2024.09.10 Kardinali Pizzaballa huko Jenin kutembelea waamini. 2024.09.10 Kardinali Pizzaballa huko Jenin kutembelea waamini.  (Latin Patriarchate of Jerusalem)

Kard.Pizzaballa:Hamko peke yenu,majengo yatajengwa upya

Patriaki wa Kilatini wa Yerusalemu,Kardinali Pizzaballa alitembelea parokia ya Kilatini ya jiji la Ukingo wa Magharibi ambao kwa siku 10,limekuwa eneo la operesheni ya Israeli dhidi ya ugaidi."Kaeni kwa umoja na ustahimilivu na kukata tamaa sio chaguo zuri."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kardinali Pierbattista Pizzaballa, Patriaki wa Kilatini wa Yerusalemu, akitembelea Parokia ya Kilatini ya Jenin, alizungumza na waamini, huku akiwahakikishia kwamba majengo yaliyoharibiwa na operesheni ya hivi karibuni ya jeshi la Israeli yatakuwa na ujenzi mpya na kuitaka Jumuiya ya Kikristo ya Jenin na maeneo ya jirani iendelea kuwa na umoja na uvumilivu. "Hamko peke yenu licha ya nyakati ngumu, na kukata tamaa sio chaguo jema,"alisema Kardinali.

Kardinali Pizzaballa atembelea Parokia ya Jenin
Kardinali Pizzaballa atembelea Parokia ya Jenin

Patriaki, akifuatana na Monsinyo William Shomali, aliwasili  katika mji huo tarehe 10 Septemba 2024, ulioko Kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi, eneo linalojitawala kinadharia chini ya Mamlaka ya Kitaifa ya Palestina, ambayo kwa muda wa siku kumi ilikuwa eneo la operesheni ya wanajeshi wa Israeli. Katika taarifa kutoka Upatriaki wa Kilatini wa Yerusalemu, tunasoma kuwa, "Kardinali Pizzaballa alitembelea parokia ya Kilatini, ili  kutathmini uharibifu uliosababishwa na operesheni ya kijeshi.” Wakimkaribisha Kardinali na wajumbe waliofuatana naye, pamoja na Paroko wa Parokia ya mji huo, Padre Amer Jubran, mapadre, watawa na waamini wa parokia hiyo ambao pamoja na kueleza mahitaji na matumaini, pamoja na kuthamini msaada endelevu wa Patriaki, walimweleza Kardinali uharibifu mkubwa uliosababishwa na mali za Kanisa, pamoja na matatizo ambayo jumuiya sasa inajikuta. Na wao kwa hiyo walipokea maneno ya kuungwa mkono ya Patriaki huyo ambaye, mara baada ya mkutano huo uliofanyika katika eneo la Parokia, pamoja na ujumbe wake walipitia baadhi ya mitaa ya Jenin ili kujiridhisha wenyewe, kama inavyoeleza taarifa hiyo, "uharibifu ulioletwa operesheni ya kijeshi."

Kardinali Pizzaballa atambelea parokia ya Jenin
Kardinali Pizzaballa atambelea parokia ya Jenin

Jeshi la Israeli liliondoka Jenin mnamo Septemba 6 baada ya siku 10 za "operesheni ya kupambana na ugaidi", kama ilivyofafanuliwa na Israeli, muda mrefu zaidi katika eneo la mji na kambi ya wakimbizi, na wakati ambapo watu kadhaa waliuawa,  Wapalestina 21, kulingana na takwimu zilizotolewa na Wizara ya Afya ya PA. Tangu shambulio la Hamas tarehe 7 Oktoba 2023, zaidi ya Wapalestina elfu tano wamekamatwa na Israeli katika Ukingo wa Magharibi, ambapo zaidi ya elfu mbili wanaaminika kuwa na uhusiano na Hamas. Tena kulingana na Wizara ya Afya ya PA, zaidi ya Wapalestina 670 wameuawa katika Ukingo wa Magharibi katika miezi hii 11.

Kardinali Pizzaballa alitembelea Jenin

 

 

11 September 2024, 10:42