Tafuta

2024.08.29 PAPUA NEW GUINEA - MAAnDALIZI YA PAPA:BANGO LA MAKARIBISHO HUKO VANIMO 2024.08.29 PAPUA NEW GUINEA - MAAnDALIZI YA PAPA:BANGO LA MAKARIBISHO HUKO VANIMO  

Papua New Guinea:kufika kwa Papa ni bembelezo la roho

Padre Diaz,mtawa wa Shirika la Neno Kufanyika Mwili,anatayarisha makaribisho ya Papa huko Baro na Vanimo.Mwargentina,amekumbuka mikutano na aliyekuwa na Kadinali Bergoglio huko Buenos Aires:alitusaidia sana kujenga uwepo wetu.Matarajio miongoni mwa watu wa kiasili ni makubwa,umaskini ni mkubwa sana;lakini kuwaona watu wenye kiu sana ya Mungu ni tukio la mbinguni.

Vatican News

Katika Kanisa ambalo bado ni changa, lililo hai, na lina njia chache sana lakini za kujenga, matukio ya mbinguni. Ndilo linalomsubiri Baba Mtakatifu Francisko huko Papua New Guinea, katika hatua ya pili ya Hija yake ya kitume huko Asia na Oceania itakayoanza tarehe 2 Septemba 2024. Padre Alehandro Diaz, mwenye asili ya Argentina,na mtawa wa Shirika la Neno lililofanyika Mwili, na mmisionari kwa muda wa mwaka mmoja tu katika kijiji cha Wutung, aliviambia vyombo vya habari vya Radio Vatican kuhusu maandalizi ya mapokezi hayo ya kipapa. Katika mazungumzo hayo Padre Alehandro alikuwa na  sauti ya kutuliza, akiwa pamoja na mtawa mwenzake ambao walianzisha mchakato wa ujenzi kile kitakachokuwa Monasteri ya kwanza ya kiume katika nchi nzima. Ndani ya mwaka huu Padre huyo  anaamini awamu tatu ya mchakato wa ujenz itakamilika ambayo itashuhudia muundo uliojengwa katika eneo kama dakika 40 kwa gari kutoka Vanimo. Kwa njia hiyo Shauku ya kuwekwa kwa jiwe la kwanza ni kubwa na itashirikishwa na Papa ambaye atakwenda katika jiji la Vanimo (lenye wakazi wenyeji elfu 150, ambao karibu elfu 45 ni Wakatoliki) Dominika tarehe 8 Septemba 2024 kwa ziara ya masaa machache tu.

Waamini wakatoliki huko Vanimo, Papua New Guine
Waamini wakatoliki huko Vanimo, Papua New Guine

Kwa hiyo Uwepo wake hapa ulitamaniwa hadi mwisho na Francesco ambaye, kama inavyojulikana, ana upendeleo kwa maendeo ya pembeni. Vanimo ni maskini sana, alisema Padre Alejandro, “lakini, tunamshukuru Mungu, kwa msaada wa watu wengi, tunafaulu kuandaa ziara hii. Juma  moja lililopita kila kitu kilionekana kuwa kigumu sana. Kulikuwa na ukosefu wa pesa kwa vitu vingi, kwa skrini kubwa, kwa mfano, kwa vifaa vya kiteknolojia ambavyo ilikuwa ngumu kupata. Hata hivyo, kutokana na msaada wa serikali na Kanisa, baada ya mazungumzo mengi, tulipokea vifaa hivyo ili tumkaribishe Papa kwa njia ya heshima zaidi.” Padre huyo alizungumzia umeme wa vipindi, uhaba wa maji ya kunywa, ukosefu wa bafu kuwa: “Tulilazimika kufikiria juu ya maelezo mengi. Tunapaswa kutoa chakula kwa wale ambao watatoka msituni, watu elfu. Tunafanya kazi kwa bidii sana, kwa roho ya shangwe na kujisadaka sana. Watu wamefahamu nini maana ya Papa kufika hapa. Kwa sababu Wenyeji watakusanyika hadi siku tatu kabla ya kuweza kutulia, watakuja bila kitu na hakuna hoteli zenye uwezo wa kuwakaribisha, zipo, mbili tu kwa wale walio matajiri. Watalala kwenye hema ambalo tutaliweka huko Vanimo. Tatizo kubwa ni usafiri,” alieleza matawa huyo, ambao haufai kuwakutanisha wale wote wanaopenda; barabara ni mbovu sana: “Yeyote anayetaka kumuona Papa alisema kwamba ni Yesu anayekuja, anataka kumsikiliza na kupokea baraka.”

Kutembelea vijiji vya misitu: matukio ya mbinguni

Miongoni mwa wale ambao watatoa ushuhuda kwa Papa katika uwanja wa Kanisa Kuu la Msalaba Mtakatifu, pia kutakuwa na Katekista. Hapa makatekista wanatimiza kazi muhimu kwa ajili ya tangazo la Injili: “Hao ndio watu wanaounga mkono imani ya vijiji. Wamefunzwa vyema katika imani, kila Dominika wanasambaza Komunyo. Wao ni 'mkono wa kuume' wa padre. Ni kuzaliwa kwa idadi kubwa ya miito ya ndani ambayo humshangilia zaidi mtawa: “Uchaji wa kidini wa Kanisa unaweza kuonekana sana. Ni Kanisa linalozaliwa, lina umri wa miaka themanini, tu na tunapanda mbegu na tayari tunaona matunda: ubatizo mwingi unafanyika, ushiriki katika liturujia za Ekaristi unasongamana, hasa kwa vijana na watoto.”Ilitubidi hata kuwaambia wavulana wanaotumikia altareni wasije wote pamoja kwa sababu ni wengi sana, wako 25 kwenye Misa ya  kila asubuhi! Ni wazi kwamba hakuna mtu anayewalazimisha, wanafanya hivyo kwa sababu wanataka.” Kwa kawaida ziara ya kutembelea vijiji hufanyika mwishoni mwa juma: unakwenda kwenye vijiji viwili au vitatu, ukisafiri kwenye barabara zenye matope, na kila aina ya vikwazo. “Wakati mwingine tunafika jioni sana lakini watu wanatusubiri, tunakiri, tunasherehekea Misa, watu wanatoka kijijini, wanashangilia wakituona tunafika, inakuvunja moyo, huwezi kufanya chochote zaidi ya kulia. Watu wana kiu sana kwa Mungu ambaye hujenga roho zetu. Licha ya matatizo yote, hii kwangu ni tukio la mbinguni, la kipekee, ambalo limeniimarisha katika ukuhani wangu, si kwa sifa yangu, bali zawadi kubwa kutoka kwa Mungu,” alihitimisha Padre Diaz mahojiano yake.

31 August 2024, 14:26