Tafuta

Askofu Mkuu Maurice Muhatia Makumba,wa Jimbo Kuu la Kisumu, Kenya anasema:Mabadiliko ambayo vizazi vipya vinaomba yanaongozwa na maadili,hofu ya Mungu na kujaliana. Askofu Mkuu Maurice Muhatia Makumba,wa Jimbo Kuu la Kisumu, Kenya anasema:Mabadiliko ambayo vizazi vipya vinaomba yanaongozwa na maadili,hofu ya Mungu na kujaliana. 

Rais wa KCCB:tunataka kutoa kwa‘kizazi Z’mafunzo stahiki kwa mabadiliko ya Kenya

Katika mahojiano na Shirika la Habari za Kimisionari Fides na Rais wa Baraza la Maaskofu Kenya,Askofu Mkuu Muhatia Makumba,kuhusiana na maandamano ya hivi karibuni yalioongozwa na kikundi kiichwacho 'kizazi cha Z' alisema:“Vijana wa Kenya,wachangamfu sana na waliojaa nguvu, wanataka kubadilisha nchi kuwa bora.Ukweli huu wenyewe ni changamoto chanya kwa sisi sote.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Vijana wa Kenya wanachangamshwa na nia njema na wanataka mabadiliko makubwa nchini huo, aliyasema hayo Askofu Mkuu Maurice Muhatia Makumba, wa Jimbo Kuu katoliki la  Kisumu, na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya (KCCB), ambaye alitoa mahojiano na Shirika la Habari za Kimisionari Fides. Katika mahojiano hayo mwandishi anauliza kwamba;

Katika Maandamano ya hivi karibuni yaliyopelekea Rais wa Jahuri, William Ruto kuondoa sheria ya bajeti na kufanya mabadiliko ya serikali yalichangiwa na kile kinachoitwa kizazi Z. Je, unaonaje maendeleo haya?

Vijana wa Kenya, wachangamfu sana na waliojaa nguvu, wanataka kubadilisha nchi kuwa bora. Ukweli huu wenyewe ni changamoto chanya kwa sisi sote.

Je, tunaweza kuwapa mafunzo gani vijana wenye kiu ya haki?

Mabadiliko ambayo vizazi vipya vinaomba yanaongozwa na maadili, hofu ya Mungu na kujaliana. Hivyo Baraza letu la Maaskofu limejipanga kutoa mafunzo kwa vijana ili waweze kufanya mabadiliko hayo na kuongoza nchi.

Je, hii ina maana gani hasa?

Kama Baraza la Maaskofu tunachukulia matatizo ya vizazi vipya kwa uzito mkubwa. Katika ngazi ya kikanisa, kwanza kabisa, tunashughulika na vijana si kama kundi moja bali kulingana na umri wao. Watoto wanatunzwa na Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu, huku vijana na vijana wakiwa na makundi mbalimbali ya Kikatoliki kwa ajili ya mafunzo. Kwa njia hiyo tuna wingi wa makundi ambayo vijana wanaweza kujizoeza kulingana na umri wao ili waendelee kiimani.

Je, kwa maoni yako Kizazi kipya Z kitaweza kuzalisha viongozi ambao watakuwa na manufaa ya pamoja moyoni?

Ndio, kwa sababu ya jinsi vijana hawa wanavyochukulia masuala ya kijamii kwa usahihi kulingana na maadili ya mshikamano.Tutakuwa na uongozi bora kesho nchini Kenya na Afrika, hasa kwa maandalizi na mafunzo mazuri. Kwa sababu vijana wana nia njema.

Je, vijana wa Kenya wanaweza kuwa mfano kwa wenzao katika nchi nyingine za Afrika?

Hakika, lakini niruhusu kusisitiza juu ya mafunzo. Nchi nyingine za Kiafrika zitaweza kupata msukumo kutoka kwa nchi yetu, lakini zitalazimika kuwapa vijana wao mafunzo ya kutosha ili kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

Hatimaye, Kanisa nchini Kenya linapitiaje awamu hii?

Kanisa nchini Kenya linazidi kuchangamka, tuna watu wengi zaidi wanaoeneza imani, ndoa za kidini zinakua, kama vile miito ya kipadre na kitawa. Hebu tuombe sasa ili roho hii ya kufanywa upya ambayo imeenea miongoni mwa vijana wa Kenya iweze kuzaa matunda chanya kwa Kanisa na kwa nchi.

29 August 2024, 13:47