Askofu Flavian Matindi Kassala aliadhimisha Misa huko Geita ya shukrani kwa kutimiza miaka 25 ya upadre. Askofu Flavian Matindi Kassala aliadhimisha Misa huko Geita ya shukrani kwa kutimiza miaka 25 ya upadre. 

Tanzania:Askofu Kassala atimiza miaka 25 ya Upadre,tuwaombee mapadre!

Tarehe 11 Agosti 2024,Jimbo Katoliki la Geita,Tanzania,liliadhimisha Misa Takatifu kwa ajili ya Shukrani kwa Mungu kutimiza miaka 25 ya Upadre wa Askofu wa Jimbo hilo,Flavian Matindi Kassala.Katika misa mahubiri yaliongozwa na Askofu Nzigilwa wa jimbo la Mpanda."Mungu anawachagua watu wake kama alivyomchagua Musa,waende kuokoa watu wake."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Dominika tarehe 11 Agosti 2024 iliadhimishwa Jubilei ya Miaka 25 ya Daraja Takatifu ya Upadre wa Askofu Flavian Matindi Kassala, wa Jimbo Katoliki la Geita nchini Tanzania, ambapo Misa iliadhimishwa katika Parokia ya Bikira Maria Malkia wa Amani, mjini Geita. Katika Misa  hiyo  iliudhuriwa na Kardinali Protase Rugambwa, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Tabora Tanzania, Maaskofu wa Tanzania na nje yake, Mapadre washangwela wanaoadhimisha miaka 25 ya Upadre kwa mwaka 2024, na mapadre wote wa jimbo na nje ya majimbo, mashemasi, watawa wa kike na kiume, waseminari,na walei watu wa Mungu; vile vile viongozi wa Serikali, akiwepo mgeni rasmini, Dk. Mwigulu Lameck Nchemba, Waziri wa Fedha nchini Tanzania, aliyemwakilisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk. Doto Biteko, na viongozi wengine wa kisiasa na madhehebu mengine ya kidini.

Maadhimisho ya Jubilei ya miaka 25 ya Upadre wa Askofu Kassla
Maadhimisho ya Jubilei ya miaka 25 ya Upadre wa Askofu Kassla

Kabla ya kuanza misa, Takatifu, Askofu Kassala aliwasha mshumaa wa 26, hasa baada ya kuashwa kwa mishumaa 25 iliyoandaliwa, kama ishara ya miaka yake ya utume ambayo tayari amejikita nayo, hivyo mshumaa wa mwisho ulikuwa kama kiashiria cha kuanza na moja ya mwendelezo wa utume wa wito wake kwa Bwana. Kati ya nyimbo na utamadunisho wa watoto wa Utoto Mtakatifu, misa ilipendeza sana ambayo kama mshangwela alioongoza mwenyewe, japokuwa mahubiri yaliongozwa na Makamu Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Tanzania (TEC), Askofu Eusebius Nzigilwa wa Jimbo Katoliki la Mpanda Tanzania.

Katika mahubiri yake,  kwa kuongozwa na Masomo ya Siku, Askofu Nzigilwa wa Jimbo katoliki la Mpanda, alifafanua juu ya wito kwamba Yesu aliwambia mitume wake kuwa: "si ninyi mlionichagua mimi bali ni mimi niliye wachagua ninyi.” Kwa njia hiyo ni Mungu anayechagua. Na hakuna Mtu anayeweza sema mimi ninastahili kuwa padre. Mungu akikuchagua si kwamba wewe unastahili kuliko wengine wote uliowaacha nyuma, hapana. Na Mungu anapomwita kama Padre, hamwiti awe kwa ajili ya wokovu wake binafasi wa padre huyo, bali alichamchagua kwa ajili ya wokovu wa wale ambao Mungu alimtuma kwenda kuwahudumia watu," alisisitiza Askofu Nzigilwa. "Mungu anawachagua watu wake kama alivyo mchagua Musa aende kuwaokoa watu wake na si kwa ajili ya wokovu wa Musa, badala yake Mungu aliona shida za watu wa Israeli na kilio chao. Na  ndiyo alifanya hivyo huko Geita, kwa kuona mahitaji ya watu wake."

Askofu wa Mpanda kadhalika alisisitiza kuwa: "Hata Mungu alipomtuma mwanae Yesu Kristo, alitumwa kwa ajili ya wokovu wa watu duniani. Alimtuma ili wanadamu wapate wokovu." Askofu Nzigilwa kwa mifano iliyo hai, aliendelea kusisitiza kuwa "ukuhani sio jambo ndogo, maana ni wito na zawadi kubwa kutoka kwa Mungu. Ni vema kufahamu kwamba upadre ni fumbolisiloelewekwa kwa nguvu ya binadamu. Na utume wa Upadre una changamoto nyingi zinazoweza hata kuwakatisha tamaa, kwa njia hiyo ni wajibu kwa waamini kuwaombea." Na wakati huo huo Askofu Nzigilwa pia aliowaomba "mapadre kutambua kwamba pamoja changamoto hizo wanazokutana nazo Mungu awaachi kamwe!"

Mapadre wakati wa misa ya shukrani ya Upadre wa Askofu Kassala
Mapadre wakati wa misa ya shukrani ya Upadre wa Askofu Kassala

Askofu Nzigilwa akiendelea kudadavua zaidi katika masomo yaliyosomwa aidha alisisitiza jinsi ambavyo hata leo hii, watu wako kama enzi zile za nyakati.  Pamoja na Elia kuwahikishia kuwa kuna Bwana, watu wengi walimkataa na zaidi kufanya shauri la kutaka kumuua kwa sababu aliwaeleza ukweli baada ya kuwashinda manabii wa Uongo. Na kweli walifanya njama  za kumuondoa kwa sababu hawakuwa tayari kupokea ukweli." Askofu aliongeza kusema "hali hizi zilizoanza wakati wa Elia na leo hii zinaendelea. Watu wanakataa ukweli hadi kufikia kufanya shauri la kuondoa maisha ya walio wa kweli."

Hatimaye Askofu Nzigilwa alikumbusha jinsi ambavyo njia za Mungu zio nja zetu. “Njia zangu si njia zangu. Tengenezeni mazingira ya tulivu na kukutana na Mungu. Kama vile Malaika alivyompa Elia Mkate akala na kumwezesha  kutembea kwa siku arobaini hadi kukutana na Mungu na Yesu anajitambulisha kwetu kama Mkate wa uzima, na tumpokea Kristo Mkate wa uzima na sisi Mapadre tutakuwa na uhakika wa kusafiri mchana na usiku mpaka kuweza kukutana uso kwa uso na Mungu."

Askofu Flavian Kassala wakati wa Sinodi 2023 mjini Vatican
Askofu Flavian Kassala wakati wa Sinodi 2023 mjini Vatican

Kwa upande wa Askofu Kassala wakati wa kutoa salamu na shukrani kwa wote waliofika na waliowezesha siku hiyo mara baada ya misa Takatifu, aliwashukuru wote kwa kila mmoja kuanzia maaskofu, mapadre, watawa, wazazi, waamini na wageni kutoka nje na ndani ya nchi, wanasiasa na viongozi wote wa Serikali. Katika salamu hizo Askofu Kassala alimwambia Dk. Mwigulu ambaye tayari alikuwa amezungumza,  kwamba afikishe salamu na pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan kwa ushirikiano anao utoa na jitihaza zake za kuongoza Taifa. Lakini kufuatia na hotuba ya Waziri wa Fedha, Askofu Kassala aliomba serikali kuhakikisha kwamba inawashirikisha viongozi wa dini katika kuthimini na kushauri kuhusu masuala ya kodi ambayo ni maumivi kwa watu walio wadhaifu na wanyonge na wakati huo huo aliomba serikali pia itekelezea haraka msamaha wa kodi zilizotolewa katika taaasisi za kidini kwani wao hawafanyi biashara na kwamba mfumo liokuwepo ulisababisha maumivu kwa kutoza kodi bila kutazama huduma zitolewazo.

Askofu Kassala alisema: “Tunajua Rais ametangaza Tume Maalum inayoshughulika kuangalia masuala ya kodi, msiache kutushirikisha na sisi tukaweleza pale ambapo pana maumivu zaidi, hasa kwa walio wanyonge kuhusiana na suala la kikodi.”

Misa ya Shurani kwa miaka 25 ya Upadre wa Askofu Kassala
Misa ya Shurani kwa miaka 25 ya Upadre wa Askofu Kassala

Kwa upande wa mgeni Rasmi, Waziri wa fedha Mwigulu wakati wa kutoa neno, alizungumza kwamba serikali italiendea kuunga mkono uhuru wa kuabudu na kushirikiana na taasisi za dini katika ujenzi wa Taifa. Mwigulu alibainisha kuwa, kupitia hoja zilizotolewa na viongozi wa dini walipokutana na Rais Samia, imesababisha kufanywa marekebisho ya sheria ya mapato ya mwaka 2014 iliyowezesha taasisi za kidini kutambuliwa kama taasisi za hisani ambazo hazitengenezi faida yaani hazifanyi biashara. Na uamuzi huo unalenga kuzipatia nafuu kwa masuala ya kodi, kwa sababu ni taasisi ambazo hazifanyi biadhara, badala yake zinasaidia Serikali kwa mfano kwenye sekta za Afya, elimu  na nyinginezo.

Dk. Mwilgulu alisema: "Kuna maeneo ambayo Taasisi za dinia sinasaidia Serikali kama vile sekta ya Afya elimu na maneneo mengine kwa hiyo sheria yam waka 2024 tumeirekebisha na kuziwezesha taasisi za kidini kama taasisi za hisani zisizotengeneza faida, hivyo zitapata unafuu wa kodi ya mapato. Vile vile tumeruhusu taasisi za kidini zinazofanya miradi ya kijamii kama shule, hospitali kupata msamaha wa ongezeko la kodi pale zikapofanya shughuli hizo na zimeingia makubalinao na Serikali zikapokuwa zinatekeleza majukumu hayo."

Askofu Kassala wakati wa Sinodi 2023
Askofu Kassala wakati wa Sinodi 2023

Waziri Mwigulu kadhalika akiendelea na hotuba yake alitaja R nne za Rais Samia ambazo ni zinahusiana na maridhiano, ustahilimivu, mabadiliko na kujenga upya) kuwa: zimeleta makutokeo makubwa hasa kwa hali ya siasa ambapo maridhiano na ustahimilivu vimesababisha kuleta pamoja taifa. Kwa njia hiyo alitoa ombi na kusema: “Baba Askofu ninaomba muendelee kuombea hali ya aina hii iendele hivyo kutokana na utaifa wetu. Ni muhimu kuliko migawanyiko wetu na hatuwezi kwenda hatua kubwa mbele bila kuwa na umoja.” Kwa njia hiyo Waziri Mwigulu aliomba viongozi wa dini kushirikiana na Serikali ili kukemea pia ukatili wa kijinsia na imani za kishirikisha ambazo hazina faida kwa jamii. Na hatimaye alishukuru sana Utoto Mtakatifu ambao ulitumbuiza na kutamadunisha wakati wote wa misa Takatifu.

Jubilei ya Askofu Kassala Jimbo la Geita kutimiza maiaka 25 ya Upadre
12 August 2024, 10:35