Tafuta

Kardinali Robert Walter McElroy wa Jimbo la Mtakatifu  Diego,mji kwenye pwani ya Pasifiki ya California,Marekani. Kardinali Robert Walter McElroy wa Jimbo la Mtakatifu Diego,mji kwenye pwani ya Pasifiki ya California,Marekani.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

29 Septemba,Pax Christi Kimataifa itazindua Taasisi ya Kusitisha Vurugu

Taasisi hii ni Mpango Katoliki wa Kusitisha Vurugu wa Harakati ya Kikatoliki kimataifa ya Pax Christi.Tukio hilo litafanyika tarehe 29 Septemba 2024 katika Ukumbi wa Taasisi ya Maria Mtoto Mtakatifu(Santissima Bambina)Jijini Roma,Italia.Kardinali Maung Bo na McElroy ni kati ya watakaoongoza uzinduzi huo.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Taasisi ya Kikatoliki ya Kusitisha Vurugu itazinduliwa mnamo Dominika tarehe 29 Septemba 2024, katika ukumbi wa Taasisi ya Maria Mtoto Mtakatifu,(Maria Santissima Bambina), jiji Roma nchini Italia. Ni tukio litakalo ongozwa na Kardinali Charles Maung Bo kutoka Myanmar, Kadinali Robert McElroy kutoka Jimbo la Mtakatifu Diego, Califonia nchini Marekani, Sista Teresia Wachira kutoka Shirika la Bikira Maria na mwandishi na mtafiti mashuhuri Dk. Maria Stephan. Uzinduzi huo utatiririshwa kupitia viunga vya mtandaoni kwenye YouTube. Taasisi Mpya ya Kikatoliki ya Kutotumia Vurugu, asili yake ni kutoka katika Mpango wa Harakati ya Kikatoliki Kimataifa ya Pax Christi. Hii inalenga kuwezesha utafiti usio na vurugu, nyenzo na uzoefu kwa viongozi wa Kanisa Katoliki, Jumuiya na taasisi mbalimbali kwa lengo la kuimarisha uelewa wa Kikatoliki na kujitolea kwa desturi ya Injili ya kutotumia Vurugu.

Wataalimungu na watafiti wa masuala ya unyanyasaji wanaalikwa

Taasisi inawaalika wataalimungu, watafiti na watendaji wakuu wasio na unyanyasaji kama Washirika wa Taasisi wanaofanya kazi katika maeneo kama vile Uasi wa Injili, Matendo ya Kutotumia Ukatili na Nguvu za Kimkakati na Uzoefu wa Muktadha wa Kutonyanyasa. Wajumbe wa Baraza la Ushauri ni pamoja na Maria Clara Bingemer, Profesa wa Idara ya Taalimungu ya Chuo Kikuu Katoliki cha Kipapa cha Rio de Janeiro nchini  Brazili, Askofu Mkuu Peter Chong kutoka Fiji, na Erica Chenoweth, ambaye, kama Mkuu na Profesa katika Chuo Kikuu cha Harvard, mamlaka ya kwanza  ya juu ya kutokuwa na ukatili wa kimkakati.

Tuzo ya Pax Christi 2024 kwa:Tume ya Haki na Amani ya Haiti na mmisionari wa Wakarmeli wa Peru

Siku hiyo hiyo, hafla ya Tuzo ya Kimataifa ya Amani ya Pax Christi pia itatolewa. Tangu 1992, Harakati ya Kimataifa ya Pax Christi imekuwa mfadhili wa tuzo hiyo, ikitoa heshima kwa wanaume na wanawake wanaotetea amani, haki na kutokuwa na vurugu duniani kote. Mwaka huu 2024, tuzo hiyo itakwenda kwa Tume ya Haki na Amani ya Haiti, shirika lisilo la kiserikali lililojitolea kukuza utu na haki za binadamu. Tuzo hilo pia litatolewa kwa Sr. Gladys Montesinos, mmisionari wa Wakarmeli wa Peru ambaye amejitolea kwa miaka sita kusaidia watu wa asili mbalimbali katika Amazoni ya Bolivia.

Mwezi Oktoba semina za kujibu maswali kuhusu kutotumia vurugu

Baadaye, mwezi wa Oktoba na kama mchango wa mazingatio juu ya kutotumia nguvu yaliyotolewa na Mkutano Mkuu wa Kumi na Sita wa Sinodi ya Maaskofu, Taasisi ya Kikatoliki ya Kusitisha Vurugu itatoa semina ambazo zitajibu maswali yaliyoulizwa kuhusu kutotumia nguvu na kujilinda halali na malezi katika usimamizi wa migogoro isiyo na vurugu.

Kuhusu Taasisi ya Kikatoliki ya Kutotumia Vurugu

Taasisi ya Kikatoliki ya Kusitisha Vurugu, inayoanzishwa na Harakati ya  Kimataifa ya Kikatoliki  Pax Christi ni mpango  wa mnamo 2024 na yenye makao yake mjini Roma, ambayo inajitolea kuendeleza namna ya kukomesha vurugu kama fundisho kuu la Kanisa Katoliki. Dhamira yake ni kufanya utafiti, rasilimali,na uzoefu wa msingi katika kutokuwa na vurugu kufikiwa zaidi na viongozi wa Kanisa, jumuiya na taasisi duniani kote na hivyo kupunguza vurugu na kuimarisha kujitolea kwa Kanisa kwa kutotumia nguvu kama mazoea ya kila siku. Taasisi ya Kikatoliki ya Kutotumia Vurugu italeta uzoefu wa kutotumia nguvu kutoka pembezoni duniani kote katika mazungumzo na watafiti, Wataalimungu na viongozi wa Kanisa. Habari zaidi soma: www.paxchristi.net/catholic-institute-fornonviolence/

Kuhusu Harakati ya Kimataifa ya Pax Christi

Harakati ya Kimataifa ya Pax Christi  ni hatakati ambayo inafundisha kutotomia vurugu na lenye mashirika wanachama 120 duniani kote ambayo yanahamasisha amani, heshima ya haki za binadamu, haki, na upatanisho duniani kote. Kwa msingi wa imani kwamba amani inawezekana na kwamba mizunguko mibaya ya jeuri na ukosefu wa haki inaweza kuvunjwa. Kwa njia hiyo “Pax Christi International “inashughulikia sababu za msingi na matokeo haribifu ya migogoro na vita vikali. Kwa habari zaidi unaweza kubonyeza hapa: www.paxchristi.net

Kuhusu Mpango wa kikatoliki wa  Kutotumia Vurugu wa Pax Christi

Mpango wa Harakati ya Kikatoliki wa Kimataifa wa Pax Christi unathibitisha maono na desturi ya kutotumia nguvu katika moyo wa Kanisa Katoliki na umejitolea kwa wito wa muda mrefu wa uponyaji na kupatanisha watu na sayari. Kwa maelezo zaidi bonyeza hapa:www.paxchristi.net/cni-about-us

Kardinali MacElroy: 'Vurugu ni neno gumu sana...'

Kardinali McElroy wa Mtakatifu Diego akizungumza na Vatican News kuhusiana na suala zima hilo alisema “Ingawa Wakristo wamepambana na dhana ya vita vya haki tangu Mtakatifu Agostino kuweka misingi yake ya maadili katika karne ya 4, fundisho la vita vya haki haliwiani kamwe na ujumbe wa Injili, zaidi ya jinsi nadharia hii inaweza kuwa ya maadili kiufundi. Katika maisha ya Kanisa, nadharia za vita tu ni kipengele cha pili katika mafundisho ya Kikatoliki; kwanza ni kwamba tusijihusishe na vita hata kidogo. Mara nyingi, nadharia ya vita vya haki na tamaduni ni ambayo msingi wake umetumiwa kuhalalisha vita. Hili ni tatizo muhimu.” Katika suala hilo la kutotumia vurugu kardinali alieleza kwamba “vurugu ni neno gumu sana, kwa sababu kuna aina mbalimbali za vurugu duniani ambazo, zote ni kinyume na njia ya Injili katika kiini chake.”

Taasisi Mpya inatafuta kuzingatia mapambano mengi sana

Kardinali McElroy alithibitisha kwamba Taasisi ya Kutokuwa na Vurugu itatafuta kuzingatia mapambano mengi, vita vya wenyewe kwa wenyewe na vita katika mipaka ya kitaifa: “Inazidi kuwa muhimu kwamba Kanisa lishuhudie utafutaji wa njia mbadala za kutatua migogoro inapozuka, hata kama kujenga amani ni ahadi pana zaidi kuliko kumaliza migogoro.” Kwa hiyo, “amani si ukosefu wa vita tu, bali kwa hakika uondoaji wa migogoro huleta maelewano mapana zaidi na vipengele vya Injili, kujali utu wa binadamu na mshikamano kati ya watu. Mandhari haya mapana zaidi ni ya lazima kama sehemu ya ujenzi wa amani,  na ambayo yakazea mambo makuu lakini msingi ni kuweka kutotenda kwa jeuri katikati ya taalimungu  ya Kikatoliki juu ya vita na amani.”

Chuo cha Kusitisha Vurugu Pax Christi
26 September 2024, 16:00