Kipindi cha kazi ya Uumbaji 2024 kilizinduliwa huko Assisi
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika siku ya kuanza kwa kipindi cha Kuombea Kazi ya Umbaji, mnamo tarehe 1 Septemba iliyopita, ambacho kitadumu, hadi tarehe 4 Oktoba, sambamba na Siku Kuu ya Mtakatifu Francis wa Assisi ilifanyika uzinduzi huo. Katika siku hiyo, matukio ya kufungua Kipindi cha Kazi ya Uumbaji iliandaliwa na wajumbe na wawakilishi wa Assisi wa Terra Laudato Si'. Katika siku hiyo, Antonio Caschetto, mkuu wa Kituo cha Harakati ya Laudato Si' alisema: “Katika wakati huu ulio na aina tofauti za kukata tamaa kutokana na dhuluma nyingi tunazoziona duniani, kila mmoja wetu anaitwa kujiuliza swali la maana. Tunajua tumesababisha uharibifu mkubwa kwa Uumbaji." Kwa upande mwingine, Caschetto aliendelea kusema, “katika moyo wa kila mmoja wetu Mungu amepanda mbegu, alitaka tutunze Uumbaji wake, tukikuza na kulinda bustani yake. Tunatumaini kwa dhati kwamba Kipindi hiki cha Uumbaji kitasaidia kuchanua kwa mbegu nyingi za matumaini kati ya washiriki na mahujaji wanaopitia Assisi".
Matukio ya kazi ya uumbaji
Programu ya matukio ya Siku ya kuombea kazi ya Uumbaji ilijumuisha hija, adhimisho la Ekaristi na mkutano wa maombi ya kiekumene. Pamoja na Askofu wa Assisi, Domenico Sorrentino, miongoni mwa wengine, Askofu Claudio Giuliodori, msaidizi wa kikanisa wa Chama cha Matendo ya Kikatoliki, walishiriki, na watu wengine wa kiekumene kama vile Askofu wa Kianglikani wa Willochra John Stead, shemasi wa Kanisa la Kiorthodox la Kiromania kwa ajili ya Umbría - Marche Petru Heisu, Marche, rais wa Baraza la Kanisa la Waaldensia la Perugia Antonella Violi; Shemasi Yousif Mina Stella wa Jumuiya ya Kanisa la Kikoptic la Kiorthodox la Gualdo Tadino, pamoja na meya wa Asisisi Stefania Proietti.
Mchakato wa kuleta furaha na juhudi
Kwa mujibu wa Caschetto, mkuu wa Kituo cha Laudato Si, alisisitiza kuwa "Siku ya kuombea kazi ya Uumbaji ilikuwa ya ajabu, iliishi kwa nguvu na hamu kubwa ya kujitolea kwa ulimwengu bora". Shughuli na uzoefu utakaoashiria kipindi hiki ni kuunganisha watu kutoka duniani kote katika safari ambayo imedumu kwa miaka mingi, ambayo imetufanya tuwe na wakati mzuri sana na wa kina na kutuona tukitarajiwa kuelekea siku zijazo. Hii inatoa furaha kwa juhudi za kupanga na kuhuisha, kuona kwamba hatuko peke yetu."