Kikundi cha Waliowekwa wakfu(Ordo virginum). Kikundi cha Waliowekwa wakfu(Ordo virginum). 

Italia,Ordo Virginum:umeihitishwa mkutano wa Kitaifa nauchaguzi wa wakuu 2024-2026

Askofu Ricciardi,Askofu Msaidizi wa Jimbo la Roma,mhusika wa mawasiliano ya Baraza la Maaskofu Italia CEI wa OV aliyeshiriki siku nne za Mkutano wa kitaifa huko Torino kuanzia Agosti 25-28 Agosti,alibainisha:“Mkutano wa kitaifa wa Ordo Virginum huko Valdocco-Turino ulikuwa wakati wa neema kubwa,uliokuwa chini ya uangalizi wa Mtakatifu Maria Msaada wa Wakristo na Don Bosco."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kuanzia tarehe 25 hadi 28 Agosti 2024 ulifanyika mkutano wa kitaifa katika Jimbo Kuu la Torino kwa Watu waliowekwa wakfu wajulikanao (Ordo Virginum. “Bikira aliyewekwa wakfu katika maelewano  ya Kanisa: utunzaji wa mahusiano” ndiyo ilikuwa kauli mbiu ya mkutano huo ambao kati ya washiriki na watoo mada alikuwa Kardinali Giorgio Marengo,(Mkonsolata)Mwakilishi wa Kitume wa Ulaanbaatar nchini (Mongolia). Kwa siku nne za majadiliano na maombi yalifanyika katika nyumba ya Don Bosco, ya Valdocco huko Torino nchini Italia pia yaliongozwa na Sr. Katia Roncalli, Mfransiskani na mhusika mkuu wa Udugu wa  Evangelii Gaudium ambaye tarehe 26 Agosti 2024 alijikita na mada: “Kutoka katika mahusiano yanayotokana na Kristo hadi mahusiano yanayozalisha maisha na Askofu Mkuu Roberto Repole, wa Jimbo Kuu la Torino ambaye tarehe 27 Agosti 2024, alizungumza juu ya mada ya “Maisha ya kuwekwa wakfu na mahusiano katika Kanisa la jimbo.”

Utunzaji wa Upendo kwa wadhaifu

Tarehe 28 Agosti 2024 ambayo ilikuwa ni siku ya mwisho  kulikuwa na  meza ya mduara ambayo iliongozwa na mada: “Wanawake waliowekwa wakfu: utunzaji wa upendo kwa udhaifu katika maisha ya kila siku,” ambapo Sr. Maria Silvia wa Shirika la Wadominikani wa Bethania(nyumba ya wafungwa ya Lorusso na Cutugno huko Torino-sehemu ya Wanawake), Sr. Elena Bernasconi (Wa shirika la watawa wa Mtakatifu Giuseppe Benedetto Cottolengo wa Torino) na Rosanna Tabasso wa (Fraternità della Speranza-Sermig-(Udugu wa Matumaini-Sermig) waliweza kuwapatia shuku kubwa washiriki 200 waliowekwa wakfu, walioko kwenye malezi na wawakilishi wa majimbo wa OV na tafakari zao na ushuhuda. 

Kufahamu ukaribu wa Ordo Virginum

“Mkutano wa kitaifa wa Ordo Virginum huko Turino-Valdocco ulikuwa wakati wa neema kubwa, uliopatikana chini ya uangalizi wa Mtakatifu Maria Msaada wa Wakristo na Don Bosco. Tumefahamu ukarimu wa Ordo Virginum ya mahali hapo na tumepumua hamu ya utakatifu katika maisha ya kila siku, katika kujitolea upya kwa kutunza uhusiano na Mungu na wengine katika utoshelevu wa wale ambao wameyafanya maisha yao kuwa zawadi. Shukrani za pekee sana kwa Askofu Roberto Repole ambaye alitusaidia kufahamu uzuri wa Kanisa na utambulisho wa bikira aliyewekwa wakfu ndani yake.  Kwa hivyo Sr Katia Roncalli na sauti zingine ambazo zilikuwa ishara ya mwaliko mzuri wa kurejea kwenye njia pamoja ili kuwahudumia wanadamu kwa furaha,” alisema hayo Askofu Paolo Ricciardi, msaidizi wa Jimbo la Roma, mhusika wa  mawasiliano ya Baraza la Maaskofu Italia  CEI wa OV, ambaye alishiriki katika siku  zote nne huko Turino.

Uchaguzi wa viongozi wapya wa OV 2024-2026

“Wakati wa mkutano, kikundi kipya cha mawasiliano kilichaguliwa na tunatumaini kuendelea na huduma yake kwa Ordo nchini Italia ili kukuza ukuaji wake wa kibinadamu na ushirika. Kwa kuutazama Mwaka Mtakatifu, waliowekwa wakfu nchini Italia wazidi kuwa ushuhuda na taswira ya Kanisa kama bibi arusi na wasaidie kufunua uso wa Kristo ambaye, kama Sanda inatuonesha, ni uso wa msalaba mfufuka, matumaini pekee ambayo hayakatishi tamaa,”  alisema Askpfu Ricciardi. Kikundi kipya kilichochaguliwa kwa viongozi wa kuunganisha majimbo nchini Italia, kwa kipindi cha miaka miwili 2024-2026, kinaundwa na Marta Bartolucci kutoka (jimbo la Jesi, mwalimu), Domenica De Cicco (Jimbo la Nola, mwalimu), Marinella Mandelli. (Jimbo kuu la Milano , mwalimu), Viviana Paliotta (Jimbo la Roma, daktari).

Misa ya tarehe 26 Agosti 2024 askofu Giraudo Msaidizi wa Jimbo Kuu la Torino

Askofu Alessandro Giraudo, askofu msaidizi wa Jimbo la Torino nchini Italia, akiwa katika misa Takatifu katika Kanisa kuu la Maria Msaada wa Wakristo, iliyoadhimishwa tarehe 26 Agosti 2024  wakati wa mkutano wa kitaifa wa Waliowekwa wakfu “Ordo Virginum,” na ambao umehitimishwa  tarehe 28 Agosti, 2024 kwenye Nyumba ya Don Bosco-Valdocco,Torino alianza kusema katika mahuburi: “Siyo rahisi kuanza juma na siku kwa Neno hili ambalo tumetoka kulisikia hivi punde, kwa shtaka hili maradufu ambalo Yesu anawaambia waandishi na Mafarisayo na ambalo, kwa namna fulani, pia anaelekeza kwetu sisi kuwa waamini ya kuwa wanafiki na kuwa vipofu.” Katika mahubiri hayo kwa kufafanua Injili iliyosomwa Askofu alisisitiza kuwa: “Mzizi wa unafiki ni katika kujaribu kujielewa wenyewe, kwa kutotambua kwamba tumeitwa kusindikizana na sio kushikilia, kutotumia na kutojichukulia. Na mzizi mkuu wa upofu ni kutoweza kutambua Mungu tunayemwamini ni nani na kwa hiyo furaha ya kweli iko wapi ambayo tuliomba katika sala ya tuliyoanza yano katika adhimisho la Ekaristi.”


Ni katika hilo Askofu aliotoa wito kuwa: “Tunaweza kukaribisha, basi, sala na ahadi ambayo ilipatana na maneno ya Paulo kwa jumuiya ya Thesalonike, jumuiya ambayo ilikuwa inaanza kupoteza mvutano wake kuelekea furaha hiyo ya kweli. Na mwaliko wa sala, ahadi ambayo tunapokea kwa mara nyingine tena kutoka kwa Mungu ni kwamba tunapokuwa katika ushirika naye tunaweza pia kupitia magumu ya safari ya kila siku bila kupoteza shauku hiyo ya kina, upendo huo ambao umetushinda, kwamba, furaha ambayo tumeahidiwa na ambayo tayari tunapata tunapokuwa na ujasiri wa kujivua unafiki wetu, ya shauku hiyo ya kuwa sawa na kuweza kushinda kitu au mtu fulani, kushikwa daima na Kristo na kuweza kumwona na kumtambua yule ambaye kwa mara nyingine tena anajitoa nafsi yake kwa ajili yetu, Yeye ambaye kweli ni furaha isiyo na mwisho, ni kweli ahadi ya uzima, ni Neno kweli ambalo hurejesha njia yetu na kuangaza mtazamo wetu.”

29 August 2024, 15:20