia tarehe 23 hadi 25 Agosti 2024. Waliohudhuria sherehe za ufunguzi walikuwa, miongoni mwa wengine, maaskofu wote wa Madagascar na Rais wa Jamhuri ya Madagascar, Andry Rajoelina pamoja na Bi wake. Katika fursa ya tukio hilo hata, Baba Mtakatifu Francisko alituma barua maalum ambapo alisisitiza madhumuni ya Ekaristi katika utume na maisha ya Kanisa, na zaidi  umuhimu wa kuabudu Ekaristi. Papa aidha aliandika kuwa  Kongamano hilo “liwasaidie kugundua tena umuhimu wa kukutana, kusali na kujitolea wenyewe na wengine katika nyayo za Yesu katika Ekaristi” na akikumbuka, kama alivyosema katika Ujumbe wa kamati ya maandalizi ya Kongamano la Kitaifa la Ekaristi la Marekani, tarehe 19 Juni 2023, kwamba “Ekaristi inatusukuma kuwa na upendo wa dhati kwa jirani yetu.”


Kwa upande wake, Askofu Mkuu wa Antsiranana, Benjamin Marc Balthason Ramaroson, alikazia mambo mawili: kwanza kabisa, Ekaristi inawakilisha shukrani. Katika muktadha wa umaskini uliokithiri kama ule wa Madagacar, kuzungumza juu ya mchango wa bure inaonekana kama ndoto! Lakini Yesu anatufundisha kutoa hadi kujitoa kabisa; lengo lingine lilikuwa juu ya umuhimu wa sadaka, kwa sababu Ekaristi ni sadaka. Kongamano hilo, ambalo mwaka huu 2024 limekwenda sanjari na kuadhimisha miaka mia moja ya “Harakati ya Ekaristi ya Vijana, lilikuwa ni wakati muhimu wa mafunzo si tu kwa mahujaji elfu 30 waliofika mahali hapo bali pia kwa ulimwengu wote wa Kikatoliki wa Madagascar, katekesi na tafakari zinazotangazwa kupitia mitandao ya kijamii na radio ya Kikatoliki.

Kongamano III la Ekaristi Kitaifa huko Antsiranana Madagascar
27 August 2024, 15:25