Tafuta

2024.09.12 Kongamano la V la Ekaristi Takatifu Nchini Tanzania. 2024.09.12 Kongamano la V la Ekaristi Takatifu Nchini Tanzania. 

Ask.Mkuu Ruwa'ichi:Kushuhudia imani ni jukumu la kila mmoja

“Kongamano la Ekaristi limeanza kwa Adhimisho la Misa ya Roho Mtakatifu ambaye ni msukumo na mwalimu wa imani yetu ya Kanisa Katoliki.Kila mmoja awe Mtume wa Kristo,aliyewapatia mitume nguvu ya Roho Mtakatifu kuwasaidia kumtangaza zaidi.Ni mahubiri ya Askofu Mkuu Ruwa'ichi katika ufunguzi wa Kongamano la V la Ekaristi Takatifu Kitaifa,Dar Es Salaam,Tanzania.

Na Tekla Revocatus -Radio Maria na Angella Rwezaula – Vatican.

Kongamano la VI la Ekaristi Takatifu  nchini Tanzania limezinduliwa Alhamisi tarehe 12 Septemba 2024 katika viwanja vya Msimbazi Centre,  Jimbo Kuu la Dar es Salaam na litahitimishwa tarehe 16 Septemba 2024. Katika Kongamano hilo la Kitaifa linaongozwa na kauli mbiu: “Udugu wa kuponya Ulimwengu: “Nanyi nyote ni ndugu,” kutoka kifungu cha Injili ya Matayo 23: 8, iliyochaguliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuongoza Maadhimisho ya Kongamano la 53 la Ekaristi Takatifu Kimataifa ambalo bado linaendelea huko Jimbo Kuu la Quito, nchini Ecuador, barani Amerika Kusini ambalo lilianza tangu tarehe 8 na litahitimishwa tarehe 15 Septemba 2024.

Ufunguzi wa Misa ya Kongamano la V la Ekaristi Kitaifa,Tanzania
Ufunguzi wa Misa ya Kongamano la V la Ekaristi Kitaifa,Tanzania

Kwa hiyo katika tukio la Jimbo Kuu la Dar Es Salaam, Askofu Mkuu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi wa Jimbo Kuu hilo  ambaye ni mwenyeji wa Kongamano hilo  na ambaye aliongoza Ibada ya Misa Takatifu kwa kuona ushiriki mkubwa wa maaskofu, mapadre, mashemasi, waseminari, watawa kike na kiume, waamini Watu wa Mungu wa Jimbo Kuu hilo, lakini pia wawakilishi mbalimbali kutoka majimbo yote Katoliki nchini Tanzania.

Kongamano la V la Ekaristi Takatifu Kitaifa,Tanzania
Kongamano la V la Ekaristi Takatifu Kitaifa,Tanzania

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam,  katika mahubiri yake  alisema kuwa “huwezi kushuhudia imani yako, pasipo nguvu ya Roho Mtakatifu ndani mwako na utayari wa kutenda.” Alisisitiza kuwa “Kongamano la Ekaristi limeanza kwa Adhimisho la Misa ya Roho Mtakatifu ambaye Roho Mtakatifu ni msukumo na mwalimu wa imani yetu ya Kanisa Katoliki.” Kwa njia hiyo  alimwalika “kila mmoja kuwa Mtume wa Kristo, ambapo mara baada ya kifo chake aliwashukia na kuwapa nguvu ya Roho Mtakatifu, nguvu iliyowasaidia kumtangaza zaidi kwa watu na hadi sasa tunaishuhudia Imani hiyo," Askofu Mkuu Tadeus. Kwa kuendelea  alisema kuwa: “Kushuhudia imani ni jukumu la kila mmoja, kwani Kristo alikufa na akaacha ukumbisho wa maisha yake ya Ekaristi Takatifu, hivyo tuwe na juhudi ya kuadhimisha Ekaristi Takatifu.”

Kongamano la V la Ekaristi Takatifu Tanzania
Kongamano la V la Ekaristi Takatifu Tanzania

Askofu Mkuu Askofu Mkuu Rwa’ichi akiendelea aliwaalika waamini waweke juhudi za kumpokea Roho Mtakatifu ndani ya mioyo yao, ili awasaidie kumtumikia Mungu na kuweza kuimba matendo yake Makuu kwa taifa kubwa la Mungu.” Vile vile, alisisitiza kila mmoja kwamba anapaswa kuienzi “Imani kwanza kwa kuziombea familia ili ziweze kusimama imara na kuchanua kama shule ya Imani na ushuhuda, kuliombea taifa la Tanzania na Ulimwengu mzima na mwisho Kumwombea Baba Mtakatifu na Kanisa lake, ili aliimarishe daima.”


Kongamano la V la Ekaristi Takatifu Kitaifa,Tanzania
Kongamano la V la Ekaristi Takatifu Kitaifa,Tanzania

“Tuadhimisha Imani yetu, tutoe ushuhuda wa imani, tuombe neema na baraka za Mungu kwa maisha yetu kama familia, Kanisa na taifa kwa ujumla. Kongamano la Ekarsiti tunaliadhimisha na kusherehekea imani yetu, ambaye ni Mungu pamoja nasi katika maumbo ya mkate na Divai," Askofu Mkuu Rwa’ichi.

Kongamano la V la Ekaristi Kitaifa,Tanzania
Kongamano la V la Ekaristi Kitaifa,Tanzania

Kwa kuhitimisha, Askofu Mkuu alisema kuwa: “kila mmoja anapaswa kusikiliza mada mbalimbali zilizoandaliwa ili ziwasaidie na mtakaporudi nyumbani na mzigo wa Neema zinazopatikana hapa kwenye Kongamano la Ekaristi Takatifu.” Hata hivyo baada ya adhimisho la Misa Takatifu aliwaalika waamini wote walioshiriki Kongamano hilo la Ekaristi Takatifu wajiandae vizuri kupokea mada zilizoandaliwa  na kwa hiyo “ziwe chimbuko la imani, upendo, uadilifu na utume katika Kanisa moja Takatifu Katoliki la Mitume.” Kwa siku hizi hadi tarehe 16 washiriki watajifunza mengi na pamoja na kuabudu Ekaristi Takatifu, kifungo kikuu cha Maisha yaliyotolewa Msabalani. Mada mbalimbali zimeanza kutolewa na wabobezi wa masuala mbali mbali ya Taalimungu, falsafa na kiroho.

Kongamono V la Ekaristi Kitaifa,Tanzania
Kongamono V la Ekaristi Kitaifa,Tanzania
Kongamano la V la Ekaristi Takatifu Kitaifa, Tanzania
12 September 2024, 15:13