Kardinali Pizzaballa ameandika barua katika matazamio ya Siku kuu ya Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni. Kardinali Pizzaballa ameandika barua katika matazamio ya Siku kuu ya Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni. 

Patriaki Pizzaballa:Tuombe Maria aweze kufungua nuru ya dunia kwa ajili ya amani!

Kardinali Pizzaballa,Patriaki wa Yerusalemu,katika ujumbe wake kwa ajili ya Siku kuu ya Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni,amezungumzia juu ya Vita vya Mashariki ya Kati inayoendelea kusababisha huzuni na mateso,chuki,hasira na vurugu tu kwa kuweka umbali wa uwezekano wa kupata suluhisho. "Unabii wako na utimie:wenye kiburi watatawanyika katika mawazo ya mioyo yao."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Chuki, hasira na dharau huongeza vurugu na kuweka umbali wa uwezekano wa kutafuta suluhisho la mzozo wa Mashariki ya Kati. Hayo yameandikwa na Kardinali Pierbattista Pizzaballa, Patriaki wa Kilatini wa Yerusalemu, kwa ajili ya Wakristo wa Nchi Takatifu katika ujumbe mzito, kuelekea fursa ya Maadhimisho ya Sikukuu ya Kupalizwa mbinguni Bikira Maria itakayofanyika tarehe 15 Agosti 2024 huku akieleza machungu ya vita vya kutisha vilivyosababisha mateso na masikitiko ambayo, licha ya miezi mingi kupita bado hakuna suluhisho. Kardinali Pizzaballa anaandika kuwa hadi sasa, vita hiyo inazidi kuwa vigumu kufikiria hitimisho la mzozo huo, ambao “athari yake kwa maisha ya watu wetu ni ya juu na yenye uchungu zaidi kuwahi kutokea. Na pia inazidi kuwa ngumu kupata watu na taasisi ambazo inawezekana kufanya mazungumzo nao juu ya siku zijazo na uhusiano wa amani. Sasa hii, ni zingatio, lililochanganyika na vurugu nyingi na, bila shaka, pia na hasira, inaoyoonekana kuponda kila mtu.”

Kwa njia hiyo katika mtazamo wa Siku Kuu ya Bikira Maria Mpalizwa mbingu tarehe 15 Agosti, kama moja ya siku ambazo zinaonekana kuwa muhimu ili kugeuza mzozo huo  Patriaki wa Kilatini  amewaalika waamini  “kuwa na wakati wa maombi kwa ajili ya kuombea  amani kwa maombezi ya Bikira Mtakatifu aliyepalizwa mbinguni,” huku akionesha zaidi “nia ya kwamba parokia, jumuiya za kitawa na za kitume, na pia mahujaji wachache waliopo kati yetu  waungane katika dhamira ya pamoja ya amani wanayoikabidhi kwa Bikira Mtakatifu.” Kardinali ameandika: “Ni Miezi mingi sasa imepita tangu kuanza kwa vita hivi vya kutisha. Mateso yanayosababishwa na mzozo huu na kufadhaika kwa kile kinachotokea sio tu kwamba yanazuiliwa, lakini yanaonekana kuchochewa tena na tena na chuki, hasira na dharau, ambayo huzidisha vurugu na kusukuma mbali uwezekano wa kupata suluhisho. Kwa hakika, inazidi kuwa vigumu kuwazia hitimisho la mzozo huu, ambao athari yake kwa wanaoishi hivyo ni kubwa na chungu zaidi kuliko hapo awali. Inazidi kuwa ngumu kupata watu na taasisi ambazo mazungumzo juu ya siku zijazo na uhusiano wa amani inawezekana.

Sisi sote tunaonekana kukandamizwa na sasa hii, ambayo ina sifa ya vurugu nyingi na, kukubalika, hasira. Pamoja na hivyo, siku hizi zinaonekana kuwa muhimu kuweza kugeuza wimbi la migogoro, na miongoni mwao ni hasa tarehe 15 Agosti, ambayo kwetu sisi ni siku ya Maadhimisho ya” Kupalizwa kwa Bikira Maria Mbinguni. Katika siku hii, kabla au baada ya adhimisho la Ekaristi au wakati mwingine unaofaa, ninawaalika kila mmoja kwa wakati wa maombezi kwa ajili ya amani kwa Bikira Maria. Ni matumaini yangu kwamba, Parokia, jumuiya za kitawa tafakari na kitume na hata mahujaji wachache walioko miongoni mwetu wataungana katika dhamira ya pamoja ya amani tunayoikabidhi kwa Bikira Mtakatifu. Baada ya kutumia maneno mengi na baada ya kufanya kile tuwezacho kusaidia na kuwa karibu na kila mmoja, hasa wale walioathiriwa zaidi, kilichobaki ni sisi kusali. Kwa mtazamo wao maneno yoyote ya chuki ambayo yote yanasemwa mara nyingi, tungependa kutoa sala yetu, ambayo inajumuisha maneno ya upatanisho na amani. Katika kiambatanisho utapata sala kwa Mama Yetu wa Kupalizwa ambayo unaweza kusali siku ya Maadhimisho haya. Tuombe kwamba katika usiku huu mrefu tunaoishi, maombezi ya Maria Mtakatifu zaidi yafungue mwanga wa nuru kwa ajili yetu sisi sote na kwa ulimwengu wote.”

Sala kwa Bikira Maria Mpalizwa

“Maombi ya amani kwa Bikra Maria Mpalizwa Mbinguni, Mama Mtukufu wa Mungu, aliyeinuliwa juu ya kwaya za malaika, utuombee pamoja na Mtakatifu Mikaeli Malaika Mkuu na kwa uwezo wote wa malaika wa mbinguni na watakatifu wote, kwa Mwana wako mtakatifu zaidi, Bwana na bwana. Pokea kwa ajili ya Nchi hii Takatifu, kwa ajili ya watoto wake wote na kwa wanadamu wote zawadi ya upatanisho na amani. Unabii wako na utimie: wenye kiburi watatawanyika katika mawazo ya mioyo yao; wenye nguvu watapinduliwa kutoka katika viti vyao vya enzi, na wanyenyekevu hatimaye watainuliwa; wenye njaa washibishwe na mali, wenye amani watambuliwe kuwa wana wa Mungu na wapole wapate nchi kama zawadi. Yesu Kristo, Mwanao, atujalie sisi, ambao leo hii tunakusifu juu ya kwaya za malaika, akakuvika taji la ufalme, na kukuweka kwenye kiti cha enzi cha fahari ya milele. Heshima na utukufu una yeye hata milele na milele. Amina.”

Sala ya Kardinali Pizzaballa
10 August 2024, 15:33