Tafuta

2024.09.11 Makaribisho ya Papa huko Singapore 2024.09.11 Makaribisho ya Papa huko Singapore   (Vatican Media)

Kuwasili kwa Papa Francisko ni majarajio ya matumaini kwa Jumuiya za kidini za Singapore

Kabla ya Papa Francisko kuwasili nchini Singapore Jumatano,11 Septemba,viongozi kadhaa wa dini mbalimbali walielezea matumaini yao ya kuwepo kwa amani na mazungumzo ya kidini katika nchi hiyo ya Asia.

LiCAS News

Siku chache kabla ya ziara ya Baba Mtakatifu Francisko kuwasili nchini Singapore, Kituo cha Majadiliano ya Kidini na Kiekumene cha Jimbo Kuu la Singapore(AIRDECS) na Habari za Kikatoliki zilitafuta mawazo kutoka kwa viongozi wa dini mbalimbali kuhusu Baba Mtakatifu na msimamo wake wa mazungumzo ya kidini. Yafuatayo na mawazo ya viongozi hao kama yalivyochapishwa na Habari za Kanisa la Asia(LICAS).

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Kihindu

Bwan K. Sengkuttuva, mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Kihindu, alisema kuwa “wito wa Papa Francisko kwa waa\mini wote wa kukuza amani kwa kuheshimiana, bila kugeuzwa imani na vikwazo, umeonekana vyema na Wahindu wanaoishi nje ya nchi.” Sengkuttuva alizungumzia Papa Francisko katika ujumbe wake, kwamba “Kengele zimelia kwa sauti ya maelewano ya kidini kupitia mahubiri yake. Amesimamia hayo kama tiba ambayo ulimwengu unahitaji."

Mkuu wa Jumuiya ya Kiyahudi

Kwa mjibu wa Mordechai Abergel, Mkuu wa Jumuiya ya Kiyahudi, ya Singapore alisema “Jumuiya ya Wayahudi, inafarijika kusikia kuhusu ziara ya Papa Francisko nchini Singapore na kuongeza kuwa ziara hiyo "ni ya majaliwa kwa sababu itatuma ujumbe wa kuishi pamoja wakati wa kuongezeka kwa ghasia za kidini katika sehemu nyingi za dunia.” Mkuu wa Kiyahudi huyo alisema kuwa ziara ya Papa Francisko "bila shaka itaimarisha" uhusiano kati ya imani za Ibrahimu na dini mbalimbali nchini Singapore, ahadi ambayo Papa anajitolea kwa undani na kwa bidii.”

Rais wa Jumuiya ya Wazoroasti wa Parsi ya Kusini Mashariki mwa Asia

Naye Rais wa Jumuiya ya Wazoroasti wa Parsi ya Kusini Mashariki mwa Asia alisema, Papa amekuwa akisisitiza mara kwa mara mazungumzo ya kidini kama njia ya kukuza maelewano, heshima na amani kati ya imani tofauti. "Wazoroastria wanashiriki imani sawa katika kukuza mazungumzo ili kujenga madaraja, kupunguza mvutano,na kuhimiza juhudi juu ya usawa, haki ya kijamii, mazingira na masuala ya kibinadamu," alisisisitiza Bwana Hormuz E. Avari.

Shirikisho la Mabudha, nchini  Singapore

Kwa upande wa Seck Kwang Phing wa Shirikisho la Mabudha, nchini  Singapore alisema kwamba viongozi wa kidini kutoka dini mbalimbali walitambua uhitaji muhimu wa kutetea amani na upatanisho, jambo ambalo ni muhimu nyakati zote na ulimwenguni pote.  Uelewa huu ulisababisha kuanzishwa kwa Jumuiya ya Dini Mbalimbali katika Monasteri ya Phor Kark See mnamo 1949, muda mfupi baada ya Vita vya Kidunia vya pili. "Ziara ya Papa Francisko nchini Singapore hakika itahimiza na kuthibitisha kazi ya kujenga maelewano ya kidini katika taifa letu la kisiwa," alisema.

Shirikisho la Watao na Jumuiya ya Kidini ya Jain

Bwana Tan Thiam Lye wa Shirikisho la Watao na Bwana Kenal Kothari wa Jumuiya ya Kidini ya Jain, wote wawili walikubali kwamba ziara ya Papa Francisko nchini mwao "ingeongeza uelewano wa kidini, kuimarisha kuaminiana, na kuimarisha upatanisho wa kidini nchini Singapore."

Baraza kuu la Kiprotestanti nchini Singapore

Kwa upande wa Baraza kuu la Kiprotestanti nchini lilisali kwa ajili ya “kuendelea afya na hekima ya papa katika kuchunga jumuiya ya Kikatoliki ya ulimwenguni pote.”

Askofu wa Kilutheri 

Naye Askofu wa Kilutheri Lu Guan Hoe alisema uwepo wa Papa Francisko ni "baraka kubwa na ukumbusho wenye nguvu wa imani yetu ya pamoja na kujitolea kwa amani, umoja na huduma".

Mufti wa Singapore

Dkt. Nazirudin Mohd Nasir, Mufti wa Singapore kutoka Baraza la Dini la Kiislamu la Singapore, alimtaja Papa Francisko kama mtetezi mkuu wa kuishi pamoja kwa amani na alibainisha sifa ya Singapore kama ishara ya amani na maelewano. Dk. Nasir alirejea juu ya 'Hati ya Udugu wa Kibinadamu,' ambayo Papa Francisko alitia saini pamoja na Sheikh wa Al-Azhar, kama "mwendelezo wa juhudi za muda mrefu za Vatican kuimarisha uhusiano na jamii ya Waislamu."

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Sikh

Naye Malminderjit Singh, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Asikh, alisisitiza kwamba "imani ya Sikh imejitolea kukuza amani ya dunia na kusaidia wengine, maadili ambayo Papa Francisko ametetea na kuimarisha katika kazi yake yote ya maisha."

Mwenyekiti wa Bunge la Kiroho la Wabaha’í wa Singapore

Bwana  K Elango, Mwenyekiti wa Bunge la Kiroho la Wabaha’í wa Singapore, alisema ziara ya Papa "inatarajiwa kuongeza juhudi za ushirikiano za watu wenye mapenzi mema kutoka kwa jumuiya mbalimbali, taasisi, na vikundi vya kidini kote Singapore."

13 Septemba,Papa atakutana na viongozi wa vina wa dini mbali mbali wa Singapore

Katika ratiba ya Papa Francisko, tarehe 13 Septemba 2024, anatarajiwa kukutana na viongozi wa vijana kutoka dini na imani mbalimbali nchini Singapore. Jimbo kuu la Singapore liliandaa toleo la mada: "Vijana wa kidini pamoja na Papa Francisko", na lifuatiwa na maonesho ya sanaa ambayo yatafanyika katika Chuo cha Kikatoliki cha Vijana.

Maoni ya viongozi wa dini kuhusu zira ya Papa Singapore
11 September 2024, 14:05