Kardinali wa Angola Alexandre do Nascimento ameaga dunia
Vatican News
Amekuwa na maisha marefu, ambapo aliaga dunia akiwa katika mji mkuu wa nchi yake mnamo tarehe 28 Septemba 28024 kulingana na kile kilichoripotiwa na Jimbo Kuu la eneo hilo. Huyo ni Kardinali Alexandre do Nascimento ambaye alikuwa mmoja wa makadinali walioleta Kanisa la Afrika katika milenia mpya. Mwanamume ambaye pia aliona mwisho wa ujeuri usoni wakati tarehe 15 Oktoba 1982 alitekwa nyara akiwa katika ziara ya kichungaji na kundi la watu wenye silaha, ambao wakamwachilia huru tarehe 16 iliyofuata. Kwa ajili ya kuachiliwa kwake Papa Yohane Paulo II alikuwa amezindua wito katika Sala ya Malaika wa Bwana siku ya Dominika tarehe 31 Oktoba hiyo.
Askofu akiwa na Papa Paulo VI
Na Papa Wojtyla mwenyewe alikuwa amemthamini mtu huyo mwenye asili ya Malanje, ambako alizaliwa karibu karne moja iliyopita, tarehe 1 Machi 1925 na ambaye pia alisoma katika Chuo Kikuu cha Gregorian Roma, na kupata Shahada ya Kwanza ya Falsafa na Leseni katika Taalimungu na kisha akawekwa wakfu mwaka wa 1952. Papa wa Poland alimtunuku kofia ya ukardinali katika (Consistory)mkutano wa uchaguzi wa mnamo Februari 1983 lakini tayari kabla yake, mnamo Agosti 1975, Papa Paulo VI alikuwa amempandisha hadhi ya uaskofu, akimkabidhi jimbo lake la asili. Hapo awali alikuwa paroko, mwalimu, katibu mkuu wa Caritas ya kitaifa, rais wa Mahakama ya Kikanisa ya Luanda. Wakati wa Kwaresima 1984 pia alikuwa amehubiri mafungo ya kiroho mjini Vatican kwa ajili ya Curia Romana ambapo Mtakatifu Yohane Paulo II alikuwa ameshiriki. Akiwa askofu mkuu wa Luanda tarehe 16 Februari 1986, alitawala jimbo Kuu hadi tarehe 23 Januari 2001.